Jumatano, 21 Februari 2018
Jumanne, 20 Februari 2018
Waziri Prof. Ndalichako aziagiza Taasisi za Elimu kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria za nchi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako amezitaka Taasisi zinazotoa Elimu ya Juu hapa nchini kufuata
taratibu, Sheria na kanuni za nchi katika kuendesha Taasisi hizo.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii leo jijini Dar es
Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika Chuo Kikuu cha Kampla kilichopo
Gongo la Mboto ambapo amebaini kuwepo
kwa idadi kubwa ya watumishi ambao hawana vibali vya Makazi na Ajira.
Waziri Ndalichako amesema Chuo hicho kumekuwa na
udanganyifu wa taarifa za kiutumishi ambapo watu walioajiriwa kama madereva na
wahudumu wamekuwa wakiingizwa katika orodha ya watumishi ambao ni Walimu huku wakijua watumishi hao
hawana sifa za kuwa Walimu.
Waziri Ndalichako amesema baadhi ya walimu katika chuo
hicho kutoka nje ya nchi wanakuja kama wanafunzi lakini wakifika Chuoni hapo
wanahalalishwa na kuwa walimu ambao wanafundisha wanachuo bila kuwa sifa
stahiki.
Profesa Ndalichako pia amekitaka chuo hicho kuhakikisha
kinafuatilia kwa karibu nidhamu ya wanafunzi wanaosoma Chuo hapo kwa
kuhakikisha wanazingatia na kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi.
“Nidhamu ni jambo la
msingi sana, sasa hakikisheni wanafunzi wanaomaliza katika chuo hiki wanakuwa
na nidhamu ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu za ndani na nje ya nchi na siyo vinginevyo, maana kuna
baadhi ya wanafunzi ambao nyaraka zinaonyesha wamemaliza kwenye Chuo hiki na
wako nje ya nchi lakini hawana maadili, liangalieni hili kwa umakini,”alisema
Profesa Ndalichako.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna
Makakala amezitaka Taasisi zote za Elimu
nchini kuhakikisha zinatoa ushirikiano kwa ofisi hiyo ili kuepuka kukiuka
taratibu na miongozo iliyowekwa na nchi.
Jumatatu, 19 Februari 2018
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA
Nimepokea
kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya kifo cha Akwilina Bafhata Akwiline aliyekuwa mwanafunzi wa
mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Kifo
hicho kimetokea wakati askari wakiwa wanadhibiti maandamano yaliyokuwa
yakifanyika tarehe 16/02/2018 kwenye eneo la Mkwajuni Wilaya ya kinondoni,
jijijini Dar es salaam.
Napenda
kutumia fursa hii kutoa pole sana kwa Familia ya Ndugu, jamaa na marafiki wote wa Akwilini. Pia napenda kutoa pole kwa Uongozi na Jumuia
ya Chuo cha Usafirishaji, wanafunzi wote nchini na wananchi wote kwa ujumla.
Ndugu
Akwilini ni binti aliyekuwa anatambua na kuthamini umuhimu wa Elimu, na
alijitoa kuhakikisha kuwa anasoma kwa bidii kwa manufaa yake binafsi, familia
yake na kwa manufaa mapana ya taifa taifa.
Kifo chake kimetokea wakati akiwa kwenye kutekeleza wajibu wake kama
mwanafunzi wa kupeleka barua mahali alipokuwa anatarajia kufanya mazoezi kwa
vitendo yatakayoanza tarehe 27/02/2018. Kifo hicho cha kusikitisha kimezima
ndoto yake Serikali ikekipokea kwa masikitiko makubwa sana.
Mhe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli
amesikitishwa na kuhuzunishwa sana na
kifo cha mwanafunzi Akwilini na anaungana na familia, ndugu jamaa na watanzania
wote kuwapa pole za dhati kutokana na msiba huo.
Serikali
inatumia fedha nyingi kuwasomesha wanafunzi kuanzia Elimu msingi, sekondari na
hutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kwa sababu tunatambua mchango wa Elimu
katika maendeleo ya nchi yetu. Marehemu Akwilini alikuwa ni miongoni mwa
wanufaika wa Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Mimi
Waziri mwenye dhamana ya sekta ya Elimu nimesikitika sana kuona binti
huyo amepoteza maisha yake akiwa katika kutekeleza shughuli za kielimu.
Wizara
yangu itagharamia shughuli zote za mazishi ya Marehemu Akwilina hadi hapo
atakapopumzishwa katika makao yake ya milele.
Namuagiza
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo kusimamia
shughuli zote za msiba huo hadi Akwilina
atakapozikwa katika nyumba yake ya milele.
Nitumie
fursa hii kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwafikisha mara moja wahusika
waliosababisha kutokea kwa tukio hilo kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi
yetu.
Nawasihi
sana watanzania wenzangu tujiepushe kukiuka tarataibu na miongozo inayokuwa
inatolewa ikiwemo maandamano na vitendo
vyote ambavyo vinaweza kusababisha maafa kwa watu wasio na hatia.
Mungu
aiweke roho ya Marehemu Akwilini mahala pema peponi Ameni
Imetolewa
na:
Prof
Joyce Lazaro Ndalichako
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia.
18 /
02/2018
Katibu MKuu Akwilapo: awataka watumishi wa wizara yake kufanya kazi lea bidii na weledi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amewataka
watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu
yao ya kila siku.
Dk.
Akwilapo ameyasema hayo wakati wa kikao cha kwanza cha watumishi wa wizara hiyo
kilichofanyika mkoani Dodoma tangu serikali itangaze rasmi kuhamishia makao
makuu ya nchi mkoani humo.
Dk.
Akwilapo amesema utii, ushirikiano,bidii na upendo mahali pa kazi miongoni mwa
watumishi ndiyo silaha pekee ya kufikia malengo ambayo Wizara imejiwekea katika
kuinua Sekta ya Elimu hapa nchini.
"Nipende
kuwapongeza watumishi wote kwa kushiriki majukumu mbalimbali ya Wizara ikiwemo
kuisimamia vyema miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara, nawasihi sana
tuusifanye kazi kwa kujitenga, ushirikiano miongoni mwetu ni jambo la msingi
sana na tukiwa na Umoja basi mafanikio lazima yatapatika katika Sekta hii ya
Elimu,"alisema Dk.Akwilapo.
Pia
Katibu Mkuu Dk.Akwilapo amewataka watumishi kuwa na matumizi sahihi ya
Teknolojia,kujibu barua mbalimbali kwa wakati pamoja na kushughulikia faili
zinazofika kwenye ofisi zao ndani siku mbili
na siyo kuziacha zikae muda mrefu.
Kupitia
kikao hicho watumishi pia walipata fursa ya kuwaaga viongozi ambao walitumikia
Wizara hiyo ambao hivi sasa wamehamiahiwa Wizara nyingine na kuwakaribisha
viongozi wapya ambao wamehamia kwenye Wizara hiyo.
Viongozi
waliokaribishwa ni pamoja na Naibu Waziri William Ole Nasha na Naibu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe na walioagwa ni Naibu Waziri
Mhandisi Stella Manyanya na Profesa Saimon Msanjila ambaye hivi sasa ni Katibu
Mkuu anayesimamia Sekta ya Madini.
Alhamisi, 15 Februari 2018
TBA yatakiwa kulipa madeni ya wananchi katika ujenzi shule ya wavulana Ihungo
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakala wa majengo nchini TBA
kulipa madeni wanayodaiwa na Wananchi mbalimbali kufuatia ujenzi unaoendelea wa
Shule ya Sekondari wavulana Ihungo iliyopo Wilayani bukoba mkoani kagera.
Waziri Ndalichako amesema kuwa tayari
wizara imekwisha ilipa TBA zaidi ya bilioni Tisa na garama ya ujenzi kwa
mradi wote ni shilingi bilioni 10 nukta 48.
" Mnyonge mnyongeni haki yake
mpeni, nipende kuwapongeza Wakala wa Majengo TBA kwa kazi nzuri ambayo
wameifanya.
"Lakini nasikikitika sana
kupokea malalamiko kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa inayoeleza kuwa bado kuna
Wananchi wanaidai TBA kutokana na kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile
mbao, matofali, na vibarua ambao wameshiriki katika ujenzi huo wa shule ya
wavulana Ihungo na kuwa mpaka sasa hawajalipwa, hii haipendezi ni vyema TBA
kuhakikisha inalipa madeni hayo,"alisema Waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako amesema haoni
sababu kwa nini wananchi hawajalipwa wakati tayari Serikali imekwisha ilipa
TBA, ni vyema wakalipwa ili kusaidia kuepusha migogiro isiyo ya lazima baina ya
Serikali na wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa TBA mkoa
wa Kagera Salum Chanzi amekiri kuwepo kwa sababu mbalimbali zilipelekea
mradi kutokamilika kwa wakati na hivyo kuomba wapewe muda zaidi mpaka mwezi
machi mwaka huu ili waweze kukamilisha.
"Mheshimiwa Waziri mradi huu
haijakamilika kwa wakati uliokuwa umepangwa kutokana na changamoto ya kuagiza
vifaa kutoka nje ya mji wa bukoba, na hii inatokana na bei wakati mwingine kuwa
kubwa hapa bukoka lakini nje ya hapa tunavipata kwa bro nafuu,"
alisema Chanzi.
Chanzi amemhakikishia Waziri Ndalichako kuwa tayari madeni yote
wanayodaiwa na wananchi katika ujenzi huo wa Ihungo Sekondari yamewasilishwa
kwenye Taasisi yake yanafanyiwa kazi na wahusika wote watalipwa.
CHINESE GOVERNMENT SCHOLARSHIP APPLICATION FOR 2018/2019
The general public is hereby
informed that the 2018/2019 Chinese Government Scholarship is now open for
application. Online application and
corresponding application documents should be submitted to application
receiving agency not later than April 1st, 2018. For more information, please refer to http://www.csc.edu.cn/studyinchina or www.campuschina.org
Step 1: Visit http://www.csc.edu.cn/laihua or www.capuschina.org and click “Scholarship Application Online for International Students”.
Eligibility:
To be eligible, applicants
must
·
Be citizen of a country other than the
People’s Republic of China, and be in good health;
·
Be a high school graduate under the age of 25
when applying for master’s programs;
·
Be a bachelor’s degree holder under the age
of 35 when applying for master’s programs;
·
Be a master’s degree holder under the age of
40 when applying for doctoral programs;
·
Be under the age of 45 and have completed at
least two years of undergraduate study when applying for general scholar programs;
·
Be a master’s degree holder or an associate
professor (or above) under the age of 50 when applying for senior scholar
programs.
Application
Documents
a)
Application Form for Chinese Government
Scholarship (in Chinese or English);
b)
Certified highest diploma: Prospective
diploma winners must submit official proof of student status by their current
school. Documents in languages other
than Chinese or English must be attached with certified Chinese or English
translations;
c)
Academic transcripts: Transcripts in languages other than Chinese
or English must be attached with certified Chinese or English translations;
d)
A Study Plan or Research Proposal in Chinese
or English. (A minimum of 200 words for
undergraduates, 500 words for non-degree students, and 800 words for
postgraduates);
e)
Recommendation letters: Applicants for graduate programs or senior
scholar programs must submit two letters of recommendation in Chinese or
English from professors or associate professors;
f)
Applicants for music studies are requested to
submit their own works. Applicants for
fine arts programs must submit their own works which include two sketches, two
color paintings and two other works;
g)
Applicants under the age of 18 should submit
the valid documents of their legal guardians in China; and
h)
Applicants planning to stay in China for more
than 6 months must submit a photocopy of the Foreigner Physical Examination
Form completed in English (the original copy should be kept by the
applicant. The form designed by the
Chinese quarantine authority can be downloaded from http://www.csc.edu.cn/studyiinchina or www.campuschina.org. The physical examinations must cover all the
items listed in the Foreigner Physical Examination Form. Incomplete records or those without the
signature of the attending physician, the official stamp of the hospital or a
scaled photograph of the applicants are invalid. Please select the appropriate time to take
physical examination as the result is valid for only 6 months.
Please
submit the following documents where applicable
i)
Pre-admission Letter from Chinese Government
Scholarship universities; and
ii)
Language qualification certificate. E.g., HSK
certificates, IELTS or TOFEL report.
ONLINE
APPLICATION OF THE CHINESE GOVERNMENT SCHOLARSHIP INFORMATION SYSTEM
Step 1: Visit http://www.csc.edu.cn/laihua or www.capuschina.org and click “Scholarship Application Online for International Students”.
Step 2: Read “Tips for online application” carefully
before clicking “NEXT” to the
registration page.
Step 3: Log in with your user name
and password. For new user, please click
“Create an account” for registration.
Step 4: Fill in the correct Program Category and
Agency Number. An Agency Number
represents a specific application receiving agency and a correct choice of
Program Category is necessary before filling in the Agency Number. Please make sure you fill it in correctly,
otherwise you will not be able to continue your online application or your
application will not be accepted.
Your
‘Program Category’ is:
Type A and Agency Number is:
8341. Once the correct
‘Agency Number’ is entered, the name of the agency will automatically emerge.
Step 5: Fill in the Online Application Form and Upload Supporting Documents truly,
correctly and completely following the steps listed on the left of the page.
Applicants
are required to select a discipline before choosing their majors. Please refer to the Disciplines Index, which
could be downloaded from help, if you have any doubt about the disciplines and
majors.
Step 6: Check
each part of your Application carefully
before submitting it. Click Submit to submit your Application. The submitted documents will be the only
reference for the applied universities to confirm the admission.
Step 7: You can make changes to your
application by clicking Withdraw and Edit the Application on the top of the
page. But make sure to submit it again
by clicking Submit after finishing all the changes. Otherwise, the retrieved application will
become invalid and your new application will not be received either.
Step 8: You can download and print
the completed Application Form by
clicking Print the Application Form.
Step 9: Send the paper application
form and other supporting documents to the dispatching authorities if they
require you to do so.
Please
note that only Chinese and English are accepted for the online application.
Kindly
submit your application to the undersigned not later than 1st April,
2018
Executive Secretary,
Tanzania Commission for Universities,
Mlimani Tower, Sam Nujoma Road,Opposite Mliman City,
P. o Box 6562, Dar es Salaam-Tanzania.
Waziri Ndalichako :Maafisa Elimu Nchini fuateni Sera na Miongozo inayotolewa na Wizara
Maafisa Elimu nchini
wametakiwa kufuata miongozo na sera inayotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia wakati wa kutekeleza majukumu yao na endapo watakiuka maelekezo hayo
wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa Wilayani
Muleba mkoani Kagera na kusema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya
Maafisa Elimu kupeleka wanafunzi wengi kwenye shule kuliko uwezo wa shule.
Waziri Ndalichako amesema
kuwa hali hiyo inachangia kuwepo kwa matokeo mabaya na hivyo amewaagiza
wathibiti ubora wa shule nchini kukagua shule zote ili kuondoa changamoto hizo.
Katika ziara hiyo Waziri
Ndalichako pia ametembelea na kukagua shule ya Sekondari ya Profesa Joyce
Ndalichako iliyoko Wilayani Muleba ambapo amewaagiza walimu wa shule hiyo
kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanafanya vizuri kitaaluma.
" Walimu hii shule
imebeba jina langu, nawaomba sana matokeo ya shule hii yaendane na Mimi
mwenyewe kwa maana ya wanafunzi kufanya vizuri na Wizara itahakikisha
inazipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zilizopo katika shule hii,"
alisema Waziri Ndalichako.
Katika ziara hiyo Waziri
Ndalichako alitembelea na kukagua Chuo cha Ualimu katoke, shule ya Sekondari
Anna Tibaijuka zilizopo Wilayani Muleba.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)