Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako ameigiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi(VETA) kuhakikisha inapeleka fedha kwa wakati katika ofisi za Kanda na
Vyuo vya Wilaya na Mikoa ilikuharakisha
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Mamlaka hizo.
Waziri
Ndalichako ametoa agizo hilo akiwa ziarani mkoani Katavi ambapo amesema VETA
kanda, Mikoa na Wilaya zimekuwa na changamoto za kujiendesha kutokana na
kutokuwa na fedha za kutosha.
Waziri, Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifalishwa skafu na Mwanafunzi wa Chuo cha
VETA Mpanda ikiwa ni ishara ya
kumkaribisha katika Chuo hicho. Waziri Ndalichako aliwashauri vijana na
wanafunzi kujiunga katika vikundi vya skauti ili kujiepusha na kujiingiza
katika makundi hatarishi
Amesema amesikitishwa kuona baadhi ya mitambo
katika Chuo cha VETA Mpanda iliyonunuliwa kwa gharama kubwa na Serkali haifanya
kazi kwa kukosekana fedha kidogo za ufungaji wa mitambo hiyo katika karakana za
chuo hicho .
“Ukiangalia
VETA za mikoani na wilayani zinahitaji fedhak kidogo tu ili zipige hatua lakini
hazitolewi, naagiza VETA Makao Makuu kuhakikisha katika mipango yenu mhakikishe
mnaweka usawa wa upelekaji fedha kwa VETA zote nchini ili nazo ziweze kupiga
hatua katika kutoa mafunzo,”amesema Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua baadhi ya mitambo katika moja ya
karakana za Chuo cha VETA Mpanda alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya
Elimu katika Mkoa wa Katavi. Waziri ameitaka VETA Makao Makuu kuhakikisha mitambo
yote katika Vyuo vya Wilaya na Mikoa inafanya kazi .
Katika
hatua nyingine Waziri Ndalichako ameahidi kutoa cherehani mbili kwa wanafunzi
Gift Giles na Benitha William wwenye umri wa miaka kumi na tano ambao
wamejiunga katika Chuo cha VETA Mpanda baada ya kutokuchaguliwa kuendeleana
masomo ya kidato cha kwanza.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makala amenuahidi Waziri kuwa
atakisimamia Chuo cha VETA Mpanda ili kiweze kuwa na tija kwa wanakatavi.