Jumatano, 17 Aprili 2019


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY

 STUDY OPPORTUNITY TENABLE AT CENTRE FOR INNOVATIVE DRUG DEVELOPMENT AND THERAPEUTIC TRIALS FOR AFRICA (CDT-AFRICA), ADDIS ABABA UNIVERSITY ETHIOPIA 2019/2020

Call for Application
The General Public is hereby invited to apply for Postgraduate Scholarships tenable at; The Centre for Innovative Drug Development and Therapeutic Trials for Africa (CDT-Africa) which is a World Bank supported Africa Centre of Excellence for Higher Education and Research at the College of Health Sciences, Addis Ababa University, Addis Ababa, Ethiopia. The Centre aims to improve access to health care through novel medical discoveries (medicines, vaccines, diagnostics, care delivery mechanisms) supported by clinical trials. CDT- Africa is one of the centres in a World Bank supported, multi county project titled “The African Centres of Excellence-II” which Tanzania is a partner country to ACE II therefore eligible candidates are strongly encouraged to apply.

Mode of Application
Application information is available at thelink:

Submission
Application package should include copies of; Curriculum Vitae(CV), Official Transcript, Degree Certificates, A motivation letter, and Birth Certificate. All these documents must be submitted as electronic copy to Dr.TsegahunManyazewal (Email: tsegahunm.cdtafrica@gmail.com) with a copy of the submission availed to Ms SamrawitKetema (Email: samryket@gmail.com)

Application must be submitted not later than 15th May 2019.

Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,P .O. Box 10, 
40479 DODOMA.

Jumapili, 14 Aprili 2019

HESLB SASA YATOA ELIMU UOMBAJI MIKOPO SHULENI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanza kuendesha programu za elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari waliopo mikoani ili kuwaelimisha kuhusu sifa na taratibu za kuomba mikopo kwa usahihi.

Akizungumza wilayani Maswa, mkoani Simiyu na wanafunzi 1,166 wa kidato cha sita kutoka shule zote 12 za mkoa huo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema uendeshaji wa programu hizo unalenga kuondokana na changamoto wanazopata wanafunzi wakati wa kuomba mikopo ya elimu ya juu. HESLB ilianza kuendesha programu hizo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wanafunzi hao wapo katika kambi iliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha sita inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa Mei. Kambi hiyo ipo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu Dkt. Seif Shekalaghe akiongea katika mkutano kati ya HESLB na wanafunzi 1,166 wa kidato cha sita kutoka mkoa wa Simiyu. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru. HESLB inaendesha programu za elimu ya uombaji mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa kidato cha sita nchini kote.
“Uzoefu wetu na maoni ya wadau wetu umetufanya tuanzishe programu hizi nchini kote ili wakati wa kuomba mikopo, muombe kwa usahihi na wale wenye sifa wapate na hatimaye kutimiza ndoto zao,” aliwaambia wanafunzi hao na kueleza kuwa kuanzia kesho (Aprili 15, 2019) maafisa wa HESLB watakua katika shule mbalimbali mikoani kutoa elimu hiyo.

Katika mikutano hiyo, wanafunzi wanaelezwa kuhusu sifa, nyaraka muhimu zinazotakiwa, namna ya kuomba na kuwasilisha kwa usahihi kwa njia ya mtandao na utaratibu na umuhimu wa kurejesha mkopo mara wamalizapo masomo. Katika programu hizi, wanafunzi pia hupata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi.
Mwanafunzi Casto Nyakalungu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Binza, mkoani Simiyu akiuliza katika mkutano kati ya wanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule 12 za mkoani humo na maafisa wa HESLB waliofika kutoa elimu kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mkopo.
Kwa mujibu wa Badru, katika mwaka wa masomo 2018/2019, kati ya waombaji wa mikopo zaidi ya 57,000 ambao walipata udahili vyuoni, maombi zaidi ya 9,000 yalikua na upungufu mkubwa ikiwemo kukosa nyaraka kama vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho sahihi vya wadhamini, kutosainiwa na waombaji, wadhamini au serikali za mitaa au vijiji.

Akizungumza na wanafunzi hao, Afisa Mikopo Mwandamizi kutoka HESLB Daudi Elisha aliwasihi wanafunzi hao kusoma kwa makini mwongozo utakaotolewa na HESLB mwezi ujao ambao utaeleza hatua kwa hatua kuhusu uombaji wa mkopo.

“Kuna baadhi ya waombaji wa mikopo huwa na haraka, mwezi ujao tukianza kupokea maombi, tutatoa mwongozo kwa lugha ya kiswahili na kiingereza, ninawasihi mtulie na msome kwa makini, msiwe na haraka kwa kuwa mtakuwa na miezi zaidi ya miwli ya kuomba,” alisema Elisha na kuongeza:
Afisa Mikopo Mwandamizi wa HESLB Daudi Elisha akiongea wilayani Maswa jana  na wanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule za mkoa wa Simiyu kuhusu sifa na utaratibu wa kuomba mikopo ya elimu ya juu.
“Hivi vipeperushi tunavyowapa vina maswali na majibu 21 ambayo nayo yanawaeleza hatua kwa hatua, mkisoma na kuzingatia, naamini wale wenye sifa watafanikiwa,” alisema Elisha.

Akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe aliishukuru HESLB kwa kutambua changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na kuamua kuzitatua.

“Sisi kama mkoa, tunawashukuru sana kwa kuwa jitihada zetu za kuongeza ufaulu hazitakua na faida kubwa kama vijana masikini watafaulu halafu wakashindwa kutimiza ndoto zao kwa kukosa mkopo … hii ni programu nzuri sana,” amesema Dkt. Shekalaghe.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watanzania wasio na uwezo na pia kukusanya mikopo iliyoiva iliyotolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.

Jumamosi, 13 Aprili 2019

SERIKALI KUJENGA SEKONDARI NA CHUO CHA UFUNDI DODOMA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kujenga shule ya Sekondari  na  Chuo cha Ufundi katika jiji la Dodoma ili kutoa fursa za elimu kwa wakazi wa jiji hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mji wa kiserikali jijini Dodoma Rais wa Jamhuri wa Muungano  wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli amesema shule hiyo ya sekondari itakayojengwa kwa Sh. Bilioni 13 itachukua wanafunzi wa  kidato cha kwanza hadi cha sita.
 
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na watumishi wa serikali wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.
Rais Magufuli ameongezea kuwa  Sh Bilioni 18 pia zitatumika kujenga Chuo kipya kikubwa cha ufundi kitakachotoa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali jijini Dodoma.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Dodoma kuhakikisha wanatumia vyema taasisi hizo za elimu katika kuwapatia maarifa vijana wao kwa maendeleo ya Dodoma na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waliofika Jijini Dodoma kuhdhuria uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba ambapo Ofisi za Serikali zimejengwa.
Rais Magufuli amezindua mji wa kiserikali katika eneo la Mtumba jijini Dodoma ambapo majengo hayo yatatumiwa  Wizara mbalimbali na baadhi ya Taasisi.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Mbalimbali  wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Wizara Mbalimbali  wakati wa uzinduzi wa Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.

WAZIRI NDALICHAKO AMUAGIZA KAMISHNA WA ELIMU KUREJESHA MAFUNZO YA UFUNDI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemuagiza Kamishna wa Elimu kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 mafunzo ya ufundi yanaanza kutolewa kikamilifu katika shule saba za ufundi ambazo Serikali imezikarabati.

Pia amemuagiza kuhakikisha ifikapo 2020 michepuo inayoendana na mwelekeo wa Serikali kama kilimo inaanza kufundishwa lakini pia kuwepo na somo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa tahasusi za wanafunzi wa kidato cha tano.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia panya ambao wana uwezo wa kubaini vimelea vya ugonjwa wa TB wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine Mkoani Morogoro wakati wa kufunga wiki ya kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine
Waziri Ndalichako ametoa maagizo hayo mkoani Morogoro wakati wa kufunga Wiki ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine ambapo amesema tukitaka watoto wetu waweze kuingia katika soko la ushindani hatuwezi kuacha nyuma masomo hayo.

Profesa Ndalichako aliongeza kuwa Serikali imetumia takribani shilingi bilioni moja kukarabati shule hizo za ufundi na kwamba ni vyema zikaanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi ili nchi iweze kuneemeka na matunda ya utaalamu wa wanafunzi hao pindi watakapomaliza.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo ya namna mashine za kuvunia mpunga zinavyofanya kazi kutoka kwa mtaalamu anayesimamia mashine kutoa Chuo Kikuu cha Sokoine.
Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ameeleza kufurahishwa na namna Chuo Kikuu cha Sokoine kinavyoendelea kumuenzi na kumpa heshima kubwa Hayati Edward Moringe Sokoine ambaye alikuwa shujaa, mchapakazi, mzalendo na mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia Taifa na kwamba mpaka mauti yanamkuta alikuwa kazini.

“Tuna wajibu wa kuyaishi mazuri ambayo yamefanywa na kiongozi huyu, SUA nafurahi kuona mnawashirikisha wanafunzi katika midahalo hii ni vizuri wakajua Taifa limetoka wapi, nchi hii imetulia kwa kuwa kuna watu walifanya kazi usiku na mchana ya kujenga amani, umoja na mshikamano ni rahisi sana kufanya kitu kimoja cha kuvuruga amani na mshikamano lakini ikivurugika kuijenga inaweza kuchukua karne kuirudisha kwa hiyo tuendelee kuwaenzi waasisi wa Taifa hili kwa kuyaishi waliyoyafanya,”  alieleza Waziri Ndalichako.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inatambua kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ajira zao ni kilimo na katika kuenzi mazuri yaliyofanywa na Hayati Edward Moringe Sokoine Serikali imeendelea kukiimarisha Chuo kikuu cha Sokoine ikitambua kilimo bora kinatakiwa kuwa na utaalamu bora.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia shamba darasa la zao la zabibu lililopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine mkoani Morogoro.
Kufuatia umuhimu huo Serikali imetumia zaidi ya bilioni 2 kujenga na kununua vifaa vya maabara ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Sokoine yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400, pia katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali imetoa fedha zaidi ya shilingi billioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa maabara mtambuka pamoja na bweni la wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 700 pindi litakapokamilika.

Pia kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia Chuo kimepatiwa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha maabara ya udongo itakayowasaidia wakulima kujua aina ya udongo na mazao yanayostahili kupandwa kwani wakati mwingine mazao yanaweza yasiwe na tija kwa sababu wakulima wanajipandia bila ya kuwa na utaalamu wa kujua afya ya udongo na kile kinachostawi na kupelekea kuathiri uzalishaji.

Wakizungumzia utendaji wa Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa uhai wake baadhi ya viongozi waliowahi kufanya nae kazi akiwemo Mhe. Getrude Mongela na Mzee Paul Kimiti walisema Kiongozi huyo alikuwa mchapakazi, muadilifu na mzalendo aliyetumia muda wake kuipigania nchi yake bila kuchoka.


 Muonekano wa shamba darasa la zao la zabibu lililopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine mkoani Morogoro.

Ijumaa, 12 Aprili 2019

PROF. MDOE AZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA KUANZISHWA VITUO VYA TEKNOLOJIA


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe leo amefungua Kikao Kazi cha kupitia na kutoa maoni yatakayowezesha kuboresha rasimu ya Mwongozo na Mpango wa Utekelezaji wa kuanzisha vituo vya Teknolojia nchini.

Akizungumza na washiriki wa kikao hicho mkoani Dodoma Prof. Mdoe ameainisha kuwa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, unalenga katika kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.
Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe akizungumza na washiriki (hawapo pichani) katika kikao Cha kujadili rasimu ya mwongozo wa kitaifa wa kuanzisha na kuendeleza vituo vya Teknolojia na ubunifu. Kikao hicho kimefanyikia mkoani Dodoma.
Amesema Mpango huo, umebainisha umuhimu wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika maendeleo ya nchi na Uendelezaji wa Teknolojia na Ubunifu kuwa unakabiliwa na changamoto ya kuwepo kwa vituo mahiri vya kuzilea, kuziendeleza au kuhawilisha teknolojia na bunifu ili kuzigeuza na kuwa fursa za kiuchumi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia Hotuba ya mgeni rasmi wakati wa kikao cha kujadili rasimu ya Mwongozo wa kitaifa wa kuanzisha na kuendeleza vituo vya Teknolojia na ubunifu.
Prof. Mdoe amesema vituo vya kuendeleza teknolojia na ubunifu ni nyezo muhimu katika maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na huchochea kuwepo kwa tija katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.

“Uwepo wa vituo hivyo hujenga mazingira wezeshi kwa Taasisi za utafiti na maendeleo kwa kutoa huduma za kulea, kuendeleza na kuhawilisha  teknolojia kwa makampuni madogo na ya kati (SMEs).  Aidha, vituo hivi vina umuhimu wa kutoa ufumbuzi wa kisayansi, na kiteknolojia katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii,” alisisitiza Prof. Mdoe.

Washiriki wa kikao cha kujadili rasimu ya mwongozo wa kitaifa wa kuanzisha na kuendeleza vituo vya Teknolojia na ubunifu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa umuhimu wa vituo hivyo ni kuimarisha matumizi chanya ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kama vile Teknolojia za kuendeleza viwanda.

Naibu Katibu Mkuu Prof.James Mdoe aliyekaa katikati akisoma hotuba yake wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili rasimu ya mwongozo wa kitaifa wa kuanzisha na kuendeleza vituo vya Teknolojia na Ubunifu kikao ambacho kinafanyika mkoani Dodoma.

Kikao kazi hicho cha siku moja kimehudhuriwa na washiriki kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi zinazojishughulisha na masuala ya utafiti, na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Washiriki wa kikao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza mgeni rasmi kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili Rasimu ya Mwongozo wa kuanzisha vituo vya teknolojia.