Ijumaa, 22 Mei 2020

WAZIRI NDALICHAKO ATANGAZA TAREHE ZA MITIHANI KWA KIDATO CHA SITA NA VYUO VYA UALIMU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amezitaka  shule zote zenye wanafunzi wa kidato cha sita kuanza maandalizi ya kupokea wanafunzi hao ili waanze masomo Juni 1 2020 kama ilivyoelekezwa.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati alipoongea na waandishi wa habari ambapo amesema ni vizuri kwa shule za bweni zikaanza kupokea wanafunzi hao Mei 30, 2020 ili waanze masomo katika muda uliopangwa.
 
Amesema wakati shule za bweni zikipokea wanafunzi Mei 30, 2020 shule za kutwa nazo zianze maandalizi huku akilitaka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kusambaza ratiba za mtihani mapema kwa ajili ya maandalizi.

"Mitihani ya Kidato cha sita na Vyuo vya Ualimu inaanza Juni 29, 2020 na kukamilika Julai 16, 2020 hivyo NECTA sambazeni ratiba za mtihani mapema ili shule  na vyuo vianze maandalizi na kumbukeni mtapaswa kutoa  matokeo ya mtihani huo kabla ya Agosti 30, 2020,"alisema Wziri Ndalichako.

Kwa upande wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Kati waziri   Ndalichako ameyataka mabaraza pamoja na Seneti ya Vyuo kupanga ratiba za masomo kwa lengo la kufidia muda wa masomo ambao wanafunzi wamepoteza wakiwa nyumbani na kuwasilisha ratiba hizo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) ili mwaka huu wa masomo ukamilike bila kuathiri ratiba za masomo kwa nwakali 2020/2021

Pia amevitaka vyuo hivyo kuwasilisha nyaraka muhimu zinazohitajika Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ili Mikopo kwa wanafunzi na ada zao ziweze kutolewa mapema kwa kuwa tayari Serikali imeshatoa jumla ya sh Bilioni 122.8  kwa ajili hiyo.

Itakumbukwa kwamba Mei 21 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia wananchi kupitia Vyombo vya habari alitangaza kufungua vyuo vya elimu ya Juu, Kati na Masomo kwa wanafunzi wa kidato cha sita.

WAZIRI NDALICHAKO ATANGAZA TAREHE ZA MITIHANI KWA KIDATO CHA SITA NA VYU...

Jumatano, 13 Mei 2020

TAARIFA KWA UMMA

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY


STUDY OPPORTUNITIES TENABLE AT THE HELWAN UNIVERSITY IN THE ARAB REPUBLIC OF EGYPT FOR 2020/2021 ACADEMIC YEAR

1.0  Call for Application

The general public is hereby informed that, Helwan University has granted scholarship opportunities to eligible Tanzanian nationals to pursue Undergraduate and Postgraduate studies for the academic year 2020/2021.

 

2.0  Application Requirements

Applicants should submit the following documents in PDF form;

1.      A recommendation letter;

2.      A statement of purpose describing reasons for selecting the relevant program;

3.      Certified photocopies of academic certificates, transcripts and birth certificate;

4.      A certificate of English Language Proficiency;

5.      A detailed Curriculum Vitae;

6.      A copy of the information page of the passport; and

7.  Applicants for Masters and Doctorate degrees should include their research proposal.

NB: Incomplete application forms and application documents will not be considered.

For details on application procedures, an application form and required application documents visit:

http://www.helwan.edu.eg/InternationalStudents/wp-content/uploads/2013/01/HU-IASSP-2020.pdf

 

3.0  Scholarship Coverage

This is a partial scholarship which covers only tuition fee. It does NOT cover accommodation expenses, monthly stipend, travel expenses, healthcare or any category of insurance, stationery or visa costs.  

 

4.0  Submission

A filled application form and the corresponding application documents should be submitted to the following email: hisb-scholarships@hq.helwan.edu.eg not later than 31th May, 2020.

 

Issued by

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

Government City,

Mtumba Area,

Afya Street,

P. O. Box 10,

40479 DODOMA.

Alhamisi, 23 Aprili 2020

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AWAPONGEZA WABUNGE KUJENGA SHULE YA WASICHANA


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Ave Maria Semakafu wakikagua ujenzi wa miundombinu ya shule ya sekondari maalum ya wasichana inayojengwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo Chamwino, Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amefanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule maalum ya wasichana inayojengwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kata ya Kikombo wilayani Chamwino Jijini Dodoma

Kiongozi huyo amesema lengo la ziara hiyo pamoja na mambo mengine ni kuona maeneo ambayo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaweza kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo katika muda uliopangwa.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akikagua ujenzi wa miundombinu mipya ya shule ya sekondari maalum ya wasichana wa kidato cha tano inayojengwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo Chamwino, Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Ave Maria Semakafu.
Naibu waziri Ole Nasha amewapongeza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa kujenga shule ya wasichana kwani kumuelimisha mtoto wa kike ni sawa na kuelimisha jamii nzima.

Shule ya Wasichana ya Bunge ilianza kujengwa Januari 2020 itakamilika Juni mwaka huu na inatarajiwa  kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano. 

Katika ziara hiyo Naibu waziri Ole Nasha aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ave Maria Semakafu.Muonekano wa baadhi ya majengo ya shule ya sekondari maalum ya wasichana inayojengwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo Chamwino, Dodoma.