Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kwa kushirikiana na Asasi za vyuo na
taasisi za Canada wataanzisha Mpango wa kutekeleza mradi wa
Mafunzo ya kukuza stadi kwa ajili ya uajiri (Improving Skills Training for Employment Programme - ISTEP ). Mpango huu utajenga uwezo wa asasi
za Mafunzo ya ufundi nchini kufundisha kwa umahiri stadi zinazoitajika katika
sekta za uchimbaji wa madini, mafuta, gesi na sekta ya utalii.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Stadi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalirwe
alieleza hayo jijini Dar es Salaam katika warsha ya makubaliano na wadau
iliyokuwa ikijijadili hatua mbalimbali
katika kujenga ushirikiano wa
jinsi wanafunzi na tasnia
zitakavyofaidika na mpango huu.
Alisema Mradi
huu utajikita katika sekta
za madini, gesi na utalii,
kwamba utajenga uwezo wa asasi za kitanzania
za Mafunzo ya ufundi kufundisha kwa umahiri stadi zinazohitajika katika sekta
zote za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi na sekta ya utalii, na hivyo
kuwapatia vijana takribian 1,200 stadi mwafaka zitakazowawezesha kujiajiriwa kwenye sekta ya uchimbaji na
utalii ama kujiajiri.
“Tayari
wataalanu wamefanya upembuzi katka
maeneo mbalimbali , ili
kupata mahitaji ya utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano, ambao utagharamia Dola za Canada million 13 na
utawanufainisha watanzania 12,000 hasa
katika masuala ya gesi .” alisema Katabalirwe.
Aidha, alisema
taasisi 11 zitashirikiana katika kukuza uelewa kwa vijana
kwa kuwa gesi ni kitu kipya
kinachohitaji nguvu kazi ya kutosha na yenye Mafunzo maalum. Vijana
hao watatoka katika taasisi za utalii, Madini na Gesi ambao watapatiwa Mafunzo
ya uchimbaji wa madini na uchomeleaji wa mabomba ya gesi.
Mwenyekiti kutoka shirikisho la wachimbaji na watafutaji wa Madini Tanzania , Nyanda Shuli
alisema mpango huo ni muhimu
katika kuendeleza Sekta
ya Madini na Nishati
kwa kuwa inahitaji nguvu
kazi ya kutosha kukuza
sekta hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.