Alhamisi, 24 Machi 2016

Serikali yatoa zawadi kwa Halmashauri zilizotekeleza mipango ya kuboresha Elimu


Serikali kwa kushirikiana na wafadhili wa maendeleo wanatekeleza programu inayojulikana kama Lipa Kulingana na Matokeo ambayo inalenga kutoa zawadi kwa Serikali kuu na Halmashauri kulingana na utekelezaji ambapo kwa kuanzia vigezo vifuatavyo vimewekwa kwa ajili ya kupima utendaji wa Halmashauri. Vigezo vilivyowekwa viliangalia Eneo la Ruzuku zinazopelekwa shuleni.  Katika eneo hili Halmashauri 167 zilipimwa kwa kanuni ya kuchukua fedha iliyopelekwa shuleni.

Eneo lingine lililoangaliwa ni upatikanaji wa  Takwimu. Eneo hili liliangalia idadi ya shule zilizopo kwenye Halmashauri ambazo takwimu zake zimekusanywa na kuwekwa mtandaoni.  

Aidha, eneo lingine lililoangaliwa ni Uwiano wa Mwalimu kwa Mwanafunzi: Halmashauri zilipimwa kwa idadi ya shule ambazo zilikuwa na walimu wachache na zimeongezewa walimu. Hii ni kwa sababu Halmashauri zinapimwa uwezo wake wa kupunguza walimu kwenye shule zenye walimu wengi kupeleka kwenye shule zenye walimu wachache na pia kupanga walimu wapya kwenye shule zenye uhaba wa walimu.

 Jumla ya Kila Halmashauri ilitakiwa ipate dola za kimarekani 7,000. Katika hili Serikali kuu pia inapimwa katika uwezo wake wa kupeleka walimu kwenye Halmashauri na kwa tawkimu zilizokusanywa mwaka 2014 wakati wa kusambaza walimu. Halmashauri 112 zilikuwa na uwiano wa kati ya 1:35 -1:50, Halmashauri 25 zilikuwa na uwiano zaidi ya 1:50 na Halmashauri 27 zilikuwa na uwiano wa chini ya 1:35.


Halmashauri ya zilizofanya vizuri na kupata zawadi ni Mbinga iliyopata shilingi 331,234,275.00, Chato 302,637,899.56, Busega 282,677,815.00, Lushoto 267,403,689.33 Nkasi 262,991,890.00, Liwale 260,836,890.00,  Sikonge 244,679,555.61,  Mbarali 216,749,648.88, Mpanda 213,341,853.60 na Tabora 185,191,379.60








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.