JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU,
SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia (WEST), kwa mujibu wa Waraka Namba 4 wa mwaka 2014, imeipa Taasisi ya Elimu Tanzania mamlaka
ya kufanya uthibiti wa ubora wa vitabu
na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Itakumbukwa kuwa kabla
ya mwaka 2014, ithibati kwa vitabu na vifaa vya kielimu
ilikuwa inatolewa na Kamati ya Ithibati ya Vitabu na Vifaa vya Kielimu (EMAC),
ambayo ilivunjwa mwaka 2013.
Kwa muktadha huo, Wizara
inawaagiza wachapishaji wote wa vitabu vya Darasa la Nne hadi Darasa la Saba ambavyo
vina ithibati ya EMAC kuviwasilisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili
ya kufanyiwa tathmini. Ili kufanikisha zoezi hili nakala nne (4) za kila chapisho
ziwasilishwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya tarehe
30 septemba, 2016. Baada ya muda huo kupita, vitabu vyote ambavyo havitakuwa
vimewasilishwa na kuhakikiwa na Taasisi hiyo vitafutwa katika orodha ya vitabu
vyenye ithibati.
Baada ya zoezi la
uhakiki kukamilika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na
OR – TAMISEMI, itafanya ufuatiliaji kwenye shule na maduka ya vitabu ili
kuhakiki utekelezaji wa agizo hili.
Aidha, hatua stahiki
zitachukuliwa kwa wauzaji/wachapishaji watakaoendelea kuuza vitabu
vitakavyokuwa vimefutwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.