Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali ya Canada na Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa
ajili ya Ajira unaendesha warsha ya siku
tatu inayojadili Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kushirikisha mfumo shirikishi, mafunzo ya
kuendeleza ujuzi, na Masuala ya Jinsia.
Warsha hii
inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii (Bustani) inalenga kusaidia
uanzishwaji wa mfumo wa kuongeza
ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Elimu ya Ufundi na
Mafunzo ya Ufundi Stadi sekta nchini.
Wadau mbalimbali
wameshirikishwa katik warsha hii ambayo imewaleta pamoja wadau wa elimu ya ufundi
na wawakilishi mbalimbali wakubwa, mashirika mbalimbali yanayotoa elimu na
mafunzo, watu binafsi, waajiri na vyama vya waajiri, soko la ajira mashirika ya
habari na mashirika ya kiraia ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwezesha
wanafunzi wanaohitimu katika Elimu
ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi anakuwa na ujuzi wa kujiajiri na
kuajiriwa.
: Mshauri Mwandamizi wa Ufundi na mwakilishi
wa Vyuo na Taasisi zinazosaidia vyuo na
Vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi Canada Dr. Alan Copeland (aliyesimama) ambaye kwa sasa anasimamia
Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira nchini akizungumza katika warsha ya siku tatu
ya wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayofanyika jijini Dar
es Salaam inayojadia masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo.
Baadhi
ya Washiriki wa Warsha ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya
Ufundi na Mafunzo Ufundi Stadi. Warsha hii imewaleta pamoja wadau wa Elimu ya
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi
inavyoweza kufanya vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa wakiwa na ujuzi
stahiki.