Jumanne, 6 Desemba 2016

Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakutana Dar


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali ya Canada  na Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  unaendesha warsha ya siku tatu inayojadili Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi  kwa kushirikisha mfumo shirikishi, mafunzo ya kuendeleza ujuzi, na Masuala ya Jinsia. 

Warsha hii inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii (Bustani) inalenga kusaidia uanzishwaji wa mfumo wa kuongeza  ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi sekta nchini.

Wadau mbalimbali wameshirikishwa katik warsha hii ambayo imewaleta pamoja wadau wa elimu ya ufundi na wawakilishi mbalimbali wakubwa, mashirika mbalimbali yanayotoa elimu na mafunzo, watu binafsi, waajiri na vyama vya waajiri, soko la ajira mashirika ya habari na mashirika ya kiraia ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwezesha wanafunzi wanaohitimu katika  Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi anakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.

:   Mshauri Mwandamizi wa Ufundi na mwakilishi wa Vyuo na Taasisi  zinazosaidia vyuo na Vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi Canada Dr. Alan Copeland  (aliyesimama) ambaye kwa sasa anasimamia Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  nchini akizungumza katika warsha ya siku tatu ya wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayofanyika jijini Dar es Salaam inayojadia masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo.





Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya Ufundi na Mafunzo Ufundi Stadi. Warsha hii imewaleta pamoja wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi inavyoweza kufanya vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa wakiwa na ujuzi stahiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni