Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kassim Majaliwa amekitaka Chuo kikuu Hiria
nchini kuhakikisha kinaongeza ubora wa utoaji Elimu na kupanua wigo wa udahili
kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Waziri Mkuu
Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 33 ya Chuo hicho ambayo
yamefanyikia mkoani Singida na kusisitiza kuwa Umuhimu wa Chuo kikuu huria uko
bayana katika kuhakikisha malengo ya serikali ya kutekeleza sera ya uchumi wa
viwanda inafikiwa kupitia wataalamu wanaomaliza chuoni hapo.
Waziri
Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya Tano inatambua na inaunga mkono juhudi
zinazofanywa na uongozi wa chuo hicho huku wakisisitizwa kuzingatia vigezo,
taratibu za utoaji wa Elimu iliyo bora ili wapatikane wataalamu ambao ni bora
kwa maslahi ya Taifa.
Kwa upande
wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema
Serikali inatambua mchango wa Chuo hicho katika kipindi cha miaka 25 ambapo
kimekuwa kikitoa Elimu katika masafa ya mbali hali ambayo inahitaji
mwanafunzi kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kifikia malengo.
Kutokana na juhudi hizo
Waziri Ndalichako ameahidi Serikali itaendelea Kuimarisha miundombinu ya Tehama
ili Elimu hiyo ya masafa iweze kuwafikia watu wengi zaidi.
Waziri
Ndalichako amewataka wahitimu kutumia vyema ujuzi na kuhakikisha wanaimarisha
utendaji kazi katika serikali na hata Sekta binafsi.
Pia amewataka wahitimu kujenga nadhani pamoja na kuwa na ari katika uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi katika Shughuli ambazo watakuwa wanazifanya.
Pia amewataka wahitimu kujenga nadhani pamoja na kuwa na ari katika uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi katika Shughuli ambazo watakuwa wanazifanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.