Waziri wa Elimu, Sayasni na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekihakikishia Chama cha walimu Viziwi
kuwa Serikali iko tayari kusikiliza na kujua changamoto zinazowakabili wanafunzi
wenye uziwi ili hatua madhubuti ziweze kuchukuliwa.
Waziri Ndalichako amesema
hayo leo mkoani Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na walimu wenye Uziwi
ambapo amewaeleza kuwa hajafurahishwa na matokeo ya kidato cha Nne ya shule ya
Sekondari Njombe na kubainisha kuwa ni vyema changamoto zikaainishwa ili hatua
ziweze kuchukuliwa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkurugenzi wa Chama cha
Walimu wenye uziwi Tanzania Karim Bakari.
Kwa upande wake mratibu wa
chama hicho cha Walimu Viziwi Francis Mbisso ameiomba Serikali kutoa semina kwa
walimu wanaofundisha wanafunzi Viziwi ili walimu waweze kuelewa saikolojia ya wanafunzi pale
wanapowafundisha, lakini pia kuwe na wigo
mpana wa mafunzo ya ufundi kwa wanafunzi
hao badala ya kuwalazimisha kusoma
masomo ya darasani.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akutana na kufanya
mazungumzo na Chama cha Walimu wenye Uziwi Tanzania. Mazungumzo hayo yanalenga
kutataua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye uziwi.
Mbisso ameshauri kuwepo kwa
mtaala wa lugha ya alama pekee utakaowasiadi wanafunzi wenye uziwi kuelewa kwa
uarahisi masomo yao wanapokuwa darasani ikiwa ni pamoja na kuongeza muda ya
kipindi darasani ukilinganisha na muda wanaotumia wanafunzi wa kawaida.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu
akisalimiana na Mwalimu Theresia Nkwera mwenye uziwi, ambaye alishiriki
majadiliano ya pamoja yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili
wanafunzi wenye uziwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.