Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amezitaka Taasisi za Elimu ya Juu kuzingatia
suala la ubora wa mafunzo wanayoyatoa katika programu zao ili kupata wahitimu
wenye ujuzi unaotakiwa kwenye uchumi wa viwanda.
Naibu
Waziri Ole Nasha amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Maonesho ya 13 ya Elimu ya Juu ambapo
amesema Serikali ina mategemeo makubwa ya kupata rasilimali watu bora itakayofanya
kazi katika viwanda hivyo suala la ubora wa mafunzo linahitaji kupewa
kipaumbele.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akizungumza na wanashiriki (Hawapo
pichani) katika maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu wakati wa kufunga wa
maonesho hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es alaam.
“Tunataka
mzalishe wahitimu wanaoonekana wamepata Elimu bora na si bora Elimu ambao
wataweza kufanya kazi kulingana na mahitaji na matarajio ya taifa letu lakini
pia watakaokidhi vigezo na matarajio ya wadau mbalimbali,” Alisisitiza Naibu Waziri
Ole Nasha.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akisikiliza ufafanuzi kuhusu masuala
mbalimbali ya elimu kutoka kwa mmoja wa
washiriki wa maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu yanayofanyika jijini Dar
es Salaam.
Alisema
wizara yake itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu zaidi suala la ubora
wa Elimu katika ngazi zote na kuzitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha inafuatiali vyuo kwa karibu ili
kuhakikisha wanafuata miongozo iliyopo na kwamba Serikali haitavumilia taasisi
au mtu yeyote anayejaribu kukiuka miongozo hiyo kwa sababu yoyote ile.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akikabidhi cheti cha ushiriki kwa mmoja
wa wadau wa Elimu ya Juu walioshiriki maonesho ya kumi na tatu ya Elimu ya Juu
yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Maonesho
ya Elimu ya Juu yamehitimishwa leo na yalikuwa na kauli mbiu ELIMU YA JUU BORA
KWA MAPINDUZI YA VIWANDA
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akijadiliana masula mbalimbali kuhusu Elimu
na baadhi ya washiriki wa maonesho ya Elimu Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.