Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka
wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Msingi Feza kuepuka vitendo viovu
ambavyo vinaweza kukatisha ndoto zao katika maisha.
Ole Nasha ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 15 ya
darasa la saba ya shule hiyo na kuwataka vijana hao kutambua kuwa kuhitimu katika
hatua hiyo ndio mwanzo wa safari ndefu waliyonayo katika Elimu na kuwa nidhamu pekee
ndio msingi wa mafanikio.
“Jamii yetu kwa sasa inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili vitendo viovu
kama vile vijana kujishirikisha katika masuala ya ngono, ulevi, matumizi mabaya
ya mitandao ya kijamii jihadharini navyo sana katika maisha yenu, mkijiingiza
tu mtaharibu ndoto zenu mlizojiwekea na matokeo yake mtashindwa kushiriki
katika jitihada za kuijenga nchi yenu,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akihutubia wakati wa
mahafali ya kumaliza Elimu ya Msingi Feza yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale
watakayokuwa wakifanya ili kuweza kufikia malengo yao.
Alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Sekta binasfi
katika maendeleo ya Elimu nchini kwa kuwaandaa vijana kimaadili na kitaaluma
ili kufikia dira ya Sera
ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inayolenga kuwa na mtanzania aliyeelimika na
mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitizamo chanya ili kuweza kuchangia
katika kuleta maendeleo ya Taifa.
“Mtaona Serikali sasa imefuta
tozo na kodi ambazo zilikuwa ni kero kwa wamiliki wa Shule binafsi kama vile
Tozo ya Uendelezaji Ujuzi (Skills Development Levy-SDL), Tozo ya Zimamoto, Kodi
ya Mabango na Tozo ya Usalama Mahali pa Kazi (Occupational Safety and Health
Administration-OSHA) hii yote ni kuthamini mchango mkubwa ambao mmekuwa mkiutoa
katika kuelimisha vijana wa Taifa hili,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.
Wahitimu
wa darasa la saba katika shule ya msingi Feza wakifuatilia hotuba ya Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa mahafali yao
yaliyofanyika oktoba 13, 2018 jijini Dar es salaam.
Hata hivyo amewataka wamiliki
wote wa shule nchini kutambua kuwa pamoja na shule kuwa zao wanatakiwa kufuata
taratibu, sheria na kanuni katika uendeshaji wa shule hizo kwa ni bado elimu
itolewayo ni mali ya umma na watoto ni wa kitanzania.
Naye Mkurugenzi wa Shule za Feza Ibrahimu Yunus anasema kwa sasa shule
hiyo ya Msingi ina jumla ya wanafunzi 770 ambapo wanaohitimu darasa la saba
mwaka huu ni jumla ya wanafunzi 75 huku shule hiyo ikijivunia kufanya vizuri
kwenye masuala ya Elimu katika ngazi zote zinazotolewa shuleni hapo.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akigawa cheti kwa
mmoja wa wanafunzi aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika shule ya Msingi
Feza wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.