Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa ofisi mpya za Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazojengwa kwenye Mji wa serikali Ihumwa,
mkoani Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Waziri Ndalichako amesema kukamilika kwa ofisi hizo utasaidia utendaji kazi kuimarika kwa kuwa mazingira ya kufanyia kazi yanakuwa
ni mazuri zaidi.
“Ofisi kwa ujumla ni nzuri zimejengwa vizuri naamini hata
watumishi watakuwa na ari ya kufanya kazi kwa kuwa mazingira yatakuwa bora
zaidi.” alisema Waziri Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa
ofisi za wizara kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi, Kamishna Msaidizi Aron Lunyungu
kutoka Shirika la Magereza.
Waziri Ndalichako pia
amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kuhakikisha
anasimamia kwa ukaribu ujenzi wa jengo pacha la wizara ili liweze kukamilika
kwa wakati.
Naye Msimamizi wa ujenzi huo Kamishna Msaidizi Aron Lunyungu kutoka Shirika la Magereza amesema ujenzi umefikia katika hatua ya ukamilishaji na kwamba wanatarajia kukabidhi Jengo la Wizara baada ya wiki mbili kuanzi leo.
Ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia katika mji mpya wa serikali ulianza Desemba 10, 2018.

Muonekano wa hatua ya
ujenzi wa ofisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinazojengwa katika
mji wa Serikali uliopo eneo la Ihumwa jijini Dodoma.