Alhamisi, 10 Desemba 2020

KARIBUNI WAHESHIMIWA MAWAZIRI WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Profesa Joyce Lazaro Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma  Desemba 09, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma Desemba 09, 2020.

1        Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary wakisalimiana na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.

1    Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


1        Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


        Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary akisalimiana na Mkurugenzi Uthibiti Ubora wa Shule Euphrasia Buchuma mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara, zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


      Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu Huruma Mageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara, zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni