Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako leo anawasilisha taarifa yenye
msimamo wa Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika mkutano
mkuu wa 39 wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, Utamaduni, habari
na Mawasiliano -UNESCO.
Waziri Ndalichako pia tayari ameshiriki
mikutano mbalimbali inayohusu tume za UNESCO zilizoanza oktoba 30, 2017 ambapo
amepokea taarifa mbalimbali zinazohusu fursa mbalimbali za namna ya kupata
misaada ya maendeleo kutoka UNESCO na washirika wake wa kimataifa, pia viongozi
wa Tume za Taifa za UNESCO duniani kubadilishana uzoefu na kupeana
mbinu mbalimbali za kuandika kazi miradi kwa maslahi ya nchi zao.
Katika mkutano huo waziri wa Elimu Profesa Ndalichako ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Balozi Samwel Shelukindo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Petro Lyatuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Dkt. Moshi Kimizi.
Mkutano huo Mkuu hufanyika kila baada ya miaka miwili na unahusisha nchi zote wanachama za UNESCO.