Naibu
Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa
William Ole Nasha ameitaka Wizara yake kufanya uchunguzi na kutoa ripoti ya namna
ukarabati wa Miundombinu ulivyofanyika katika Chuo cha Ualimu Butimba ili
kujiridhisha kama kweli ukarabati huo unaakisi kiasi cha fedha zilizotolewa.
Naibu
Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo Mjini Mwanza baada ya kufanya ziara katika
chuo hicho hapo ambapo amesema
hajaridhishwa na ukarabati ulivyofanyika kwa kuwa Chuo hicho kilipatiwa kiasi
cha takribani Milioni Mia Nane Sitini na
Tatu.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akikagua moja ya
Bweni la Wanafunzi katika Chuo cha Ualimu Butimba lililofanyiwa ukarabati na
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa Kulingana na
Matokeo (EP4R).
Ole
Nasha amesema lengo la Serikali ni
kuhakikisha Vyuo vya Ualimu vinakuwa na mazingira mazuri ya kuwaandaa Walimu wanaokwenda
kufundisha katika shule mbalimbali hapa
nchini hivyo ni jukumu la Wakuu wa
Taasisi na Vyuo vya Elimu kuhakikisha wanasimaia Miradi mbalimbali ya Elimu kwa
ukamilifu na kuwa Serikali haitasita
kuchua hatua kwa yeyote atakayeshindwa kusimamia Miradi hiyo kwa weledi.
“Chuo
hiki kimepatiwa takribani Milioni Mia Nane Sitini na Tatu kwa ajili ya
ukarabati wa miundombinu kama hivi ndivyo ukarabati uliofanyika hauonyeshi
thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya Chuo hiki cha Ualimu Butimba, kwa
kweli Sijaridhishwa”alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Akitoa
maelezo Mkuu wa Chuo hicho John Ole Meiludie amejitetea kuwa kazi hiyo ya
ukarabati imefanyika kwa umakini isipokuwa wanafunzi wenyewe ndiyo wanachana nyavu za madirisha lakini pia
hali ya mvua zinaponyesha huondoa rangi
ambayo inakuwa imepakwa katika majengo
ya Chuo hicho.
1.
Naibu Waziri wa Elimu akipokea maelezo
katika maabara ya baiolojia Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole akipokea maelezo kutoka
kwa Mkufunzi Ramadhani Wenge kuhusiana na maabara ya Bailojia iliyopo katika
Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza.
Akiwa
Mkoani Mwanza Naibu Waziri Ole Nasha ametembelea Shule ya Sekondari Nyegezi
iliyoko Wilaya ya Nyamagana na Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma VETA kilichopo
wilaya ya Ilemela na kuridhishwa na namna walivyotekeleza miradi ya Elimu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mhe. William Ole Nasha akiongea na Wanafunzi wa Shule ya sekondari Nyegezi
Iliyopo Mkoani Mwanza alipofanya ziara shuleni hapo kukagua miradi
inayotekelezwa na Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).