·
AWATAKA
WATANZANIA KUISHI KWA KUPENDANA
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia amewataka watanzania kujenga tabia ya kupendana, kuvumilia na
kuhurumiana katika maisha ya kila siku.
Waziri Ndalichako ameyasema
hayo leo mkoani Iringa mara baada ya kuongoza mamia ya wananchi wakati wa ibada ya
kuaga miili ya mapacha walioungana Maria na Cosolata katika viwanja vya Chuo
Kikuu Cha RUAHA mkoani Iringa.
Amesema Maria na Consolata
katika uhai wao waliishi wakiwa wameungana kwa hiyo waliishi kwa kuvumiliana na
kupendana pia.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiaga miili ya mapacha
walioungana Maria na Consolata katika viwanja vya Chuo Kikuu cha RUAHA Mkoani
Iringa.
Amesema, Watanzania
wanatakiwa kujiuliza kwa nini Maria na Consolata wamezaliwa Tanzania na Siyo
nchi nyingine? amesisitiza kuwa watoto hao wamezaliwa nchini hapa ili iwe funzo
kwa watanzania.
Maria na Consolata watazikwa
kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.
Maria na Consolata Mwakikuti
walifariki jumamosi saa mbili usiku Juni 2 mwaka huu na miili yao itapumzishwa
kwenye nyumba yao ya milele kwenye makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki
Tosamaganga mkoani Iringa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akilia kwa huzuni mara
baada ya kuaga miili ya mapacha walioungana Maria na Consolata katika Viwanja
vya Chuo Kikuu cha RUAHA Nkoani Iringa.
Kwa upande wake sista
Calista Ludega ambaye ni Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Theresa wa Mtoto wa Yesu
Jimbo Katoliki la Iringa amesema kuwa wamewazika Maria na Consolata mahala
wanapolala Masista wa Maria Consolata kwa ajili ya kuwaenzi masista wa
Wamishionari wa Consolata kwa kuwa wao wamekuwa sehemu kubwa ya malezi tangu
waliopozaliwa watoto hao hadi wanapomaliza maisha yao duniani.
Familia ya Baba na mama wa
mapacha hao kutoka Mkoani Mbeya na Kagera, masista wa Consolata wa Iringa na
waombolezaji wengine wameungana katika kuwasindikiza katika safari yao ya
mwisho duniani.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiweka saini kitabu cha
maombolezo ya Msiba wa mapacha walioungana Maria na Consolata.