Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeiagiza serikali kuhakikisha
inafanikisha upatikanaji wa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha
ukarabati na upanuzi wa jengo la Utawala la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar
es Salaam (DUCE).
Agizo
hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba Jijini Dar es
Salaam baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi huo wa ukarabati na upanuzi wa jengo
hilo ambapo amesema kuchelewa kumalizika kwa wakati kunaweza kusababisha kuongezeka
kwa gharama za ujenzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupanda kwa gharama
za vifaa.
Mhe.
Serukamba amesema kiasi hicho cha fedha ni muhimu kikapatikana kwa sasa ambapo kazi
ya ujenzi na ukarabati ikiwa inaendelea kwani itasaidia pia kuondoa usumbufu kama
jengo hilo litakamilishwa nusu na kuanza kutumika.
“Kucheleweshwa
kwa fedha zilizobaki zitafanya jengo hili kujengwa kwa gharama kubwa sana kwani
vifaa vya ujenzi vinapanda, lakini pia haitakuwa vizuri kumalizia upande mmoja wa
jengo watu waingie wafanye kazi baadaye wapishe ujenzi inakuwa ni usumbufu kwa watumishi”
amesema Mhe. Serukamba.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakielekea katika jengo la Utawala linalokarabatiwa.
|
Aidha,
Mhe. Serukamba amekitaka Chuo hicho kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha maktaba
ya Chuo hicho inakuwa kamilifu na kupewa kipaumbele ili kuwa na maktaba inayojitosheleza
kwa kuwa na eneo lenye ubora, vitabu vya kutosha ikiwemo vitabu vya elektroniki.
Vilevile ameutaka Uongozi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kuweka utaratibu wa wanafunzi wa DUCE kuweza kutumia maktaba ya kisasa
iliyopo katika kampasi yake kuu
Pamoja
na hayo Kamati pia imeitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kusimamia madai
ya watumishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ujumla na kuhakikisha madai
stahiki yanalipwa.
Awali
Rasi wa Duce, Prof. Bernadeta Killian ameieleza Kamati hiyo kuwa Mradi huo wa upanuzi
na ukarabati jengo la Utawala unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.2 kwa ujumla,
kiasi ambacho kinajumuisha gharama za ujenzi, ukarabati, kuweka mifumo ya
TEHAMA pamoja na samani za ndani za jengo hilo ambapo mpaka sasa bado kiasi cha
Shilingi Bilioni 1.1 kinahitajika ili kukamilisha.