Serikali
kwa kushirikiana na wafadhili wa maendeleo wanatekeleza programu inayojulikana
kama Lipa Kulingana na Matokeo ambayo inalenga kutoa zawadi kwa Serikali kuu na
Halmashauri kulingana na utekelezaji ambapo kwa kuanzia vigezo vifuatavyo
vimewekwa kwa ajili ya kupima utendaji wa Halmashauri. Vigezo vilivyowekwa viliangalia
Eneo la Ruzuku zinazopelekwa shuleni.
Katika eneo hili Halmashauri 167
zilipimwa kwa kanuni ya kuchukua fedha iliyopelekwa shuleni.
Eneo
lingine lililoangaliwa ni upatikanaji wa Takwimu. Eneo hili liliangalia idadi ya
shule zilizopo kwenye Halmashauri ambazo takwimu zake zimekusanywa na kuwekwa
mtandaoni.
Aidha,
eneo lingine lililoangaliwa ni Uwiano
wa Mwalimu kwa Mwanafunzi: Halmashauri zilipimwa kwa idadi ya shule ambazo
zilikuwa na walimu wachache na zimeongezewa walimu. Hii ni kwa sababu
Halmashauri zinapimwa uwezo wake wa kupunguza walimu kwenye shule zenye walimu
wengi kupeleka kwenye shule zenye walimu wachache na pia kupanga walimu wapya
kwenye shule zenye uhaba wa walimu.
Jumla ya Kila Halmashauri ilitakiwa ipate dola
za kimarekani 7,000. Katika hili Serikali kuu pia inapimwa katika uwezo wake wa
kupeleka walimu kwenye Halmashauri na kwa tawkimu zilizokusanywa mwaka 2014
wakati wa kusambaza walimu. Halmashauri 112 zilikuwa na uwiano wa kati ya 1:35
-1:50, Halmashauri 25 zilikuwa na uwiano zaidi ya 1:50 na Halmashauri 27 zilikuwa
na uwiano wa chini ya 1:35.
Halmashauri
ya zilizofanya vizuri na kupata zawadi ni Mbinga iliyopata shilingi 331,234,275.00,
Chato 302,637,899.56, Busega 282,677,815.00, Lushoto 267,403,689.33 Nkasi 262,991,890.00,
Liwale 260,836,890.00, Sikonge 244,679,555.61,
Mbarali 216,749,648.88, Mpanda 213,341,853.60
na Tabora 185,191,379.60