JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Anuani ya simu “ELIMU”
Simu: 026 296 35 33
Baruapepe: info@moe.go.tz
|
|
Chuo cha Masomo
ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Jengo Na. 10,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA
Tarehe: 4
Mei, 2018
|
TAARIFA
KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji
ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambazo zinaonesha dosari na
makosa katika vitabu. Mojawapo ni picha inayoelezea viungo vya mwili wa
mwanadamu na nyingine iko katika Kitabu cha Kiingereza chenye maneno yanayosomeka
“The Big City of Tanzania”.
Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia inapenda kuutarifu umma kuwa kitabu kinachosambazwa kinachoelezea
viungo vya mwili wa mwanadamu si chapisho la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na
wala si miongoni mwa vitabu ambavyo vimesambazwa kwenye shule. Kitabu hicho
hakina uhusiano wowote na wala hakifanani na vitabu ambavyo vimechapishwa hivi
karibuni na TET.
Aidha, kuhusu kitabu cha
Kiingereza, hilo ni chapisho la mwaka 2016 ambalo limefanyiwa marekebisho
katika chapisho la mwaka 2018.
Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia inawasihi watanzania kupuuza taarifa hizo ambazo siyo za kweli na
zina nia ya kupotosha na kuleta usumbufu kwa jamii. Wizara pia inatumia fursa
hii kuwakumbusha wananchi kuzingatia Sheria za Matumizi ya Mitandao na kutambua
kuwa kutoa taarifa za uongo ni kosa la jinai.
Imetolewa
na:
Mwasu Sware
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA
YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
04/05/2018