Ijumaa, 22 Machi 2019


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
  SCHOLARSHIP TENABLE AT KOREA ADVANCE INSTITUTE OF SCIENCE
AND TECHNOLOGY (KAIST) 2019-2020

Call for Application
The General Public is hereby informed that, the Global IT Technology Program (ITTP) at KAIST, sponsored by Ministry of Science and ICT of Korea and The African Development Bank, offers Masters and PhD Programmes for government officials, academicians, researchers or experts in Public Institutions in IT fields. Selected applicants will receive scholarships up to 2 years for Master`s, and up to 3 years for PhD studies.

Mode of Application
All interested candidates should apply through an online application found in the following link: https://apply.kaist.ac.kr/intergradapply. Furthermore, the application system will be active from 10:00 am, March 19th, 2019 to 5:00 pm, April 9th, 2019.

Candidates are strongly encouraged to read carefully instructions given in the following link: https://admission.kaist.ac.kr/international/wp-content/uploads/2019/03/KAIST_FallRegular2019_Guideline_Graduate-Admission-updated-20190315.pdf

KAIST scholarship recipients are generally exempted from paying tuition fees. A monthly allowance of KRW 350,000 for Master’s course students and KRW 400,000 for Doctoral degree course students and the National Health Insurance fees are supported by the recipient’s advisor/department.

Document submission
All filled and printed documents should be submitted via registered mail to reach the undersigned before April 16th, 2019 to the address below:
Graduate Admissions Team, KAIST
#110, 1st Floor, E16-1 B/D
291 Daehak-ro, Yuseong-gu, Daejeon 34141
Republic of Korea
T. +82-42*350-2352
Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P .O. Box 10,
40479 Dodoma.

Jumatano, 20 Machi 2019


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY

Re: NEW ZEALAND COMMONWEALTH SCHOLARSHIPS 2019


1.0 Introduction

The Ministry of Education, Science and Technology as a Nominating Agent in the Country for the New Zealand Commonwealth Scholarships is Inviting applications from qualified Tanzanians for the post graduate studies tenable in New Zealand for the academic year 2019.

2.0 Qualifications

(i)             Applicants must be citizens of Tanzania;
      (ii)          Applicants should apply to an institution in New Zealand;
      (iii)         Applicants should not be serving in a military;
      (iv)         Applicant should NOT be older than 39 years during application;
      (v)            English Language Requirement: Applicant will be required to   
                provide evidence of proficiency in English.


3.0 Area of specialization:
All applicants should align their specializations to the following sector:-  

Ø Good Governance

*   Governance services: Public policy, Public management, Policy and Governance.

Ø Climate change and Resilience;

Ø Food Security and Agriculture

*   Agribusiness;
*   Farm Management;

*   Agricultural technology;

*   Dairy systems;

*   Agriculture and/or Horticulture management;

*   Rural development;

*   Supply chain management.

Ø Renewable Energy

*    Geothermal, solar, Hydro-electric and wind Energy;

*    Energy Engineering;

*    Renewable Energy Distribution systems.

* Market reform and sector management including Energy   Economics.

*   Energy efficiency.

Note
                  *   All Applicants should fill application form in English, writing
                    clearly using black or blue pen.

* Information on the Scholarship including eligible countries, application process, deadline, priority sectors and the list of participating New Zealand academic institution is available on the Scholarships web pages of the New Zealand Ministry of Foreign Affairs and Trade at the following website. www.nzscholarships.govt.nz

4.0 Mode of Application

The application form is attached herewith. NEW ZEALAND COMMONWEALTH SCHOLARSHIP 2019 FORM

Employed applicants MUST attach a letter from their employers confirming that, if granted scholarship will be allowed to utilize this opportunity.

In order to be nominated, all applicants must submit two sets of the following:-

1.     Completely filled application form;

2.     Certified copy of birth certificate;

3.     Certified copies of academic certificates and transcripts;

4.     Certified copy of Passport page of bio data;

5.     Two reference letters.

Deadline for submission of the application is 28th March, 2019.

Kindly submit your application to the address below:-

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

College of Business and Law,

Block 10,

Room No. J404,

P.O. Box 10,

DODOMA.

Jumatatu, 18 Machi 2019

KAMATI YA BUNGE YAHITIMISHA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI ILIYO CHINI YA WIZARA YA ELIMU


Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekamilisha ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi mitatu mikubwa inayogharimiwa na Serikali kupitia bajeti ya Mwaka 2018/19 katika baadhi ya Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo.

Kamati hiyo imetembelea Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) katika mradi wa upanuzi na ukarabati wa jengo la Utawala ambalo linagharimu shilingi  Bilioni 3.2 ambapo kazi hiyo inaendelea na litakapo kamilika litaongeza nafasi kwa ajili ya ofisi za watumishi na vyumba vya mikutano.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo hicho.

Aidha kamati imetembelea mradi wa upanuzi wa vyumba vya mihadhara
katika Chuo Kikuu Ardhi kazi ambayo imekamilika kwa hatua ya kwanza na
itagharimu shilingi  Bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake.

Kamati imekamilisha ziara yake katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo Wajumbe watembelea Jengo la jipya la Mihadhara linalojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo hicho, ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 300 kwa wakati mmoja.  Aidha kamati imepongeza wizara na uongozi wa Chuo kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanyika katika kusimamia ujenzi huo. Jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akijadiliana jambo katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo hicho.


 Aidha  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako amepongeza uongozi wa Chuo kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za zinazotokana na Mapato ya ndani na kutumika kwa kutekeleza miradi yenye tija  kwa Chuo. Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia suala la kubana matumizi na kuelekeza fedha katika kazi zenye faida kwa jamii kama ilivyo kwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

 Mwenyekiti wa  Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo hicho


Katika majumuisho ya ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii  Mh. Oscar Mukasa(Mb) ameipongeza wizara na taasisi zilizotembelewa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi na kushauri taasisi hizo kujikita katika kusimamia Dira na dhima za uanzishwaji wake. Kamati pia imeshauri Serikali kupitia Wizara kuhahakisha inatoa fedha za miradi kwa wakati kulingana na bajeti. 


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa Mihadhara unaojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.


Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila (Mwenye Tai Nyekundu) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa ukumbi mpya wa mihadhara wa Chuo chicho uliyojengwa kwa fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jami.

Ijumaa, 15 Machi 2019

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI CHUO KIKUU ARDHIKamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza serikali kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 za Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Ardhi zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2018/19.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakibadilishana mawazo na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Oscar Mukasa (MB) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Ardhi.
Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Oscar Mukasa(MB) Jijini Dar es Salaam baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu hiyo ambayo ni ujenzi wa maabara, ukarabati wa karakana, nyumba za walimu, madarasa na kukamilisha ujenzi wa jengo la Lands.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Suzan Lyimo (MB) wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa (Hayupo pichani) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Chuo hicho.
Aidha, Mhe. Mukasa pamoja na Kamati wameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia utekelezaji wa Mradi kwa ubora na weledi mkubwa. Vilevile wamepongeza chuo hicho kwa kutumia vyema wataalamu wake kwenye kutekeleza kazi ya ujenzi.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakipata maelezo ya maendeleo ya ukarabati wa Chuo Kikuu Ardhi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi.
Katika hatua nyingine Kamati imeshauri Serikali kutoa kipaumbele cha kukiendeleza kituo cha utoaji taarifa za viashiria vya majanga yanayoweza kusababishwa na Volcano na matetemeko ya ardhi katika eneo la Oldonyo Lengai. Aidha wameishauri Serikali kuhakikisha Kituo kinapata vifaa vitakavyokiwezesha kufanya kazi ya kutambua viashiria hivyo katika maeneo yote ya nchi na kutoa taarifa hizo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiangalia baadhi ya kazi za mipango miji, usanifu majengo, upimaji na ramani zilizotengenezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi ikiwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa, akitoa taarifa ya utekelezaji kwa Kamati amesema Mradi huo unaogharimu Shilingi Bilioni 2.5 kwa kiasi kikubwa umesimamiwa na wataalamu wa ndani ya Chuo hali ambayo imewezesha kupunguza gharama na ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa wakati .
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wiliam Ole Nasha akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii madarasa yanayoendelea kukarabatiwa (Hayapo pichani) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara katika Chuo Kikuu Ardhi.
Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea mradi na ameahidi kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Kamati.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa akitoa maelezo ya ndege ndogo isiyo na rubani (Drone) inayotumika kwa ajili ya kuchukua picha anga za maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupanga miji, kupima miji, kusaidia wakati wa majanga kama mafuriko na utafiti mbalimbali. Hii ni moja ya jitihada za Chuo Kikuu Ardhi kuboresha teknolojia katika kufundisha na kutatua matatizo katika jamii.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Oscar Mukasa (MB) machapisho ya Chuo Kikuu Ardhi wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu.