Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate-Ole Nasha amefunga
rasmi maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambapo ameilielekeza
baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika
angalau kwa mwaka mara moja.
Naibu
Waziri Ole Nasha amesema kuwa Elimu ya Ufundi ni nyenzo inayomsaidia mtu
kupambana na changamoto ikiwemo kujiajiri na siyo kusubiria kuajiriwa, hivyo
kupitia mafunzo ya ufundi yanawaandaa wahitimu kutatua changamoto mbalimbali
zinazojitokeza katika maisha.
Mhe.
Ole Nasha amesema Serikali ya awamu ya Tano inapozungumzia Tanzania ya viwanda
ni pamoja na kujiandaa kuhakikisha inakuwa na wataalamu wenye stadi na ujuzi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam
Ole Nasha akizungmza na wananchi (Hawapo Pichani) wa Dodoma wakati wa kufunga maonesho ya
kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyofanyika Jijini Dodoma
“Katika
kufikia uchumi wa viwanda Serikali itaendelea kushirikiana na wadau na sekta
mbalimbali katika kujiletea Maendeleo, na ili kufikia lengo hilo ni lazima tuwe
na wataalamu wa kutosha ambao watasaidia kutatua changamoto
mbalimbali,”alisistiza Mhe. Ole Nasha.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE), Prof. John Kondoro amesema madhumuni ya maonesho hayo ni
kutangaza Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu
miongoni mwa washiriki.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam
Ole Nasha na Naibu Katibu Mkuu AveMaria Semakafu wakisikiliza kwa makini
maelezo kutoka kwa Skauti anayeshiriki katika Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya
Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na
Mafunzo.
Prof.
Kondoro amesema miongoni mwa changamoto ni pamoja na muda wa maandalizi kuwa
mfupi na hivyo washiriki wengi kushindwa kujipanga na kuja kushiriki ameahidi
kuwa baraza litajipanga ili kutoa fursa kwa washiriki wengi zaidi kushiriki
katika maonyesho yajayo.
Kauli
mbiu ni “Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda
Tanzania”
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akizungumza na mmoja wa washiriki wa maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo wakati alipotembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma