Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali iko
tayari kulipa madai  ya walimu ambayo
wanaidai serikali endapo madeni hayo yatakuwa yamehakikiwa na kuthibitishwa
kuwa ni madai halali.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Walimu ambao unafanyika katika ukumbi
wa Chimwaga mkoani Dodoma Rais amesema anatambua sana shida za walimu  na kuwa serikali yake iko tayari kupatia
ufumbuzi changamoto hizo.
Rais
Magufuli amesema mpaka sasa tayari Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni
56 kulipa madeni ya walimu na  kuwa kila
mwezi  serikali imekuwa ikituma ruzuku kiasi
cha shilingi bilioni 18 mpaka bilioni 23 kwa ajili ya   kuwalipa walimu.
Rais
Magufuli amewataka walimu na wanafunzi 
kukubali kufanya kazi katika vituo wanavyopangiwa mara wanapohitimu, Pia
amesisitizia suala la mwalimu kutokuhamishwa kituo cha kazi bila kulipwa fedha
yake yote na hivyo amewataka walimu kuzingatia suala hilo.
Akizungumza
kabla ya Kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Ndalichako amewapongeza walimu kwa umoja na mshikamano ambao wamekuwa
wakiuonyesha kupitia chama hicho cha walimu.
Chama
hicho cha walimu kupitia Risala yao imeeleza kuwa inatambua jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kutatua changamoto mbalimbali
zilizopo katika sekta ya Elimu.
Katika
mkutano Rais Magufuli aliwaongoza viongozi wengine kuchangisha  fedha kiasi cha shilingi milioni 60 ambazo
zitagawanywa kwa walimu zaidi ya 1000 ambao wanashiriki mkutano huo.





