·
WAJADILIANA
NAMNA YA KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro Clifford Tandari ameishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kusomesha vijana wengi katika fani ya ufundi ili kupata wataalamu watakaofanya
kazi katika viwanda ili kuendana na sera ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwa
na uchumi wa Kati na wa viwanda ifikapo mwaka 2015.
Tandari amesema hayo Mkoani
Morogoro wakati akifungua Mkutano wa 25 wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia na kusisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais
John Pombe Magufuli imeweka misingi imara itakayowezesha kila Mtanzania kupata
Elimu bora na yenye tija kwa Taifa ili kufikia malengo ya Taifa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro Clifford Tandari akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa 25 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mkoani Morogoro.
Akizungumza na baraza hilo
la Wafanyakazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard
Akwilapo amesema kufanyika kwa baraza hilo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya
kuwashirikisha wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi na kuwa mkutano
huo pia utapitia na kujadili utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia mwaka 2017/18 na mwelekeo wa bajeti ya mwaka 2018/19.
kwa upande wake Katibu wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Gerald Mweli amesema Baraza hilo ndio
chombo cha juu kabisa cha sheria ya majadiliano kazini kinachojumuisha
wafanyakazi wote kujadiliana kwa pamoja mafanikio, changamoto na kuweka mipango
ya namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Viongozi
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwa wameshikana mikono kuonesha
umoja wao wakati wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Mkutano huo wa siku mbili
ulioanza leo utakamalizika kesho ukiwa na kauli mbiu inayosema “Elimu Jumuishi, Sayansi na Teknolojia ni
Msingi wa maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Viwanda Tanzania".
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akizungumza na
wajumbe wa mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia (hawapo pichani), ambapo amesisitiza suala la Umoja, Upendo na
ushirikiano mahali pa kazi. (hawapo pichani)