· EP4R IMEONDOA ADHA YA VYOO ILIYOKUWA INAIKABILI SHULE
YAMBAWALA
Mkuu wa shule ya Ufundi Mtwara
Paul Kaji amepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha miundombinu ya
shule hiyo na hivyo kuondoa kabisa changamoto mbalimbali zilizoKuwa kikwazo kwa
wanafunzi na walimu shuleni hapo.
Kaji ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na timu ya wanahabari waliofika shuleni hapo kwa lengo la kuangalia
ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo ambapo zaidi ya bilioni moja imetumika
kukarabati vyumba vya madarsa, ofisi za walimu, mabweni, Bwalo la chakula,
sehemu za kuandalia chakula (majiko), kukarabati njia Maalumu za wanafunzi
wenye ulemavu, kurejesha miundombinu ya umeme na Maji katika hali ya kawaida.
Pia baadhi ya wanafunzi
waliohojiwa wameelezea kufurahishwa na ukarabati huo na hivyo kuwafanya kuwa katika
mazingira mazuri ya kusomea.
“Tunaishukuru Serikali kwa
kutuboreshea miundombinu ya shule siyo tu shule yetu imependeza bali hata sisi
tuna uwezo wa kusoma muda wowote kwa kuwa umeme upo, tunawasilisha shukrani na
hivyo tunaahidi tutasoma kwa bidii ili tufaulu vizuri” anasema David Andrew
mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo ambaye anasomea fani ya
ujenzi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbawala Ali
Haroun amesema licha ya kujenga madarasa mapya lakini jambo ambalo limeleta
heshima kwao ni ujenzi wa matundu ya vyoo.
Alisema katika fedha hizo wamejenga matundu ya vyoo 10 na
kufanya jumla ya matundu ya vyoo kuwa 16 na madarasa 8 jambo ambalo limesaidia
kuongeza wanafunzi na kila darasa kukaa wanafunzi kulingana na ukubwa wa
darasa.
Hata hivyo aliongeza kuwa matundu ya vyoo yamewasaidia katika
kuhakikisha walimu wanakaa shuleni muda wote kuliko hapo zamani ambapo ilikuwa
ni lazima kwenda kujisaidia majumbani kwao.
‘’Hapo awali kulikuwa na shida kabisa kwani walimu walikuwa
wanafika shuleni wakijisikia kubanwa na haja wanakimbilia nyumbani na kuwafanya
kuchukua muda mwingi hadi wa vipindi ndipo wanarejea shuleni kwa ajili ya
kuendelea na masomo,’’
‘’ Programu hii ni mkombozi kwetu kwani hata wanafunzi waliokuwa
wakikaa katika madarasa kwa kubebana sasa wanakaa kwa nafasi na mpaka chumba
kimoja kimebaki kwa kukosa wanafunzi,’’aliongeza mwalimu Ally.
Mwalimu wa darasa la awali katika
Shule ya Msingi Msijute Mariamu Milanzi akifundisha kwa kutumia zana zilizowekwa
katika darasa darasa la awali. Matumizi ya Zana za kufundishia unasaidia watoto
kuelewa kwa urahisi kupenda shule na kupunguza utoro.
Naye mwalimu, Isabela Mwambona alisema mradi huo umewarahisishia
kazi kutokana na kufundisha kwa nafasi na hata kuwafikia
wanafunzi mmoja baada ya mwingine kwa ufundishaji.
Katika hatua nyingine programu ya Kusoma, Kuandika
na Kuhesabu (KKK) imezaa matunda katika shule mbalimbali za Mkoa wa
Lindi na Mtwara.
Isabela alisema tangu wapeate mafunzo ya ufundishaji wa KKK
kwa kutumia vitendo na michoro kwa sasa wamefanikiwa kupunguza idadi ya
wasiojua Kusoma na Kuandika shuleni hapo.
Wanafunzi wa Darasa la Awali katika shule ya Msingi Msijute wakiwa
darasani tayari kwa kuanza masomo.