Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema nchi inahitaji rasilimali
watu yenye ufahamu na ujuzi stahiki katika kujenga uchumi wa viwanda.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kongamano na maonesho ya Wahandisi wanawake wa Taasisi ya
Wahandisi Jijini Dar es Salaam Ndalichako amesema Wizara yake imeweka mikakati
mbalimbali ili kuhakikisha nchi inakuwa na rasilimali watu ya kutosha, wenye
ujuzi utakaowawezesha kuchangia maendeleo ya Taifa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wa washiriki
wa Kongamano na Maonesho ya Wahandisi Wanawake wa Taasisi ya Wahandisi iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam. Amesisitiza Wahandisi hao kuweka katika vitendo tafiti
zao ili kuwasaidia wananchi katika kutatua changamoto.
“Tunao
mradi wa Mkakati wa Kukuza Staadi za Kazi (ESPJ unaotekeleza Mkakati wa Kujenga
Ufahamu na Ujuzi katika maeneo muhimu ya kiuchumi kwa Taifa, miongoni mwa
maeneo hayo ni kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo; viwanda,
usafirishaji, Tehama, nishati, ujenzi na maeneo ya utalii na huduma ambayo
uhandisi una mchago mkubwa.” Amesisitiza Ndalichako
Aametoa
wito kwa wahandisi hao kuhakikisha wanafanya jitihada zaidi ya kutafuta njia za
kuendeleza matokeo ya tafiti wanazofanya na kuziweka katika vitendo ili ziweze
kuchangia ipasavyo ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akitoa zawadi kwa Mhandisi
Mama Kinasha ambaye ni miongoni wa wahandisi wa wa kwanza kusajiliwa na Taasisi
ya Waandisi wakati wa ufunguzi wa Kongamano na Maonesho ya Wahandisi Wanawake
wa Taasisi ya Wahandisi iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo
kutoka kwa mmoja wa washiriki wa maonesho ya ubunifu katika toa ufunguzi wa
Kongamano na Maonesho ya Wahandisi Wanawake wa Taasisi ya Wahandisi
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.