Waziri wa Elimu, Sayamsi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amehaidi kujenga na
kuboresha miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi ya
Kiomboni ambayo miundombinu yake kwa sasa ni chakavu.
Waziri Ndalichako ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya Shule hiyo iliyopo katika Kijiji cha Kiomboni
Kata Salawe Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.
Amesema kuwa shule hiyo pamoja na kuwa chakavu ina
upungufu wa vyumba vya madarasa hvyo kupelekea hali ya ufundishaji na
ujifunzaji kuwa ngumu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikaribishwa na baadhi ya viongozi na wananchi wa Kijiji wa Kiomboni Wilayani Kibiti mkoani Pwani alipowasili katika kijiji hicho ili kujionea changamoto zinazoikabili shule ya msingi ya Kiomboni. Waziri Ndalichako aliwahaidi wanakijiji hao kuwa serikali kupitia wizara yake watajenga miundombinu mipya katika shule hiyo
"Nimezinguka katika shule hii nimejionea kwa macho
yangu jinsi miundombinu yake ilivyo kwenye hali mbaya na ninaahidi kuwa wizara
yangu itafanya uboreshaji wa miundombinu hii ili mazingira ya kujifunzia yaweze
kuwavutia watoto kupenda shule " Aesema
Ndalichako.
Waziri huyo amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia
kuboresha miundombinu ya Shule kwa kukarabati na kujenga mipya ili kuwezesha
watoto kjifunza katika mazingira rafiki.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na viongozi wa
wilaya ya Kibiti wakikagua miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo ya shule ya msingi kiomboni ambayo yamechakaa.
Waziri huyo yupo wilayani Kibiti katika ziala ya kukagua miradi ya elimu
inayotekelezwa na wizara ya elimu kupitia programu ya EP4R
Ndalichako amewahakikishia walimu wa shule hiyo pamoja na
wanakijiji kuwa ujenzi na Ukarabati huo utafanyika mapema kabla ya mvua za
masika hazijaanza.
Awali katika taarifa yake Mkuu wa shule Musa Mapange alimweleza Waziri kuwa Shule hiyo haina vyoo
imara kwani vilivyokuwepo vimeharibika na kufungwa na sasa watoto wanajisaidia
katika vyoo vilivyotengenezwa kwa dharula.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako, Mbunge wa Kibiti
Ali Ungando na Mkuu wa Wilaya hiyo Philiberto Sanga wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule msingi
kiomboni. Ndalichako amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii.
Waziri Ndalichako upo katika ziara ya siku mbili ya kikazi
Wilayani Kibiti mkoani Pwaniku kagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na wizara
Kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R)