Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia mheshimiwa William Ole Nasha ameiagiza
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)
kuhakikisha inakamilisha uratibu wa
udahili wa wanafunzi wa Elimu ya Juu ili kuwezesha zoezi la upangaji wa mikopo
kufanyika katika muda uliopangwa.
Naibu
Waziri ametoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa TCU jijini Dar es Salaam ili kupata taarifa ya
maendeleo ya udahili huo ambapo amesema kukamilika mapema kwa taratibu za udahili
itawezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi hao
mapema.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha akizungumza na viongozi wa Tume ya
Vyuo Vikuu nchini alipokutana nao Jijini Dar es Salaam ili kupata taarifaya
uratibu wa udahili wa wanafunzi wa Elimu ya juu.
“TCU
mkifanya vibaya katika uratibu wa udahili Bodi ya Mikopo ndio inayoathirika
kwani lawama zote huishia huko na siyo
TCU, hivyo ili kuweka utaratibu mzuri ni vyema mkafanyakazi kwa ukaribu na
kushirikiana ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza,” amesisitiza Naibu
Waziri huyo.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri amekutana na watendaji wa Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kuwataka kuhakikisha wanashughulikia
kwa haraka upangaji na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na
kuwasadia wanafunzi pale zinapotokea changamoto .
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul Razaq Badru akizungumza na Naibu
Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha wakati wa
kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.