Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Consolata Mgima ameitaka idara ya
Ukaguzi wa Shule kusimamia ubora wa Elimu nchini, kwa kuhakikisha kuwa sera,
sheria, kanuni na viwango vya elimu vilivyowekwa katika mfumo wa utoaji elimu
vinazingatiwa ipasavyo kwa kuhakikisha mitaala na viwango vya elimu
vilivyowekwa vinafuatwa ili kuongeza ufanisi na ubora katika elimu.
Akizungumza katika
mkutano wa viongozi wa Elimu uliofanyika mjini Morogoro hivi karibu uliokuwa
ukijadili kuhusu umuhimu wa uanzishwaji wa mfumo wa Menegement ya Habari na Mawasiliano katika Idara ya Ukaguzi wa Shule unaotekelezwa kwa
kusirikiana kati ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na Shirika linalohudumia Watoto Duniani UNICEF, alisema Kwa kutambua
hilo, wizara imekuwa ikiiwezesha ukaguzi wa shule kwa kuongeza wakaguzi wa
shule, vitendea kazi na kuongeza vyombo vya usafiri.
Naibu Katibu
Mkuu alisema Uanzishwaji wa mfumo wa Menejimenti ya Habari na Mawasiliano wa
Idara ya Ukaguzi wa Shule, unategemewa kuwa utaleta mafanikio makubwa katika
upatikanaji wa yale yaliyojiri baada ya shule kukaguliwa. Mafanikio hayo yatawezesha wadau wengi kupata
taarifa za ukaguzi kuliko ilivyo hivi sasa.
“Aidha, ni
ukweli usiopingika kuwa suala la ubora wa elimu ni la ushirikishwaji wa wadau wote
katika ngazi zote ikiwemo jamii hivyo naipongeza idara ya ukaguzi wa shule
pamoja na UNICEF kwa mkakati waliokuja nao wa kuanzisha vituo vya mafunzo vya
jamii katika kata, kwa uhakika jamii ikishirikishwa katika hatua
za awali elimu itaimarika.”
Alisisitiza Naibu Katibu Mkuu
Akizungumzia
Mfumo huo Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Ukaguzi wa shule Dkt. Edicome Shirima
alisema utekelezaji wa mfumo ulianza Augusti 2011 ukitekelezwa katika kata 35
zilizo katika wilaya 7 za majaribio (Pilot). Wilaya hizo ni Bagamoyo, Hai,
Makete, Magu, Siha Temeke na Mtwara Vijijini.
“Lengo
ni kuweka taarifa za Ukaguzi wa shule katika
kanzidata (data base) itakayoonesha shule na ubora wake (School -Level
Quality Assurance Data)”. Alielezea Dkt. Shirima
Taarifa
hizo zilizomo katika mfumo huo zinaweza
kuonwa na wadau wote wanaohitaji
kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Aidha zitasaidia Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa kutoa maamuzi mbalimbali yanayohusu elimu. Baada ya kukamilika kwa uandaaji wa mfumo wa (IMIS) utaingizwa katika
Mtandao mkubwa wa Elimu Kisekta (ESMIS)
Akifafanua jinsi data hizo zinavyokusanywa Dkt
shirima alifafanua kuwa Katika
maandalizi ya IMIS, orodha hakiki
inayotumika Katika ukaguzi wa shule wa jumla huchambuliwa kwa ufasaha na kuwekwa katika mtirirIko mzuri utakaowezesha data
zitakazokuwa zimekusanywa kupitia vyanzo mbalimbali kama vile
sensa ya uandikishaji kwa darasa la
awali na darasa la kwanza na hatua za Ufundishaji (lesson observation)
kupatikana na kutumika Katika uandikishaji na kuboresha ufundishaji. Haya
yote yamefanyika kwa kuzingatia viwango vya msingi vya elimu (Basic Standard)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi Dkt. Shirima
alisema zana za kukusanyia taarifa
imendaliwa Katika mifumo miwili ambayo ni Fomat A kwajili ya msimamizi wa shule na Fomati B kwa ajili ya mkaguzi wa shule, ambayo itaonesha
pia hatua za Ufundishaji darasani (lesson observation)
Orodha hakiki zote zitaonesha kipengere
kinachohitaji marekebisho Katika utendaji
Walengwa wa Uanzishaji wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano umewalenga Waratibu Elimu Kata na Wakaguzi wa
Shule kwa kuwa ni wadau muhimu Katika usimamizi wa elimu, hivyo
wamepewa jukumu kubwa Katika kusimamia na kuhakikisha ubora wa elimu unapatikana.
“Mratibu Elimu wa Kata kama msimamizi wa shule
aliye karibu na shule akisaidiana na mwalimu mkuu ambaye ni msimamizi wa shule
wa ndani. Kwa pamoja wana nafasi kubwa sana katika kusimamia
elimu Katika maeneo yao. Kwani wataweza kutayarisha taarifa na kuzitoa kwa
wadau kwa wakati, vilevile zitawasaidia
wakaguzi wa shule kufahamu mahali gani panahitaji marekebisho au kutiliwa mkazo.” Alisisitiza
Dkt. Shirima
Lengo
linguine la Mfumo huu ni kuzifanya jamii zinazoizunguka shule kutambua kuwa
shule ni sehemu yake na hivyo kuhusika moja kwa moja katika katika kufuatilia
maendeleo ya shule. Ili kuhakikisha kuwa jamii
inashirikishwa kikamilifu.
“Ili
kufikia lengo la kushirikisha jamii vimeanzishwa vituo vya mafunzo ngazi ya kata
“Community Learning Centers (CLC)”.
Katika vituo hivyo, jamii inapata nafasi
kusoma taarifa za shule, kutoa
maoni na kurekebisha mapungufu yaliyo
ndani ya uwezo wao. Fursa hii itaongeza uwajibikaji wa menejimenti na kamati
za shule kwa jamii.” Alifafanua
Dkt. Shirima