Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha
Taarifa ya Utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2017/18 na Makadirio ya Bajeti kwa
mwaka 2018/19 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Uwasilishaji wa taarifa hiyo umefanyika leo katika ofisi
za Bunge zilizopo Mkoani Dodoma ambapo
wajumbe wa Kamati hiyo wamepata fursa ya kupitia na kujadili Fungu 46.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro.Joyce Ndalichako akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji 2017/18 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka 2018/19 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Makamu Mwenyekiti wa kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Juma Nkamia akisitiza jambo
wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya utekelezaji na Makadirio ya Bajeti ya
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2018/19 Mkoani Dodoma.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Taarifa ya
utekelezaji na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kwa mwaka 2018/19.