ALIYOYAZUNGUMZA NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM PROF. BONAVENTURE RUTINWA KATIKA KIPINDI CHA JAMBO TANZANIA LEO TBC.
1. Wale wote waliiomba Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam (UDSM) wakafutiwa udahili kwa sababu ya kuwa wengi zaidi
(over capacity) wamerudishwa wote bila masharti yoyote.
2. Prof. Rutinwa ameeleza kuwa wale
walioko Dar es Salaam waendelee kuchukua barua zao za udahili (admission
letter) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wale walioko mbali na Dar es
Salaam watazipokea barua zao kuanzia tarehe 27/10/2018 watakapofika kwa
usaili.
3. Wataalamu wa mifumo ya
kompyuta wanaandaa utaratibu ili waliodahiliwa wapokee barua zao kwenye akaunti
zao za udahili.
4. Wanafunzi ambao wamekosa code
au wameshindwa kuingiza codes UDSM au vyuo vingine watapewa utaratibu wa kwenda
chuo wanachokitaka.
5. Kutakua na dirisha la wale
waliokosa nafasi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sababu ya Program hizo
kujaa wapate nafasi ya kuomba tena.
6.Serikali imeendelea kuboresha
Miundombinu katika Chuo hicho ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vyumba
vya madarasa na maabara kwa hali ya juu na ya viwango kwa ajili ya kuhudumia
wanafunzi ambao chuo hicho inataka kuwadahili.
7. Serikali pia inaendelea
kukiwezesha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuongeza idadi ya Wahadhiri wabobevu
ili kukidhi uhitaji.
8. Leo ilikuwa ni siku ya mwisho
kufunga udahili lakini mara baada ya kufanya kikao na Mhe. Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alielekeza kuongezwa kwa siku hizo
ili kutoa fursa zaidi kwa wanafunzi.
9. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kinamshukuru sana Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako kwa kusaidia kutatua changamoto iliyokuwepo katika udahili kwa
UDSM.