Alhamisi, 15 Novemba 2018

DKT. AKWILAPO AZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU KUFANYA TAFITI ZA KITAALAMU


Serikali imezitaka Taasisi za Elimu ya Juu nchini kutimiza wajibu wake wa kufanya tafiti za kitaalamu kwa kushirikiana na wadau ili kuongeza ufahamu kwa jamii na kuisaidia serikali kwenye kutunga na kusimamia sera utungaji na usimamizi wa sera mbalimbali za nchi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Katibu MkuuWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka waWadau wa Tafiti kwa Maendeleo shirikishi uliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amezitaka Taasisi zinazohusiana na Tafiti kutafuta namna ya kufikisha matokeo ya tafiti hizo kwenye jamii kwa lengo la kuwaletea wananchi Mabadiliko na Maendeleo.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na wadau waElimu kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa wadau wa tafiti kwa maendeleo shirikishi uliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo amezita kataasisi za elimu ya juu kufanya tafiti ili kuisaidia serikali  kutunga sera.



“Hakuna asiyefahamu kuwa Elimu ni chombo muhimu kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii, na kuwakupitia Elimu ndiyo njia pekee inayoweza kutoawataalamu wenye ujuzi wa kusaidia jamii kwenye kilanyanja, hivyo ni wakati muafaka kwa Taasisi za Elimu kulitambua hilo na kujua nyakati za sasa zinahitaji pia ufahamu wa masuala ya kidijitali,”alisistiza Dkt. Akwilapo.

Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg, amesema Shirika la Maendeleo la Kimatiafa (SIDA) litaendelea kuisaidia Tanzania kujikwamua kiuchumi hususani kwenye viwanda kupitiakazi za kitaaluma kupitia Shirika hilo.

Akizungumza katika mkutano huo wa mwaka wa Wadau wa Tafiti kwa Maendeleo shirikishi Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Cuthbert Kimambo amesema ni dhahiri kuwa nchi ya Sweden imekuwa na mshusiano na ushirikiano mzuri na Tanzania katika sekta ya Elimu, na kupitiamradi huo unaojumuisha UDSM, ni hatua nzuri yakuisaidia serikali na wananchi kwa ujumla kufanyashughuli zao kitaalamu na kufikia Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akiangalia na kupata maelezo kuhusu ufugaji wa samaki mara baada ya kufungua mkutono wa Kwanza wa mwaka wa wadau wa tafiti kwa maendeleo shirikishi uliofanyika jijini Dar esSalaam.

Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) unawashirikishawatunga sera, wadau kutoka sekta ya umma na binafsi.


Jumatano, 14 Novemba 2018

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA MWONGOZO NA MASHINDANO YA UBUNIFU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua mwongozo na mashindano ya ubunifu kitaifa mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi Waziri Ndalichako amesema lengo la mashindano hayo ni kutambua na kuendeleza fikra za wabunifu kwa lengo la kuongeza ajira.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma za Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba Mwongozo wa ubunifu mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dodoma.



Prof. Ndalichako amesema katika kuimarisha uchumi wa viwanda lazima matumizi ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaimarishwe kwa lengo la kuongeza tija viwandani na kwenye biashara.

“Kutoka na umuhimu wa mashindano haya naielekeza Idara ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kila mwaka, ili kukuza ujuzi, wabunifu kwa maendeleo ya viwanda,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba wakionesho mwongozo wa Ubunifu mara baada ya Kuzinduliwa leo Jijini Dodoma.

Mashindano hayo yameshirikisha Makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo Shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi, Sekta isiyo rasmi, Vyuo vya ufundi wa Kati, Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za utafiti na Maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa kuzinduliwa kwa mwongozo huo ni jambo kubwa na la kihistoria ikizingatiwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda.
 Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakifurahia mara baada ya Mwongozo na Mashindano ya Ubunifu Kuzinduliwa leo Jijini Dodoma.


Serukamba amesema bila Sayansi, Teknolojia na ubunifu nchi haiwezi kufanikisha malengo yake, hivyo ameiomba Serikali ihakikishe inawekeza fedha nyingi.

“Kama hatutawekeza fedha za kutosha kwenye Sayansi, Teknolojia na Ubunifu hatuwezi kufanya kitu, hivyo tuwekeze fedha za kutosha ili tujiletee Maendeleo kwa haraka,” amesema Mhe. Serukamba.

Kauli mbiu ya mashindano hayo ni “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda.”
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Dodoma Mwongozo wa Ubunifu mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dodoma.

Jumamosi, 10 Novemba 2018

WAZIRI NDALICHAKO AVITAKA VYUO KUFUATA MIONGOZO KATIKA KUTOA ELIMU



Serikali imevitaka vyuo vyote vya Elimu ya Juu nchini kuzingatia kanuni na miongozo  inayotolewa na Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE) na Tume ya vyuo  Vikuu Nchini (TCU) katika kutoa elimu ili kuepuka  kufungiwa au kufutiwa udahili.

Kauli hiyo ya serikali   imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam, ambapo amesema serikali kupitia TCU na NACTE itaendelea kusimamia ubora wa Elimu na kuvifungia vyuo vyote vinavyotoa elimu chini ya kiwango.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika maandamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam.

Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya Vyuo ambavyo vimekuwa havifuati taratibu na miongozo inayotolewa na TCU na NACTE na kusababisha usumbufu kwa wanafunzi pale vinapotakiwa kufungiwa, na kusisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi hizo  ni endelevu na kuwa lengo ni kuhakikisha wahitimu wanapata Elimu bora itakayowawezesha kujiajiri ama kuajiriwa.

 Waziri Ndalichako pia amewataka Wahadhiri wenye tabia yakuficha matokeo ya wanafunzi kwa madai ya kukosa maslahi yao kutoka kwa mwajiri  kuacha mara moja tabia hiyo kwani imekuwa ikiwasumbua wanafunzi ambao hawana hatia.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wahitimu katika mahafali ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam amewataka kuwa wanafunzi kuwa mabalozi wazuri na wazalendo katika kazi zao baada  ya kuajiriwa ama kujiajiri.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha CBE Prof. Emanuel Mjema amesema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uvhakavu wa miundombinu kutokana na Chuo hicho kuwa  cha muda mrefu,  hivyo Marion a serikali kukipatia udhamini ili kiweze kukopa katika Taasisi za fedha ili kuboresha miundombinu hiyo.




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimbalisha  mmoja wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo katika mahafali ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam.

Ijumaa, 2 Novemba 2018

SERIKALI KUTOA MWONGOZO WA USAMBAZAJI KOMPYUTA SHULENI


Serikali imesema inatarajia kutoa mwongozo wa utaratibu wa kusambaza kompyuta na vifaa vyake katika shule za msingi na sekondari ili kuwezesha vifaa hivyo kutambuliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi  kwa shule ambazo  zitakuwa zimepatiwa vifaa hivyo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya TEHAMA yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo amesema kwa sasa ni vigumu kwa serikali kujua ni shule ngapi zenye kompyuta ama taasisi zinazotoa misaada ya kompyuta shuleni.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza na washiriki wa mafunzo ya TEHAMA (hawapo Pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka washiriki hao kutumia maarifawaliyoyapata katika kuboresha Elimu
“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakaa pamoja na Ofisi ya Rais Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa ili tuweze kuweka mwongozo ambao utawezesha serikali kutambua taasisi zote zinazojishughulisha na usambazaji wa kompyu takatika shule pamoja na kutambua shule zilizo na kompyuta ili iwe rahisi kuziratibu”amesema Prof. Mdoe.

Akizungumza na Walimu walioshiriki mafunzo hayo amewataka kuhakikisha wanatumia  maarifa waliyoyapata katika kuboresha elimu na kuimarisha utendaji  wa kazi  ili kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Pius Joseph amesema mfuko wa Mawasiliano kwa wote ina jukumu la  kuhakikisha ina ziunganisha shule zote za msingi na sekondari katika mtandao wa inteneti, pamoja na kutoa vifaa na mafunzo kwa walimu wanaofundisha masomo ya TEHAMA .

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akimkabidhi cheti cha kumaliza mafunzo ya TEHAMA mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 Mfuko  huo wa Mawasiliano tayari umetoa  mafunzo yaTEHAMA kwa  walimu 578 kutoka mikoa yote ya Tanzania pia umetoa kompyuta 425 kwa shule za msingi,  komputa 1250 kwa shule za sekondari  na kuwa vifaa hivyo vimetolewa katika  kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.

Jumatano, 31 Oktoba 2018


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Anuani ya simu “ELIMU”
Simu: 026  296 35 33
Baruapepe:info@moe.go.tz
Tovuti: www.moe.go.tz



  
Chuo cha Masomo ya  Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jengo Na. 10,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.           



TAARIFA KWA UMMA
KUFANYA MALIPO KUPITIA MFUMO MPYA WA SERIKALI WA GePG
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuutaarifu Umma ya kwamba kuanzia tarehe 01 Novemba 2018, itahamia rasmi katika mfumo wa kukusanya mapato ya Serikali kwa njia ya kieletroniki ujulikanao kama ‘Government e-Payment Gateway’ (GePG) kwa matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma, Sura 348.

Wizara, itaanza kutumia mfumo huu kwenye makusanyo yake yote ya mapato kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Kanda za Uthibiti Ubora wa Shule. Hivyo mteja atapaswa kufika au kuwasiliana na kituo husika anachotaka kufanya malipo ili kupata namba ya utambulisho wa malipo husika (Payment Control Number) kabla ya kufanya malipo.

Wizara kwa kushirikiana na Wataalamu wa mfumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri utoaji wa huduma. Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaungana na Wizara na Taasisi nyingine za Serikali zinazotumia mfumo huo kwa mafanikio. Baadhi ya Wizara na Taasisi hizo ni Polisi, Brella, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, TRA, Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) pamoja na Mamlaka ya Maji.
Namna ya kulipa kwa kutumia mfumo wa kieletroniki (Government e-Payment Gateway);
1.   Malipo yanaweza kufanywa kwa njia ya kibenki kwa kufuata hatua zifuatazo;
a)     Unapopata kumbukumbu ya malipo (Control Number);
b)     Tembelea Tawi lolote la Benki ya CRDB, NMB na NBC;
c)      Baada ya kuwasili kwenye benki, mpe mtoa huduma wa dirishani namba kumbukumbu ili kukamilisha mchakato wa malipo yako.

2.    Malipo yanaweza pia kufanywa kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi (M-pesa, Tigo Pesa na Airtel Money) kwa kufuata hatua zifuatazo;
a)     Kupitia simu yako, piga *150*00#, au *150*01# au *150*60#;
(Kupata M- pesa, Tigo Pesa na Airtel Money);
b)     Chagua ‘Lipia malipo (Pay-Bills)’;
c)      Chagua ‘Malipo ya Serikali’;
d)    Chagua ‘Ingiza namba ya malipo’ na uingize namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number);
e)     Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa;
f)      Thibitisha muamala wako kwa kuingiza neno au namba yako ya siri; na
g)     Hifadhi ujumbe wa simu uliopokea kama ushahidi wa malipo endapo utahitajika kuonyesha kwa kituo husika.

Imetolewa na;

Dkt. Leonard D. Akwilapo
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


Jumanne, 30 Oktoba 2018

WABUNGE WAIPONGEZA WIZARA YA ELIMU KUSIMAMIA VIZURI PROGRAMU YA LIPA KULINGANA NA MATOKEO


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo leo amewasilisha taarifa ya tathmini ya Ubora wa elimu kutokana na Utekelezaji wa Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.


Akiwasilisha tathmini ya programu ya EP4R kwenye Kamati hiyo ya Bunge Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa programu imekuwa na mafanikio tangu ilipoanza kutekelezwa mwaka 2014.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwasilisha taarifa ya tathmini ya ubora wa Elimu kutokana na utekelezaji wa Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo wakati wa kikao na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii jijini Doodma.

Dkt. Akwilapo amesema fedha zinazopatikana kutokana na utekelezaji wa vigezo (DLRs) katika ngazi ya Serikali kuu na serikali za Mitaa ni kuwa fedha hizo hutumika katika kuboresha utoaji wa elimu nchini kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu mipya.

Dkt. Akwilapo ameieleza kamati hiyo ya Bunge kuwa programu ya EP4R ni ya miaka minne na inatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, Serikali ya Sweden (SIDA) na Serikali ya Uingereza (DFID) na kuwa mradi huo utakamilika 2020.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Peter Serukamba na Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe wameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo wa EP4R ambao umekuwa na matokeo chanya katika nchi.

“Katika kusimamia Programu hii ya EP4R, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya kazi nzuri na matokeo yanaonekana. Miundombinu imeboreka sana,” alisema Mhe. Hussein Bashe.

Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) Jijini Dodoma


Taarifa zinazowasilishwa kwenye kamati hiyo ni pamoja na ile ya mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo, taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na utekelezaji wa shughuli za Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni, jijini Dar es salaam.

Kikao hicho cha siku tatu kimeanza leo na kitakamilika Novemba 1, mwaka huu.

PROF NDALICHAKO: TATUENI CHANGAMOTO ZENU KIMIFUMO


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewashauri watumishi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto za mikopo ya Wanafunzi kwa njia ya mifumo.
Waziri Ndalichako amesema hayo jijini Dar Es Salaam alipotembelea ofisi ya HESLB lengo la kujiridhisha na hali ya mwenendo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (mwenye koti la samawati) akiongea na wateja waliofika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dar es Salaam kurejesha madeni yao ya mikopo ya Elimu ya juu.
Katika ziara hiyo licha ya kukutana na Menejimenti ya HESLB, Prof. Ndalichako pia aliongea na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Profesa Charles Kihampa kuhusu hali ya udahili wa Wanafunzi wa Elimu ya juu ambapo Kihampa alitumia nafasi hiyo pia kukabidhi orodha ya Wanafunzi 2,600 ambao udahili wao umethibitishwa.
Awali katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru ilisema kiasi cha shilingi bilioni 98.12 mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 27,929 kati ya wanafunzi 40,485 wa mwaka wa kwanza waliotarajiwa kupatiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (Katikati) akitambulishwa kwa Maafisa Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Abdul-Razaq Badru.
Badru alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 12,556 watapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 42 katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyokusudiwa.

Aliongeza kuwa idadi ya wanafunzi 27,929 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika ni asilimia 69 ya wanafunzi 40,485 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao  27,929 (Awamu ya kwanza 25,532 na awamu ya pili 2,397) waliokwishapangiwa mikopo inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz  na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo hiyo.