Ijumaa, 14 Desemba 2018

SERIKALI YATOA MAELEKEZO UJENZI WA VETA SIMANJIRO


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia WilliamOle Nasha ameitaka Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo Cha VETA Wilayani humo ili miundombinu ya chuo hicho ijengwe kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirikala Maendeleo ya Hiari ECLAT.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi kuhusu namna walivyojipanga kujenga Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya katika eneo la Mradi la Emboreet lililoko katika Wilaya hiyo.
Alisema ni vizuri Mamlaka husika zikahusishwa katika ujenzi wa Chuo hicho kuanzia hatua za awali na kumtaka Mkurugenzi wa kanda  hiyo na yule wa Mkoa kufika katika eneo la Emboreet ambako mradi utajengwa ili kuzungumza  na wananchi ili mradi utekelezwe kwa utaratibu  unaostahili.

“Mnataka kujenga chuo cha Ufundi ni wazo zuri lakini ni lazima kijengwe kwa utaratibu sio kiholela kwa sababu kumeanza kuibuka utitiri wa vyuo ambapo mtu anakuwa na jengo moja anakutana chuo, kuna viwango na masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla chuo kuruhusiwa kufanya kazi kwa hiyo na nyinyi fuateni taratibu hizo ili muweze kuanzisha chuo cha Ufundi,” alisisitiza Naibu Wazizri Ole Nasha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kitwai A aliyefanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2018. Shule ya Msingi Kitwai A imefaulisha wanafunzi 25 kati ya 28 waliofanya mtihani mwaka huu. 
Mheshimiwa Ole Nasha amesema Serikali ya Awamu ya Tanoimeweka mkazo mkubwa katika Elimu ya Ufundi kwa kuwa kuna vijana wengi wanaomaliza shule wanaishia kutokuwa na ajira kwa kuwa hawana maarifa yanayowasaidia kupata ajira hasa pale wanapokosa fursa ya kuendelea na elimu ya juu hivyo ujenzi wa vyuo vya ufundi vingi utasaidia kuwajengea vijana  uwezo wa kujiajiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi alisema wazo la kuanzisha  kwa Chuo hicho kutawawezesha vijana  kupata maarifa ya kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

Naye Meneja Mradi ya ECLAT Bakiri Angalia alisema  pamoja na shirika hilo kushiriki ujenzi wa Chuo hicho  pia  imefadhili miradi ya Elimu yenye thamani ya  zaidi ya sh bilioni 3 katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wakazi wa Kata ya Kitwai A iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amewataka kuhakikisha wanawandikisha shule wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule bila kuwaacha nyumbani na kuwapangia majukumu mengine.

DKT. AKWILAPO: SEKTA YA ELIMU INA MAFANIKIO MAKUBWA KWA SASA


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amesema Serikali ya awamu ya Tano ya inatambua mchango na juhudi zinazofanywa na shule zinazoendeshwa na makanisa hapa nchini (CSSC) ikiwa ni pamoja na baadhi ya shule kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani na kutoa malezi bora kwa watoto.

Dkt. Akwilapo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wakuu wa Shule za Sekondari za Makanisa na kueleza kuwa mafanikio ambayo yamepatikana katika sekta ya elimu hivi sasa ni makubwa ukilinganisha na wakati nchi inapata uhuru.
Wakuu wa shule za Sekondari za Makanisa  hapa nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wenye lengo la kujadili mafanikio na Changamoto katika shule wanazozisimamia.mkutano huo wa siku mbili unafanyika mkoani Dodoma.

Ameeleza kuwa  Wakati nchi inapata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na  shule 3,238  lakini hadi kufikia mwaka 2018  zipo  shule za elimu ya  msingi 17,704 zilizosajiliwa , Elimu ya sekondari zilianza shule 41, lakini sasa kuna  shule  4,963 zilizosajiliwa   na kati ya hizi  shule  1,266   ni shule binafsi.

Vyuo vya ualimu navyo vimeongezeka kutoka vyuo 3 Lakini sasa kuna vyuo 138  na  kati ya hivyo   103 viko chini ya umiliki wa taasisi binafsi  ambapo  makanisa  wanamiliki  vyuo  15.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akizungumza na Wakuu wa shule za Sekondari za Makanisa wakati akifungua mkutano huo na kueleza kuwa Sekta ya elimu imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu mbalimbali katika sekta hiyo.

“Nawapongeza kwa kutoa huduma na kusimamia elimu, zipo baadhi ya shule zenu ni mfano  katika kufanya vizuri kwenye matokeo, shule za makanisa  pia zinatoa malezi bora kwa watoto kwa lengo la kuwa na viongozi bora na waadailifu wa Taifa la baadae, hii ni juhudi ya kuunga mkono serikali ya awamu ya Tano na serikali yenu inatambua hilo,”alisistiza Dkt. Akwilapo.

Kwa upande wake Mwalimu Petro Masatu ambaye ni Mkurugenzi wa huduma  za elimu CSSC alimweleza Katibu Mkuu baadhi ya changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na suala la upimaji wa watoto /wanafunzi kwa kuzingatia umahiri kutoka darasa moja kwenda jingine kuwa bado kuna utata kati ya shule zisizo za serikali, Wazazi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuchelewa kwa Sekula mpya kwa shule zisizo za serikali ili uwe mwongozo mzuri kwa mwaka 2019 pamoja na kuchelewa kwa sheria mpya ya elimu ambayo yote Katibu Mkuu ameahidi kuyafanyia kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CSSC muda mfupi baada ya kupokelewa na wenyeji wake katika mkutano wa Wakuu wa shule za sekondari za makanisa unaofanyika mkoani Dodoma.

BILIONI 51 KUTUMIKA KUUENDELEZA ELIMU YA UFUNDI NCHINI


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amepokea nakala ya mkataba wa mradi wa kuendeleza ajira na Elimu ya Ufundi kutoka  serikali ya Italia wenye lengo la kuviwezesha vyuo vinavyotoa mafunzo hayo nchini.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam katika ofisi ndogo za Wizara hiyo kupitia Balozi wa Italia nchini Roberto Mengoni ambapo waziri Ndalichako ameahidi kufanya ufatiliaji wa karibu kuhakikisha mkataba huo unasainiwa haraka ili kuwezesha kuanza kwa mradi huo.

Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea nakala ya mkataba wa kuendeleza ajira na Elimu ya Ufundi kutoka kwa Balozi wa Italia nchini Roberto Mengoni, makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri Ndalichako amesema mradi huo ni wa miaka mitano utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 51 na utazihusisha  Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), naTaasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KISS) kushiriki kikamilifu kuchangia katika kufanikisha malengo ya Taifa ya ukuaji wa uchumi .

Aidha, Waziri ndalichako amesema kuanzishwa kwa mradi huo kutavisaidia vyuo kupata vifaa vya kisasa na miundombinu kuboreshwa na hatimaye utoaji wa elimu bora ya ufundi kwenye taasisi shiriki hasa elimu ya vitendo itakayowapa wanafunzi ujuzi utakao wawezesha kujiajiri.
Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa na Balozi wa Italia nchini Roberto Mengoni wakijadili na kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kusoma vipengele vya nakala ya mkataba wa kuendeleza ajira na Elimu ya Ufundi wakati wa makabidhiano ya nakala hiyo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Balozi Roberto Mengoni amesema serikali ya Italia kupitia ubalozi wa nchi hiyo tayari imetuma  mtaalam wake Marcella Ferracciolo kufanya maandalizi ya utekelezaji wa mradi ambapo mpaka sasa mtaalamu huyo ameshatembelea taasisi zote zinazotarajiwa kutekeleza mradi huo.

Jumatano, 5 Desemba 2018

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASEMA SERIKALI IMEJIZATITI KUIMARISHA ELIMU NCHINI


Serikali ya awamu ya Tano imesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kuimarisha na kuboresha Elimu nchini na ndiyo maana sekta hiyo imetengewa fedha nyingi katika bajeti ya Taifa.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha mkoani Morogoro wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wanaosimamia Elimu katika mkoa huo na kueleza kuwa kwa sasa Tanzania ni nchi inayosifiwa kwa kuongeza bajeti ya Elimu kwa asilimia 21.4 ya bajeti ya jumla ya Taifa.
 
“Ninachoweza kusema kwa sasa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka inapokea bajeti yake ambayo ni sh trilioni 1.4 na kwenye fedha za Maendeleo zinapatikana zote kwa asilimia 100 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za Elimu bila kuchelewa yote haya ni kwa sababu Sekta ya Elimu ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha akiongea na viongozi wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mara baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo kukagua miradi ya Elimu.

 Amesema katika miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumefanyika uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya Elimu kuliko wakati wowote na kuwataka watendaji wa sekta hiyo kusimamia fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ya Elimu kwa umakini ili kuweza kubadilisha mazingira ya watoto ya kujifunzia.

 “Wote ni mashahidi kuhusu ujenzi wa miundombinu ya Elimu inayoendelea nchini, Juzi mmeona Mhe.  Rais John Magufuli akifungua maktaba kubwa kuliko maktaba zote Afrika Mashariki na Kati, maktaba yenye uwezo wa kuchukua vitabu laki nane na wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja lakini pia kwenye vyuo vya ufundi na shule pia kuna uwekezaji mkubwa ambao umefanyika wa kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia vyote hivyo ni kwa sababu sekta ya Elimu ni kipaumbele,” alisisitiza Ole Nasha
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha akikagua mradi wa ujenzi ya sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Yanayoonekana hapo ni madarasa ambayo yatakuwa katika mfumo wa ghorofa. 

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kuwa ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa leo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha akikagua majengo ya Chuo cha Ualimu Ilongo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambayo miundombinu yake imefanyiwa ukarabati na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya EP4R.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASISITIZA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ikitumika vizuri katika sekta ya elimu itasaidia kujenga mazingira mazuri na kuwezesha kuwepo kwa mbinu bora katika ufundishaji na ujifunzaji.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam katika halfa ya utoaji wa tuzo  kwa washindi wa mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa mwaka 2018 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Huawei Tanzania, na kusisitiza kuwa  kutumia TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji Mwalimu  mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wengi waliosehemu tofauti.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Huawei Tanzania Emannuel Chaula kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mhe. Majaliwa amewataka wanafunzi kutumia fursa ya mashindano hayo kuendelea kujifunza TEHAMA ili wewe na  uwezo wa kumiliki mifumo  ambayo itasaidia nchi katika kurahisisha utendaji wa shughuli zake kupitia sayansi na Teknolojia

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea kuunganisha mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya serikali ya kurahisisha utendaji kazi.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka vijana walioshiriki katika mashindano hayo kuendelea kujifunza zaidi kwani nchi bado inahitaji Maendeleo katika kipindi ambacho serikali imekusudia kujenga uchumi wa viwanda.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa washindi wa mashindano ya TEHAMA tuzo katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewataka vijana walioshiriki katika mashindano hayo kuendelea kujifunza zaidi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa HUAWEI Tanzania Frank Zhou amesema kabla ya vijana hao kuingia katika mashindano hayo walipatiwa mafunzo ili kuwawezesha kuzitambua Teknolojia za kisasa kwa kuwa Teknolojia  inakua kila siku.

Mashindano hayo ya TEHAMA yalianza na  vijana  500 lakini mpaka mwishoni vijana 10  tu ndio wamefanikiwa kushinda ambapo washindi watatu wa juu wanatarajiwa kwenda katika nchi za Afrika Kusini na China kwa lengo la kujifunza zaidi masuala ya TEHAMA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China na Viongozi wa Taasisi ya Huawei Tanzania wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA 2018 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Jumanne, 4 Desemba 2018

OLE NASHA AWATAKA WALIMU KUBADILI MBINU ZA UFUNDISHAJI

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka walimu nchini kote kuachana na aina ya zamani ya ufundishaji na badala yake watumie mbinu za kisasa ili kusaidia kumuandaa mwanafunzi aweze kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Mheshimiwa Ole Nasha ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya Elimu na kuongea na Viongozi wa Elimu ngazi ya Mkoa ambapo amesisitiza kuwa Elimu ya sasa ni ile ambayo inaendeshwa na matumizi ya Tehama, uongozi mzuri na kubadili mtizamo wa Elimu kutoka katika utaratibu ule ambao mwanafunzi anakuwa mtu wa kupokea na kwenda kwenye mfumo ambapo mwanafunzi anategemewa kushiriki zoezi la ufundishaji.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua samani katika Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yaliyojengwa Wamo Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri huyo pia amesema katika vyuo mfumo unaotumika ni ule wa kumuandaa mwanafunzi kwenda kuajiriwa badala ya kujiajiri mwenyewe hali ambayo inabidi kubadilika ili vijana waweze kumaliza wakiwa wenye maarifa ya kwenda kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

“Katika vyuo vyetu, mfumo wa sasa unaotumika unawafundisha wanafunzi kama watu wa kwenda kufanya kazi baadae badala ya kufundisha watu wa kwenda kutengeneza ajira na ndio maana mwanafunzi akimaliza chuo anakuja ofisini anasubiri umpe kazi, hiyo siyo sawa lazima Elimu yetu iwe ni ya kujenga maarifa ya kujitegemea“ alisisitiza Mhe. Ole Nasha
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wanafunzi wanaosoma katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima iliyoko Wamo mjini Morogoro.  

Naibu Waziri Ole Nasha pia amewataka viongozi wa mkoa wa Morogoro kufuatilia kwa karibu miradi ya Elimu inayotekelezwa katika mkoa huo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Joyce Balavuga alimweleza Naibu Waziri wa Elimu kuwa mkoa wa Morogoro uko mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya Tehama katika ujifunzaji na ufundishaji katika shule zake ili kuinua kiwango cha ufaulu, kutunza kumbukumbu na takwimu mbalimbali za Elimu.

Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya Elimu ambapo kwa leo ametembelea Chuo cha Ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kihonda na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima iliyoko Mkoani Morogoro

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji William Ole Nasha akikagua mradi wa ujenzi wa karakana za ufundi umeme zilizojengwa katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kihonda mjini Morogoro.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY

Tender No. ME-024/2018-19/HQ/G/29

For

SUPPLY OF OFFICE EQUIPMENT FOR SCHOOL QUALITY ASSURANCE DEPARTMENT

 

Invitation for Tender


Date: 03th December, 2018
1.       This Invitation for Tender follows the General Procurement Notice (GPN) which appeared on PPRA website online on 02nd October, 2018.

2.       Ministry of Education, Science & Technology has set aside fund towards the cost to improve quality of Education and it intends to apply part of the proceeds of this fund to cover eligible payments under the contract for the Supply of Office Equipment for School Quality Assurance Department.

3.       The Permanent Secretary, Ministry of Education, Science & Technology now invites sealed tenders from eligible suppliers as tabulated below:-
  
Lot
Description of Items
Unit
Qty
Delivery Period (after contract signing)
1
Desktop Computer
Set
153
within 12 weeks
2
Printer
EA
153
within 12 weeks
3
UPS
EA
153
within 12 weeks

       Tenderers are required to quote for one lot, two lots or all lots but in any case Tenderers are required to quote for all items and quantities specified in each lot.  Tenderers who do not quote for all items and quantities will be considered non responsive and rejected in evaluation.

  1. Tendering will be conducted through the National Competitive Tendering (NCT) procedures specified in the Public Procurement Regulations, 2013 – Government Notice No. 446 and are open to all Tenderers as defined in the Regulations.
5.       Interested eligible Tenders may obtain further information from and inspect the Tendering Documents at the office of the Secretary of Tender Board, Ministry of Education, Science & Technology, College of Business Studies and Law, University of Dodoma, (UDOM), Block 10, P.O Box 10 - 40479 Dodoma, Office number 320 from 0900 to 1500 hours on Mondays to Fridays inclusive except on public holidays.

6.       A complete set of Tendering Document (s) in English and additional sets may be   purchased by interested Tenderers on the submission of a written application to the address given under paragraph 5 above and upon payment of a non-refundable fee of Tzs. 100,000/= (Tanzania Shillings: One Hundred Thousand Only), Payment should be done through Government e- Payment Gateway (Gepg) where the tender should get control number at office room No.327, at Ministry of Education, Science and Technology.

7.       All Tenders for Lots 1, 2 & 3 must be accompanied by a Tender Security in an acceptable form in the amount of TZS. 5,000,000.00 (Tanzanian shillings Five million) for each lot.

  1. All tenders in one original plus two copies properly filled in, and enclosed in plain envelopes must be delivered to the Secretary of Tender Board, Ministry of Education, Science & Technology, College of Business Studies and Law, University of Dodoma, (UDOM), Block 10, P.O Box 10 – 40479 Dodoma, Room 320 at or before 10.00 local hours on 18th December,2018. Tenders will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to attend in the opening at the Conference Room, Ground Floor, Ministry of Education, Science & Technology, College of Business Studies and Law, University of Dodoma, (UDOM), Block 10, P.O Box 10 – 40479 Dodoma.

9.       Late Tenders, Portion of Tenders, Electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened and not read out in public at the tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.



PERMANENT SECRETARY,
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE & TECHNOLOGY
University of Dodoma (UDOM), Block No. 10, P.O. Box 10 40479 DODOMA.