Alhamisi, 21 Desemba 2017
Wizara ya Elimu yaendeleza ujenzi wa Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine
Wizari
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.7 kwa ajili
ya kuendeleza ujenzi wa shule ya
sekondari ya kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine inayonengwa Wilayani
Mvomero mkoani Morogoro.
Akizungumza
leo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo
katika mkoa wa Morogoro Waziri Ndalichako amepongeza juhudi zinazofanywa na
Halmashauri ya Mvomero kwa kuhakikisha inasimamia fedha zinazotolewa na
Serikali kuwa zinatumika kama zilivyokusudiwa.
"Nawapongeza
kwa kazi nzuri, ni jambo jema la kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuhakikisha
tumekamilisha ujenzi huo ili wanafunzi waweze kuanza masomo kama
inavyotarajiwa, huu ni mfano basi ni vyema na halmashauri nyingine ziige hiki ambacho
Mvomero imefanya"alisema Waziri Ndalichako.
Profesa
Ndalichako amesema uwepo wa shule hiyo ni kumbukumbu na pia ni kielelezo kuwa
Hayati Sokoine amelitumikia Taifa hili kwa Uadilifu.
Katika
ziara hiyo Waziri ametembelea kituo cha Maendeleo DAKAWA kwa lengo la kujionea
hali ya Miundombinu katika shule ya Sekondari Dakawa, Kituo cha Ufundi Stadi
VETA na Chuo cha Ualimu.
Pia ametembelea Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichopo Kihonda na kile kilichopo
Morogoro mjini ambapo ameiagiza BODI ya
VETA kuangalia upya sifa za wakuu wa vyuo waliopo hivi sasa ili kuleta
tija na ufanisi katika kazi kwani
waliopo hivi sasa hawakidhi vigezo pia hawaendani na kasi ya serikali ya
awamu ya Tano.
Jumatatu, 18 Desemba 2017
Waziri Ndalichako aongoza Harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni shule ya Sekondari Sovi
Zaidi
ya shilingi milioni Mia moja zimepatikana wakati wa Harambee ya Ujenzi wa
mabweni ya wasichana katika shule ya
sekondari Sovi iliyopo kata ya Mtwango
Mkoani Njombe.
fedha
hizo zimepatikana wakati wa harambee
iliyoongozwa na Waziri wa Elimu, Sayasni na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako mwishoni mwa wiki mkoani Njombe ambapo amewataka vijana kuwa wazalendo, pamoja na kuhakikisha
wanasoma kwa bidii kwa maslahi ya Taifa.
Waziri
Ndalichako pia amewasihi vijana
kuhakikisha wanaipenda nchi yao pamoja na kujiepusha na makundi ambayo hayana
tija kama vile utumiaji wa dawa za kulevya, kujiingiza kwenye makundi ya
uhalifu, na utumiaji wa pombe vitendo ambavyo havina faida kwa maisha yao ya
sasa na ya baadae.
Waziri
Ndalichako amesema kuwepo kwa mabweni kutawapunguzia wanafunzi kutembea umbali
mrefu, kuwaepusha na vishawishi vya barabarani wakati wa kwenda na kurudi
shuleni na hivyo watatumia muda wao
mwingi kwenye kusoma.
Ndalichako
amesema kazi ya Serikali ni kuboresha miundombinu, na kuhakikisha mahitaji
muhimu ya wanafunzi yanapatikana shuleni hivyo wanafunzi nao lazima watimize
wajibu wao kwa kuhakikisha wanasoma na kufaulu katika mitihani yao.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema mkoa wake
unatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kutatua
changamoto mbalimbali katika sekta ya Elimu.
Amesema
katika mkoa wake kati ya Shule Kumi za sekondari za umma shule Tisa zina
mabweni lengo likiwa ni kuondoa changamoto ya upatikanaji wa mimba kwa wanafunzi,
pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha Nne.
Ijumaa, 15 Desemba 2017
Ole Nasha aitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuandaa Wataalamu katika fani za ufundishaji na ujifunzaji
Naibu
Waziri ametoa agizo hilo katika mahafali ya 53 ya Taasisi ya Elimu ya Watu
Wazima yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam,
ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa
stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesaba
(KKK) kwa vijana na watu wazima.
Naibu
Waziri Ole Nasha amesema Wizara tayari ilishatoa Mwongozo wa shule za Msingi na
Sekondari kutumika kama vituo vya
kutolea Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi, wakati utaratibu wa
kuvitumia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi FDC ukiwa unaendelea.
Mheshimiwa
Ole Nasha amesema serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutekeleza
Mipango mbalimbali ambayo inawawezesha vijana na watu wazima waliokosa fursa
katika Mfumo Rasmi wa Elimu kujiendeleza kielimu na kumudu changamoto za
maisha.
Naibu
Waziri Ole Nasha amewataka wahitimu kwenda kufanya kazi kwa weledi katika vituo
watakavyopangiwa ili kusaidia juhudi za Serikali za kupambana na adui ujinga.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Taasisi i
naendelea kuongeza fursa zaidi katika utoaji Elimu kwa kupitia programu za
mafunzo kwa kutumia njia ya ujifunzaji huria na masafa kwa ngazi ya Stashahada.
Dtk.
Mafumiko amasema hadi sasa Taasisi imeongeza vituo vya mafunzo vya Elimu ya Watu Wazima kutoka vituo 13 hadi kufikia 21 katika
mikoa13.
Alhamisi, 14 Desemba 2017
Rais Magufuli asema Serikali iko tayari kulipa madai halali ya Walimu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali iko
tayari kulipa madai ya walimu ambayo
wanaidai serikali endapo madeni hayo yatakuwa yamehakikiwa na kuthibitishwa
kuwa ni madai halali.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Walimu ambao unafanyika katika ukumbi
wa Chimwaga mkoani Dodoma Rais amesema anatambua sana shida za walimu na kuwa serikali yake iko tayari kupatia
ufumbuzi changamoto hizo.
Rais
Magufuli amesema mpaka sasa tayari Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni
56 kulipa madeni ya walimu na kuwa kila
mwezi serikali imekuwa ikituma ruzuku kiasi
cha shilingi bilioni 18 mpaka bilioni 23 kwa ajili ya kuwalipa walimu.
Rais
Magufuli amewataka walimu na wanafunzi
kukubali kufanya kazi katika vituo wanavyopangiwa mara wanapohitimu, Pia
amesisitizia suala la mwalimu kutokuhamishwa kituo cha kazi bila kulipwa fedha
yake yote na hivyo amewataka walimu kuzingatia suala hilo.
Akizungumza
kabla ya Kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Ndalichako amewapongeza walimu kwa umoja na mshikamano ambao wamekuwa
wakiuonyesha kupitia chama hicho cha walimu.
Chama
hicho cha walimu kupitia Risala yao imeeleza kuwa inatambua jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kutatua changamoto mbalimbali
zilizopo katika sekta ya Elimu.
Katika
mkutano Rais Magufuli aliwaongoza viongozi wengine kuchangisha fedha kiasi cha shilingi milioni 60 ambazo
zitagawanywa kwa walimu zaidi ya 1000 ambao wanashiriki mkutano huo.
Alhamisi, 7 Desemba 2017
Finland yaahidi kuendelea kusaidia Sekta ya Elimu
Jamhuri
ya Watu wa Finland imesema itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya Elimu
kwenye eneo la ubunifu ili kuhakikisha vijana wanakuwa wabunifu ili kuweza
kujiajiri pindi wanapomaliza masomo.
Kauli
hiyo imetolewa na Balozi wa Jamhuri ya watu wa Finland nchini Tanzania Pekka
Hukka wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo
jijini Dar es Saalam kuhusiana na namna bora ya utekelezaji wa awamu ya pili ya
programme ya ubunifu inayotekelezwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH).
Waziri
Ndalichako amesema atahakikisha Wizara yake inasimamia kwa karibu utekelezaji
wa programu hiyo ili kuhakikisha malengo ya programu yanafikiwa.
Waziri
Ndalichako amesema Serikali inatambua msaada
ambao umekuwa ukitolewa na Finland katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Elimu na kuahidi kuwa fedha zitakazotolewa zitatumika kama
zilivyokusudiwa.
Programu
hiyo ya miaka mitano inatarajiwa kuanza
2018 na kukamilika 2022.
Jumanne, 5 Desemba 2017
Chuo cha Ufundi Arusha chatakiwa
kukamilisha ukarabati ili kuwezesha vifaa vilivyonunuliwa kutumika.
Naibu
waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amekitaka chuo cha
Ufundi cha Arusha kukamilisha ukarabati na upanuzi wa karakana zake ili
kuwezesha vifaa vya kisasa vilivyonunuliwa vianze kutumika.
Naibu
waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo
mkoani Arusha ili kujionea utendaji kazi, ambapo amesisitiza kuwa serikali ya
awamu ya tano imejielekeza katika kuboresha elimu ya ufundi ili kufikia malengo
ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Ole
Nasha amesema kutokana na umuhimu huo serikali nimeamua kuwekeza katika
uboreshaji wa vyuo vinavyotoa Elimu ya ufundi kwa kununua vifaa vya
kisasa na kukarabati miundombinu ya vyuo hivyo ili viweze kuzalisha raslimali
watu watakaowezesha nchi kujenga uchumi wa viwanda.
Naibu
waziri amesema chuo hicho kimepata vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya
kisasa vilivyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 14 kutoka nchini Australia
ikiwa ni sehemu ya jitihadi zinazofanywa na serikali ya kuboresha namna
ya utoaji wa elimu ya Ufundi kwa lengo kusaidia kuzalisha vijana wengi wenye taaluma
ya kisasa katika ufundi.
Ole
Nasha amevitaka vyuo vyote vya ufundi kutambua kuwa vina jukumu kubwa la
kuwatengeneza vijana watakaokuwa na weledi na umahiri katika kuchangamkia fursa
za kazi zitakazokuwa zikipatikana katika miradi mikubwa ya maendeleo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. Erick Mgaya amesema vifaa vya kisasa
vilivyonunuliwa vitawezesha kurahisisha zoezi zima la ujifundishaji na
ujifunzaji kutokana na kuongezeka kwa udahili.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)






