Balozi wa Canada Ian Myles
 akisisitiza jambo kwa Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako 
wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kumsalimia. Katika kikao
hicho Balozi wa Canada aliahidi serikali yake kuendelea kushirikiana na
serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu 
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa balozi wa
Canada Ian Myles aliyefika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo
mengine walizungumzia Mradi wa kuboresha Elimu ya Ualimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.
Joyce Ndalichako akizungumza na Balozi wa Canada Ian Myles pamoja na Susazn
Steffen Kansela Mkuu Ushirikiano na Maendeleo kutoka ubalozi wa Canada waliofika
ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia ushirlikiano kati ya serikali hizi mbili katika kuboresha elimu.
Wakurugenzi kutoka Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Gerald Mweli Kaimu Mkurugenzia wa Mipango na
Sera (Mwenye shati Jeupe), Aletaulwa Ngatara Mkurugenzi Msaidizi Sera wa kwanza
kulia na Mbarak Said  Afisa kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wakifiatilia kwa makini mjadiliano kati ya Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia na Balozi wa Canada.




 
 


