Jumanne, 6 Desemba 2016

Waziri wa Elimu hakutana na Ujumbe wa Benki ya Dunia



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na wajumbe kutoka Benki ya Dunia waliofika wizarani kuongea naye masuala mbalimbali ya Elimu na jinsi ya benki hiyo itakavyoendelea kusaidia sekta ya elimu nchini wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Sajitha Bashir, Cornelia Jesse na Gayle Martin kutoka Benki ya Dunia.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Elimu aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya elimu ambayo imekuwa chachu ya kuleta maboresho katika sekta ya elimu nchini. Hivyo amewaomba kuendelea kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika elimu ili kuhakikisha inaendelea kuboreshwa na kuwapa fursa watoto waengi wa Kitanzania kupata elimu iliyo bora.
Naye Mjumbe kutoka Benki ya Dunia Sajitha Bashir amemuhakikishia Waziri wa Elimu kuwa Benki ya Dunia itaendelea kufadhili miradi ya Elimu nchini pale itakapoitajika. Aidha, alisisitiza kuwa miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ni lazima itoe matokeo yanayokusudiwa

Waziri wa Elimu azindua mashindano ya Ujuzi


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.

Balozi wa Uingereza amtembelea waziri wa Elimu na kufanya mazungumzo



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na Balozi wa Uingereza Sarah Cooke nchini aliyefika ofisini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu Elimu nchi. Aidha, katika mazungumz0 hayo Waziri aliishukuru Uingereza kwa kusaidia na kufadhili miradi mbalimbali ya Elimu nchini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia baadhi ya taarifa kuhusu vitabu vya lugha ya Kiingereza vinavyoandaliwa na DFID  kwa ajili ya kusambazwa kwa shuleni. Vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi pamoja na walimu, pichani ni Balozi wa Uingereza Sarah Cooke na Mwakilishi wa DFID Tanya Zebioff


Alhamisi, 1 Desemba 2016

China yakabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


Serikali ya China imekabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuwezesha wizara kufanya kazi kwa weledi. vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Prf. Saimon Msanjila ofisini kwake na Liu Yun

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Liu Yun alimwelezea Naibu Katibu Mkuu kuwa wanajisikia faraja kubwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wizara kwani China na Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa karibu sana katika sekta ya elimu hasa katika upande wa elimu ya juu.

Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na Dell desk compture 6, mashine ya kudurufu moja, scanner moja, video camera moja na komputa mpatako 10 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano

Ushirikiana huo umewezesha serikali hizi mbili kuweza kubadilishana wanafunzi wa elimu ya juu katika fani mbali mbali. Pia alimuelezea uanzishwaji wa mafunzo ya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam ambapo alisema hii ni ishara tosha ya ushirikiano uliotukuka.

Naye Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Yun kwa msaada huo wa vitendea kazi ambapo alimuahidi kuwa vitafanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba inaongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi wanaofika ofisi hapo kupata huduma mbalimbali za kielimu.

Baadhi ya vtendea kazi vilivyotolewa na serikali ya China kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wa watumishi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi 


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakisoma na kujadiliana nyaraka mbalimbali za vifaa wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakiweka saini makubaliano ya kupokea vifaa vilivyotolewa na China wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi 

Ijumaa, 4 Novemba 2016

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yakabidhiwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Mkinga akimkabidhi  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish  baadhi ya nyaraka mbalimbali zinazohusu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ambavyo sasa vitakuwa vikiendeshwa na kusimamiwa  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Saimon Msanjila.


Katibu Mkuu Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akizungumza na watendaji wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  wakati wa  makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara.



Makatibu wakuu wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hizo  mara baada ya makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

Wizara yakabidhi ramani ya michoro ya shule ya sekondari Nyakato


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akiwa ameshika ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Bukoba Vijijini Mwantumu Dau na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani ambaye yeye pamoja na wadau wengine wamejitolea kusaidia kukarabati baadhi ya miundombinu ya shule hiyo.  Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko


Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Majengo Tanzania Elius Mwakibinga akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera, huku Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani akishuhudia. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko



  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akimkabidhi Mkurugenzi wa Bukoba Vijijini Mwantumu Dau ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko



Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko


Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Balozi wa Canada amtembelea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ofisini kwake


Balozi wa Canada Ian Myles  akisisitiza jambo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako  wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kumsalimia. Katika kikao hicho Balozi wa Canada aliahidi serikali yake kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa balozi wa Canada Ian Myles aliyefika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia Mradi wa kuboresha Elimu ya Ualimu.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Balozi wa Canada Ian Myles pamoja na Susazn Steffen Kansela Mkuu Ushirikiano na Maendeleo kutoka ubalozi wa Canada waliofika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia ushirlikiano kati ya serikali hizi mbili katika kuboresha elimu.


Wakurugenzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Gerald Mweli Kaimu Mkurugenzia wa Mipango na Sera (Mwenye shati Jeupe), Aletaulwa Ngatara Mkurugenzi Msaidizi Sera wa kwanza kulia na Mbarak Said  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifiatilia kwa makini mjadiliano kati ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Balozi wa Canada.