Ijumaa, 19 Julai 2019

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY




UNDERGRADUATE SCHOLARSHIPS TENABLE IN ROMANIA DURING ACADEMIC YEAR 2019-2020

Call for Applications
The General Public is hereby informed that, the Government of Romania has granted a Scholarship programme to eligible Tanzanian Nationals to pursue undergraduate studies at Universities in Romania. The Scholarship programme is scheduled to start during 2019/2020 academic year at the following Universities:-

1.    The National University of Political Studies and Public Administration  specializing in the fields of Political Science, Public Administration, Management, Communications and Public Relations, International Relations and European studies. http://snspa.ro/en/study-snspa/admission/non-eu-students/

2. The University of Medicine, Pharmacy, Science and Technology of Târgu Mureș https://www.umfst.ro/admission/admission-2019.html

3.    The University of Agronomic Sciences and Veterinary Medicine of Bucharest specializing in the fields of Agronomic Sciences, Veterinary Medicine, Biotechnologies, Land Reclamation, Horticulture https://www.usamv.ro/index.php/en/admission-2018

4.    Lucian Blaga” University of Sibiu specializing in the fields of  Letters, History and Law, Medicine, Food and Textile Processing Technology, Engineering and Sciences  https://admitere.ulbsibiu.ro/ro/oferta/non-eu-citizens/

5.  Transilvania University of Brasov specializing in the fields of Mechanical Engineering, Technological Engineering, Civil Engineering, Materials Science and Engineering, Electrical Engineering and Computer Science, Food and Tourism, Wood Processing, Forestry, Economics, Mathematics and Computer Science, Music, Medicine, Law, Sociology and Communication, Sports and Physical Education, Letters, Product Design and Environment, Psychology and Education Sciences. https://www.unitbv.ro/en/prospective-students/admission/admission-information-for-non-eu-citizens.html

6.  West University of Timisoara specializing in the fields of Chemistry , Biology and Geography, Economics and Business Administration, Mathematics and Computer Science, Music and Theatre, Political Sciences, Philosophy and Communication Sciences. https://ri.uvt.ro/cetateni-din-state-terte-uniunii-europene-2/?lang=en

7.   Aurel Vlaicu” University of Arad specializing in the fields of Design, Economic Sciences, Exact Sciences, Humanities and Social Sciences, Educational Sciences, Psychology and Social Sciences, Theology, Engineering, Food Engineering, Tourism and Environmental Protection, Physical Education and Sport. https://www.uav.ro/en/admission/how-to-apply/non-eu-citizens

      The application package should comprise of the following:
(i)      Application form for the issuance of the Acceptance Letter, filled in ALL the fields (attached);  https://drive.google.com/open?id=1AvowzhFaxvp82rqJlz03yp6_SXr3T6pb
(ii)            Proof of Nationality;
(iii)          Birth Certificate;
(iv)          A level ACSE Results Transcripts;
(v)            O level CSE Results Transcripts;
(vi)          Diploma Results certificates and Transcripts;
(vii)        Medical Examination Certificate from a  Government Hospital; and
(viii)     A copy of the marriage certificate (if the applicant’s name changed subsequent to the marriage).

Note: In case the above documents are not in English/French/Romanian you should submit a copy of legalized translation.

Application Procedure
Scanned application package should be sent directly to the respective Universities in Romania not later than 20th July 2019.

Jumatano, 10 Julai 2019

BILIONI 40 KUJENGA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KATIKA WILAYA 25


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Wilaya ya Urambo ambapo amesema serikali katika bajeti ya mwaka  huu imetenga jumla ya Shilingi bilioni 40  kwa ajili ya kujenga vyuo vipya  katika wilaya 25.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa chuo hicho ambapo amesema ongezeko la vyuo vya ufundi nchini linasaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu ya ufundi ambao wanahitajika katika viwanda mbalimbali  vinavyoanzishwa nchini.

"Kadri tunavyoongeza vyuo hivi vya ufundi katika wilaya mbalimbali tunasogeza elimu  ya ufundi itolewayo na vyuo vya VETA karibu na wananchi ili kuwawezesha kupata ujuzi na stadi zinazohitajika katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inalenga kujenga uchumi wa viwanda kuiwezesha kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, " amesema Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na viongozi  mbalimbali wa Serikali na  wananchi wa Mkoa wa Tabora (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)

Amesema dira iliyowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda imekuwa chachu kwa wizara kuongeza kasi ya huduma ya mafunzo ya ufundi stadi ambapo mpaka sasa inakamilisha vyuo vya VETA katika Wilaya za Nkasi, Ileje, Newala na Muleba ambavyo vipo katika hatua za ukamilishaji.  Vyuo vingine vilivyo katika hatua ya ujenzi ni vya halmashauri ya Kasulu, Itilima, Ngorongoro, Chato, na Babati ambavyo vinatarajiwa kukamilika kabla ya kumaliza mwaka huu 2019.










 
Waziri Ndalichako amezitaja wilaya nyingine ambazo zitajengewa vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Wilaya za Chunya, Kilindi, Korogwe, Ukerewe, Igunga, Pangani, Kishapu, Rufiji, Uyui, Kwimba, Bahi, Mafia, Longido, Mkinga, Uvinza, Ikungi, Iringa Vijijini, Lushoto, Mbarali, Monduli, Buhigwe, Ulanga, Masasi, Butiama na Chemba.

Aidha, Waziri Ndalichako amewashukuru Viongozi wa Mkoa wa Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Mbunge wa Jimbo la Urambo, Mhe. Margreth Sitta na wananchi wote wa Wilaya hiyo kwa utayari wao wa kuhakikisha upatikanaji wa majengo na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 45,000 kwa ajili ya Chuo cha VETA cha Urambo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Viongozi wengine wakifurahia jambo mara baada ya kuzindua Chuo cha VETA cha wilaya ya Urambo Mkoani Tabora aliyevaa koti ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora


Wakati huo huo Waziri Ndalichako ametumia nafasi hiyo kuagiza Uongozi wa VETA kukamilisha ujenzi unaoendelea wa vyuo vya VETA katika wilaya kwa wakati na ubora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry, akizungumza katika uzinduzi huo, amewataka vijana wa wilaya ya Urambo kujiunga na chuo hicho ili kupata ujuzi na stadi zitakazowawezesha kufanya kazi katika miradi ya ujenzi ya kimkakati ya mkoa huo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Mbunge wa Urambo Magreth Sit, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry pamoja na Viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzindua wa Chuo cha VETA cha wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu, akitoa Maelezo  ya mradi huo amesema umehusisha ukarabati wa majengo, ununuzi wa samani za ofisi, vifaa na vitendea kazi vya ofisi , zana za kufundishia na  samani za mabweni ya wanafunzi umegharimu zaidi ya shlingi milioni 200.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akikagua baadhi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia vilivyonunuliwa kwa ajili ya Chuo cha VETA cha wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.


SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAANDIKA HISTORIA KWA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KWENYE SEKTA YA ELIMU


Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imeandika historia kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Elimu kwa lengo la kutimiza azma yake ya kupata nguvu kazi iliyo mahiri katika sekta mbalimbali za ufundi itakayofanya kazi katika viwanda ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025.

Hayo yameelezwa Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William ole Nasha alipofanya ziara katika Wilaya za Sengerema, Kwimba na Misungwi kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za Uthibiti ubora wa shule wilaya  na ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) unaoendelea katika wilaya hizo.

Ole Nasha alisema pamoja na mambo mengine mengi ambayo serikali imetekeleza katika Sekta ya Elimu katika mwaka wa fedha 2019/20 Serikali imetenga fedha kiasi cha sh bilioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vipya 25 vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) vya Wilaya lakini pia kuna vyuo 5 vya mkoa vinaendelea kujengwa ili kuwezesha vijana wa kitanzania kusomea elimu ya ufundi itakayowawezesha kujiajiri.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Karumo kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkaoni Mwanza. 

Pia alisema Serikali inajenga na kukarabati vyuo 55 vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) ili kuboresha miundombinu ya vyuo hivyo itakayotoa fursa kwa vijana wengi kujifunza na kupata elimu ya ufundi itakayowawezesha kufanya kazi za uzalishaji katika maeneo yao lakini pia watakuwa chachu ya maendeleo ambayo ndio Serikali inahitaji.



“Katika moja ya eneo ambalo Mhe. Rais Magufuli ameelekeza nguvu nyingi katika kipindi cha utawala wake ni kuboresha elimu na sababu ni rahisi  huwezi kusema unajenga nchi ili kufikia uchumi wa kati unaotegemea uchumi wa viwanda kama huna nguvu kazi iliyoelimika,”alisema Naibu Waziri Ole Nasha

Alisema kwa sasa ukitembea nchi nzima utaona ujenzi na ukarabati unaoendelea katika vyuo, shule za msingi na sekondari hii yote ni mkakati wa Serikali wa kuboresha elimu katika gazi zote za za elimu nchini.

“Mwaka uliopita pekee wizara ya Elimu, Saynsi na Teknolojia kupitia Programu ya EP4R imekarabati na kujenga miundombinu mipya kwenye shule zaidi ya 500 ambapo zaidi ya sh bilioni 90 zimetumika na hapa nazungumzia kile kinachotekelezwa na Wizara ya Elimu pekee na sio TAMISEMI. Hii inaakisi uwekezaji mkubwa ambao umefanyika kwenye sekta ya elimu,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua miundombinu ya vyoo katika moja ya bweni la wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Karumo Jijini Mwanza.


Alisema haya yote yanatokana na ukweli kwamba elimu ndio msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika nchi yetu na ndio maana serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu.

“Utaona uwekezaji huu haufanyiki tu kwenye kujenga tunaweka vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Katika vyuo ambavyo vinashughulika na ufundi wa Kati Serikali imeendelea kupeleka vifaa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha

Pia alisema kwa miaka mitatu  mfululizo Serikali imeajiri takribani walimu wapya  elfu 18, na kwamba katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuajiri walimu wengine wapya lengo ni kuwa na uwiano mzuri kati ya mwalimu na mwanafunzi.

Alitaja eneo lingine ambalo fedha nyingi za umma zinaelekezwa ni ugharamiaji wa Elimu bila malipo ambapo kila mwezi Serikali hutoa zaidi ya bilioni 20 kugharamikia elimu kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne. Alisema lengo ni kumwezesha mtoto wa kitanzani mwenye umri wa kuanza shule aweze kusoma bila kisingizio cha kukosa ada.
Muonekano wa sasa wa moja ya Jengo la Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Karumo lililojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa ESPJ. Chuo hicho kipo Kata ya Karumo Wilaya ya Sengerema Jijini Mwanza

Naibu Waziri Ole Nasha alisema kwa upande wa Elimu ya Juu Serikali imepanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambapo katika mwaka huu inategemea wanafunzi wapya elfu 45 huku fedha za mikopo zikiongezeka kutoka shilingi bilioni 427 za mwaka jana hadi kufikia 450 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha amezitaka Halmashauri za Kwimba, Sengerema na Misungwi kusimamia vizuri fedha zinazokuja katika maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na matokeo yaakisi thamani ya fedha zilizotolewa

 “Mhe. Rais katika jambo ambalo anasisitiza kila siku ni matumizi sahihi ya fedha za miradi ukiona fedha zinakuja fahamu ni kwa sababu serikali imetumia nguvu kubwa katika kukusanya kodi na kuzitafuta fedha hizo zisimamieni vizuri’’alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Senyi Nganga na yule wa Sengerema Emmanuel Kipoyo wameahidi kuendelea kusimamia ipasavyo fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa katika Wilaya zao ili ziweze kutimiza lengo na matokeo yaakisi gharama ya fedha zilizotolewa ikiwa ni pamoja na kusimamia elimu ipasavyo katika Wilaya hizo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua majengo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Jijini Mwanza ambacho kimepatiwa fedha na Wizara kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.

Jumapili, 7 Julai 2019

UJENZI WA OFISI ZA UTHIBITI UBORA WA SHULE WAANZA KWA KASI WILAYANI MISUNGWI


·        Naibu Waziri Ole Nasha afanya ziara kukagua asisitiza viwango katika utekelezaji wa mradi huo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule wa wilaya hiyo inayojengwa katika kata ya Igokelo kijiji cha Mapilinga mkoani humo.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa pongezi hizo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo ambapo amesema ameridhishwa na hatua ambayo ujenzi umefikia huku mkazo ukiwa kuzingatia ubora wa ujenzi wa jengo hilo.

“Kwa kweli mnakwenda vizuri, kama fedha mmepokea mwezi Mei mwaka huu tokea ujenzi uanze michakato yote ni kama mmetumia mwezi mmoja na tayari mmeshapaua ni jambo jema. Lakini niwapongeze zaidi kwa kuwa ujenzi huu miundombinu yake imezingatia watu wenye mahitaji maalum zingatieni ubora wa jengo katika kukamilisha kazi hii,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu Waziri wa Elimu, Saysnia na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Uthibiti ubora wa shule Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza.
Alisema ujenzi wa Ofisi za Uthibiti ubora wa shule ni mwendelezo wa nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuamua kuimarisha Idara ya Uthibiti Ubora wa shule ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa lengo la kuinua ubora wa elimu nchini.

Ole Nasha ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Elimu kwa kuwa zina lengo la kuimarisha elimu ya watoto wetu lakini pia kutumia fursa zinazokuja na miradi hiyo kujiingizia kipato kwani kwa sasa Serikali imeamua kutumia utaratibu wa Force Akaunti katika utekelezaji wa miradi yake kwani utaratibu huo umeonesha kuwa na mafanikio lakini pia unawanufaisha wananchi walio karibu na mradi unapotekelezwa.

“Wanamisungwi 34 wamefaidika na ujio wa mradi wa ujenzi wa ofisi hii ya Uthibiti ubora wa shule wapo waliopata nafasi ya kufanya kazi za ujenzi na wale wanaofanya bishara ya chakula na vinywaji na hili ndilo lengo la Serikali,’aliongeza Naibu Waziri ole Nasha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo ya namna mradi wa ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule wilaya ya Misungwi unavyotekelezwa kutoka kwa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Wilaya ya Misungwi Faustin Salala.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Ofisi hiyo Mthibiti Mkuu wa ubora wa Shule Wilaya ya Misungwi Faustini Salala alisema ujenzi wa ofisi hizo umeanza mwishoni mwa mwezi Mei 2019 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti, 2019 na utatumia zaidi ya shilingi milioni 150.

Mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Uthibiti Ubora wa shule katika wilaya ya Misungwi ni moja  ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ofisi 100 za aina hiyo zinazojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchi nzima ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watendaji wa Idara hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na baadhi ya Walimu pamoja na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za Uthibiti ubora Wilaya ya Misungwi. Amewataka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu kwani inalenga kuboresha elimu ya watoto wetu.

Jumamosi, 6 Julai 2019

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM.


Serikali imesema inatambua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum na ndio maana inachukua juhudi za makusudi kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili yawe rafiki kwao kupata elimu.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walio katika Kambi ya Joto (Summer Camp) inayoratibiwa na Taasisi ya Under the Same Sun.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walio kwenye ‘summer camp’ katika Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza. Ametumia fursa hiyo kuelezea juhudi ambazo Serikali imekuwa ikizifanya katika kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu.

Naibu Waziri Ole Nasha alisema katika kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa sasa Wizara anayoiongoza inatekeleza Programu ya Elimu Jumuishi ambayo inamuweka shuleni mtoto mwenye ulemavu na yule asie na ulemavu kwa lengo la kuondoa fikra za kunyanyapaliwa lakini pia kujenga umoja upendo na urafiki baina yao utakaowawezesha kulindana kwani siku zote mlinzi mzuri ni rafiki na ndugu hivyo inasaidia kuondoa changamoto zilizopo.

Aidha, Serikali pia inatoa mikopo kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma elimu ya juu kwa lengo la kuwasadia waweze kupata elimu zaidi kwani watu wenye ulemavu wakipata elimu wanaweza sio tu kujikomboa wenyewe lakini kuwasaidia watu wengine wenye changamoto hizo.

“Ninyi wenyewe mtakuwa mashahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Serikali yake kuna viongozi ambao wana ulemavu lakini kutokana na umahiri na uwezo walio nao katika utendaji wameteuliwa katika nafasi hizo. Tambueni kuwa watu wote wana haki sawa na hilo liko wazi,” alisema Naibu Waziri ole Nasha.

Kiongozi huyo amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa wao ni watoto wa kitanzania hivyo wanatakiwa kuwa huru kwenye nchi yao na kwamba Serikali itaendelea kuwalinda  ili waweze kuishi lakini pia kusoma kama watu wengine bila kudhuriwa na kitu chochote.

”wote ni mashahidi kwamba kwa  sasa Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kwamba mnakuwa na usalama wa maisha yenu, sidhani kama kuna kosa ambalo sasa ukipatikana nalo unachukuliwa hatua kubwa zaidi kama kujaribu kuwadhuru watu wenye ualbino, na ndio maana sasa mnapata ulinzi kaeni mkiwa huru kwa kuwa serikali inawajali,”aliongeza Naibu  Waziri Ole Nasha.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha amelitaka Shirika la Under The Same Sun   kutambua kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa wanaoutoa katika kuwasaidia  wanafunzi na watoto  wenye mahitaji maalum hasa watoto ambao wana changamoto ya ulemavu wa ngozi na kuwataka kuhakikisha mafunzo wanayoyatoa katika kambi za joto (summer camp) kila wanapokutana  pamoja na mambo mengine yalenge katika kuwaonesha watoto hao kuwa jamii inawajali na sio vinginevyo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha wakati alipokutana nao kuzungumzia juhudi ambazo Serikali imekuwa ikizifanya kutatua changamoto za watoto wenye ulemavu katika kupata elimu.

Nae Afisa kutoka Idara ya Elimu ya Shirika la Under the Same Sun Omary Mfaume amesema Shirika hilo linafadhili wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi kupitia programu za elimu zinazojihusisha na ufadhili wa elimu na ile ya uhamasishaji jamii ambayo inayowafundisha kwanini mtu anazaliwa na ualbino, changamoto zake na namna ya kuzikabili changamoto hizo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Clara Maliwa ameiomba Wizara kuwa na utaratibu wa kuwatambua Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wanaofanya vizuri katika masomo ili kutoa changamoto kwa wengine ili waweze kufanya vizuri zaidi.

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ATAKA CHUO CHA UALIMU BUTIMBA KUREJESHA MASOMO YA SANAA


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amekitaka Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kufanya tafakari ya namna gani kinakuwa chachu ya mabadiliko katika kuandaa walimu wanaoendana na mahitaji ya sasa.

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Mwanza wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 80 ya kuanzishwa Chuo hicho ambapo amesema mijadala itakayoendeshwa ijikite zaidi katika kujua ni namna gani wanabadili mfumo wa kufundisha ili wanafunzi waweze kuwa wabunifu na wanaojiamini.

“Nimeona katika maonesho yenu mna jaribu kufanya masuala ya ubunifu, ubunifu unaanza mwanafunzi akiwa mdogo na ndio maana tunasema lazima kufanya ufundishaji ambao toka mwanzo unampa mwanafunzi nafasi ya kuwa mbunifu. Usimbane mwanafunzi jaribu kumfungulia fursa mbalimbali kwani anapozaliwa anakulia katika mazingira mbalimbali ya ubunifu hapo utatoa nafasi ya kuweza kuendeleza ubunifu alio nao,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha akizungumza katika Kumbukizi ya Miaka 80 ya Chuo cha Ualimu Butimba iliyofanyika katika  chuoni hicho  Jijini Mwanza.

 Alisema Chuo cha Butimba pamoja na kwamba ni chuo cha ualimu historia yake hasa iko katika ualimu ule wa Sanaa za maonesho, Sanaa za ufundi ni vizuri kuangalia ni namna gani Chuo hicho kinarudi katika msatri na kuendelea kutoa walimu ambao watasaidia katika kufundisha masomo hayo.

“Kwa bahati mbaya kuna mahali tulikosea kufikiri kwamba music, ufundi, Sanaa za maonesho hazina nafasi katika elimu, sio vibaya tukarekebisha sababu kama unataka kumfundisha mwanafunzi ubunifu huwezi kukwepa kutumia Sanaa za maonesho, music na tamaduni zake zote kwani zinamsaidia kuwa mwanafunzi kamilifu anaeweza kubuni,” aliongeza Naibua Waziri Ole Nasha.
Washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa kuadhimisha kumbukizi ya miaka 80 ya Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo Wilaya ya Nayamagana  Jijini Mwanza

Akizungumzia Jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia Ole Nasha amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka historia ya kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya elimu kwa kujenga, kukarabati na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwenye shule.

Aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine Serikali kuanzia mwaka 2016 inatekeleza Mpango wa Elimu bila malipo, mpango ambao haujawahi kuwepo ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu ambapo inatumia zaidi ya shilingi bil. 20 kila mwezi kugharamia elimu bila malipo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo  kutoka kwa wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Butimba ya  namna wanavyotumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira wanayoishi kufundishia.

Nae Mkuu wa Chuo cha Ualimu Butimba Huruma Mageni amesema katika kuadhimisha miaka 80 ya Chuo hicho kinajivunia mambo mengi ikiwemo eneo la chuo kupimwa na kwamba rasimu ya hati ya chuo iko tayari. Pia inajivunia kuwa na vitengo ambavyo vinachangia kuboresha elimu nchini.