Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Wiliam Ole Nasha, amesema Serikali haitasita
kuvunja Mkataba na Kampuni ya Skywards Construction inayopaswa kujenga miundombinu
ya ufundishaji na ujifunzaji katika Chuo cha Ualimu Ndala kilichopo Halmashauri
ya Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
Naibu
Waziri ametoa Kauli hiyo baada ya Kampuni ya Skyward Construction iliyopaswa kujenga Mabweni, Vyumba vya Madarasa,
Ukumbi, Maktaba, Maabara na Matundu ya vyoo kutoonekana katika eneo la ujenzi
tangu alipokabidhiwa kutekeleza mradi huo mapema mwezi Januari 27, 2018.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Jacob Mtalitinya juu ya changamato zinazoikabili
Shule ya Sekondari Kampala katika kukamilisha ujenzi wa Miundombinu ya
ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza
akiwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa na Wizara
yake kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matoke- EP4R, Naibu Waziri Ole Nasha amesema Kampuni hiyo tangu
ikabidhiwe Mradi haijawahi kufika eneo la mradi kuanza ujenzi na bila taarifa
yoyote hivyo kuacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
‘Kampuni
hii ilipaswa kuanza kazi Februari 24, 2018 cha kushangaza hadi sasa haijaonekana
eneo la Mradi bila taarifa yoyote. Kampuni hii ya Skyward Constuction inapaswa
kujua imeingia mkataba na mikataba hii huwa ina taratibu zake, kama kuna jambo
haliendi sawa ni bora akaeleza kwa kuwa Serikali haitasita kuvunja mkataba
nae.’ Alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.
Naibu
Waziri Ole Nasha amezitaka Kampuni mbalimbali za ujenzi kuhakikisha zinazingatia Mikataba, kwani
kuchelewa kukabidhi Mradi kwa wakati kunaisababishia
Serikali gharama zisizo za lazima kwa kuwa vifaa vya ujenzi vitapanda bei
lakini pia Mradi kushindwa kukidhi kusudio la kuwepo kwa wakati huo.
Nae
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ndala Abinego Ndikumwe amesema pamoja na Serikali
kukarabati na kujenga miundombinu ya ujifunzaji na ufundishaji bado Chuo hicho
kina changamoto za upatikanaji wa Maji, ukosefu wa usafiri kwa matumizi ya Chuo, Bwalo na ofisi
za Wafanyakazi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akikagua ujenzi
wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari
Mwanzoli, iliyojengwa na Wizara hiyo kupitia Progamu ya Lipa kulingana na
Matokeo, EP4R ambapo mara baada ya ukaguzi huo Naibu Waziri amekiri kuridhishwa
na ukarabati huo na kuzitaka shule nyingine kuuga mfano huo.
Akiwa
Wilayani Nzega Mhe. Ole Nasha ametemtembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Nzega na Mwanhala, Shule ya Sekondari Kampala na Shule ya Sekondari Mwanhala ambapo
akiwa kwenye Shule ya Sekondari Mwanzoli na amekiri kurdhishwa na namna Shule
hiyo ilivyotekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya shule, ambapo ameahidi Wizara
yake itahakikisha inakamilisha ujenzi wa Maabara, na Nyumba mbili za Walimu.