. ·
ASISITIZA UWAJIBIKAJI MAHALI PA KAZI
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo
kufanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu
ikiwa ni pamoja na kuwa na ushirikiano miongoni mwao ili kufikia malengo
yaliyowekwa na Serikali.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza na wajumbe wa Mkutano
wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mkutano huo wa siku mbili umehitimishwa leo Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri huyo ametoa
kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa 25 wa baraza la wafanyakazi ambapo
amesisitiza kuwa mkutano huo upo kisheria na kuwa unasaidia kuainisha haki za
Wafanyakazi pamoja na Wajibu wao katika utumishi wa Umma.
Viongozi
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakiwa wameshikana mikono kuonesha
umoja wao wakati wa kufunga Mkutano wa
25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mkoani Morogoro.
Mheshimiwa Ole Nasha
amewataka Wafanyakazi hao kuhakikisha Elimu inayotolewa hapa nchini inakuwa
bora kwa kuwa Elimu ndiyo msingi pekee wa kufikia Uchumi wa viwanda.
Wajumbe
wa Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia wakati wa kufunga Mkutano wa baraza la Wafanyakazi mkoani
Mkoani Morogoro.
Pia amewataka makatibu wakuu
wa Wizara hiyo kushughulikia kikamilifu maazimio yote yalifikiwa katika mkutano
huo wa siku mbili wa baraza la Wafanyakazi kabla ya kufanyika kwa mkutano
mwingine wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyika mapema Oktoba mwaka huu.
Kauli mbiu ya mkutano wa
baraza hilo inasema: “Elimu Jumuishi, Sayansi na Teknolojia ni msingi wa
Maendeleo, Endelevu ya Uchumi wa viwanda Tanzania.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza
na wajumbe wa mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia (hawapo pichani), wakati wa kufunga mkutano huo
uliofanyika Mkoani Morogoro amabye amesisitiza kuwa jukumu la Wizara hiyo ni
kuweka viwango vya ubora vya Elimu.