Jumanne, 25 Februari 2020
Alhamisi, 20 Februari 2020
Jumamosi, 15 Februari 2020
Ijumaa, 14 Februari 2020
WAZIRI NDALICHAKO ATAKA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI YA ELIMU
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa rai kwa watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kusimamia vizuri fedha za miradi ya Elimu inayotelekezwa katika maeneo yao ili ikamilike kwa wakati na ubora.
Waziri Ndalichako ametoa rai hiyo Jijini Dar es Salaam wakati akizinduzia Jengo la Utawala la Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) lililokarabatiwa na kuongeza ukubwa ambapo amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi za Miradi lakini haikamiliki kutokana na usimamizi mbovu hivyo kutaka watendaji hao kusimamia miradi ipasavyo.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya kazi kubwa sana katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu na kwamba kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa Jengo la Utawala la Chuo Kishiriki cha DUCE ni sehemu tu ya mambo mengi ambayo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na serikali yake imefanya.
“Vyuo Vikuu vimekuwa vikijikita katika utoaji wa taaluma wakati mwingine vinakuwa vikisahau jukumu la kufanya tafiti na ndio maana tunaona idadi ya machapisho imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka. Niwaambie tunapokuwa tunafanyiwa tathmini ya upangaji wa madaraja ya vyuo, sehemu ambayo mara nyingi imekuwa ikituangusha ni sehemu ya tafiti, kwa hiyo nitumie nafasi hii kuzikumbusha Taasisi za elimu ya juu kuendelea kufanya tafiti na tafiti zenyewe ziwe ni zile zinazotoa mchango moja kwa moja katika maendeleo ya nchi,” amesema Ndalichako.
“Nakipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuweza kutumia fedha kutoka kwenye mapato ya ndani kutoa ufadhili wa masomo kwa watanzania wenye ufaulu wa kiwango cha Juu. Huu ni mchango mkubwa kwa Taifa letu kwani unatoa fursa kwa watanzania ambao wamefaulu vizuri lakini kutokana na sababu mbalimbali wasingeweza kunufaika na mikopo itolewayo na Bodi ya Mikopo,” alisema Waziri Ndalichako.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Dar es Salaam ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya DUCE Profesa William Anangisye amemuahidi Waziri Ndalichako kuendelea kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Miradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha jengo lililozinduliwa leo linatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwa chachu ya maendeleo ya Chuo hicho.
“Mhe. Waziri nakuahidi kuwa majengo haya yatatunzwa vizuri na kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya chuo,” amesema Prof. Anangisye.
Naye Kaimu Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Maluka ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa Taasisi za elimu ya Juu ambapo amesema katika Chuo hicho upanuzi wa Jengo la utawala umeondoa changamoto iliyokuwepo ya ukosefu wa ofisi za watumishi huku akiiomba Serikali kuwapatia fedha kwa ajili ya kusomesha wataalamu wao.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam |
“Vyuo Vikuu vimekuwa vikijikita katika utoaji wa taaluma wakati mwingine vinakuwa vikisahau jukumu la kufanya tafiti na ndio maana tunaona idadi ya machapisho imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka. Niwaambie tunapokuwa tunafanyiwa tathmini ya upangaji wa madaraja ya vyuo, sehemu ambayo mara nyingi imekuwa ikituangusha ni sehemu ya tafiti, kwa hiyo nitumie nafasi hii kuzikumbusha Taasisi za elimu ya juu kuendelea kufanya tafiti na tafiti zenyewe ziwe ni zile zinazotoa mchango moja kwa moja katika maendeleo ya nchi,” amesema Ndalichako.
“Nakipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuweza kutumia fedha kutoka kwenye mapato ya ndani kutoa ufadhili wa masomo kwa watanzania wenye ufaulu wa kiwango cha Juu. Huu ni mchango mkubwa kwa Taifa letu kwani unatoa fursa kwa watanzania ambao wamefaulu vizuri lakini kutokana na sababu mbalimbali wasingeweza kunufaika na mikopo itolewayo na Bodi ya Mikopo,” alisema Waziri Ndalichako.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Dar es Salaam ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya DUCE Profesa William Anangisye amemuahidi Waziri Ndalichako kuendelea kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Miradi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha jengo lililozinduliwa leo linatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwa chachu ya maendeleo ya Chuo hicho.
“Mhe. Waziri nakuahidi kuwa majengo haya yatatunzwa vizuri na kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya chuo,” amesema Prof. Anangisye.
Naye Kaimu Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Maluka ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa Taasisi za elimu ya Juu ambapo amesema katika Chuo hicho upanuzi wa Jengo la utawala umeondoa changamoto iliyokuwepo ya ukosefu wa ofisi za watumishi huku akiiomba Serikali kuwapatia fedha kwa ajili ya kusomesha wataalamu wao.
Jumatano, 12 Februari 2020
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MAAFISA BAJETI WA WIZARA NA WA OFISI ZA UTHIBITI UBORA WA SHULE KANDA
Serikali imeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo watendaji wake ili kutimiza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuongeza nidhamu katika matumizi ya fedha na usimamizi fanisi wa mali za serikali.
Hayo yamesemwa Mkoani Morogoro na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maafisa Bajeti wa Wizara na wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule Kanda yenye lengo la kuboresha utendaji kazi hususani katika maandalizi ya Bajeti.
Kiongozi huyo amesema utoaji wa mafunzo haya utasaidia kutoa maarifa mapya na stadi zaidi katika utekelezaji wa majukumu ikiwa ni Pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi.
“Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa shule amenieleza kuwa kulikuwa na changamoto katika uaandaji wa bajeti kwa kuwa haikuwa na uhalisia, natambua mwenye kujua hali halisi kwenye ofisi ya uthibiti ubora ni yule ambaye yuko katika ofisi husika za kanda na wilaya na kwa kuwa wataalamu wa bajeti wameona kuna mapungufu ndiyo maana tumeitisha mafunzo haya ili katika kupanga bajeti iwe na uhalisia,”alisema Naibu Waziri Ole Nasha
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha amesema Serikali katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha Uthibiti Ubora wa Shule kwa kuwajengea uwezo wa kiutendaji Wathibiti Ubora na kuweka mazingira sahihi ya ufanyaji kazi.
Ametaja maboresho yaliyofanyika katika eneo hilo kuwa ni pamoja na ununuzi wa magari 45 ya wathibiti ubora wa Shule kwa wilaya ambazo hazikuwa na magari Pamoja na Kujenga Ofisi 100 za Wathibiti na kuziwekea samani na vitendea kazi. Aidha Serikali pia imenunua pikipiki 2,894 za Maafisa elimu Kata ili kuimarisha usimamizi wa shule, pamoja na kuwapatia mafunzo ya kiutendaji wathibiti Ubora wa shule 1,276.
Maboresho mengine ni Kuongeza idadi ya Maafisa Uthibiti Ubora wa shule 400 ngazi ya Wilaya na Kanda pamoja na kuanzisha ofisi mpya 5 za Uthibiti Ubora wa shule katika wilaya mpya za Songwe, Kigamboni, Ubungo, Chalinze na Ushetu ili kurahisisha utoaji huduma za uthibiti Ubora huku serikali ikijipanga kununua magari mengine mapya 65 kwa ajili ya idara hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule Mwl. Euphrasia Buchuma amesema mafunzo haya yanafanyika kutokana na changamoto ambazo zimekuwa zikibainika katika bajeti zinazoandaliwa ikiwa ni pamoja na kueleweshana taratibu za matumizi ya fedha kulingana na vifungu vilivyowekwa.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa bajeti wa Wizara na wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa shule za Kanda yameanza leo Februari 12, 2020 na yana jumla ya washiriki 70 kutoka Ofisi hizo na Wizara ya Elimu Makao makuu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Maafisa Bajeti wa Wizara nawa Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule Kanda mkoani Morogoro |
Kiongozi huyo amesema utoaji wa mafunzo haya utasaidia kutoa maarifa mapya na stadi zaidi katika utekelezaji wa majukumu ikiwa ni Pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Pendo Sianga akiwapitisha wajumbe kwenye utaratibu wa kuandaa bajeti wakati wa mafunzo ya bajeti mkoani Morogoro |
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha amesema Serikali katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha Uthibiti Ubora wa Shule kwa kuwajengea uwezo wa kiutendaji Wathibiti Ubora na kuweka mazingira sahihi ya ufanyaji kazi.
Ametaja maboresho yaliyofanyika katika eneo hilo kuwa ni pamoja na ununuzi wa magari 45 ya wathibiti ubora wa Shule kwa wilaya ambazo hazikuwa na magari Pamoja na Kujenga Ofisi 100 za Wathibiti na kuziwekea samani na vitendea kazi. Aidha Serikali pia imenunua pikipiki 2,894 za Maafisa elimu Kata ili kuimarisha usimamizi wa shule, pamoja na kuwapatia mafunzo ya kiutendaji wathibiti Ubora wa shule 1,276.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Bajeti Mkoani Morogoro wakifuatilia hotuba ya Ufunguzi ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha |
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule Mwl. Euphrasia Buchuma amesema mafunzo haya yanafanyika kutokana na changamoto ambazo zimekuwa zikibainika katika bajeti zinazoandaliwa ikiwa ni pamoja na kueleweshana taratibu za matumizi ya fedha kulingana na vifungu vilivyowekwa.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa bajeti wa Wizara na wa Ofisi za Uthibiti Ubora wa shule za Kanda yameanza leo Februari 12, 2020 na yana jumla ya washiriki 70 kutoka Ofisi hizo na Wizara ya Elimu Makao makuu.
WIZARA YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA NA VITABU KWA VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI 35 KWA AJILI YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekabidhi vifaa vya TEHAMA na vitabu kwa vyuo vya ualimu vya serikali 35 kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa Chuo cha Ualimu Patandi jijini Arusha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka wakuu wa vyuo hivyo kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa na vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
"Vifaa tunavyovikabidhi leo ni vya gharama kubwa sana wito wangu kwa wakuu wa vyuo wote kuhakikisha wanavitunza vifaa hivi ili viweze tumika kwa muda mrefu na kuwanufaisha hata wanachuo watakaojiunga kwa miaka mingine" amesisitiza Katibu Mkuu.
Amesema pamoja na kukabidhi vifaa hivyo na kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu lengo kubwa ni kuimarisha na kuboresha mafunzo yanayotolewa kwa walimu tarajali ili wanapomaliza mafunzo yao wawe na mbinu bora
za ufundishaji ambazo zitasaidia kuinua ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ave Maria Semakafu amesema utoaji wa vifaa hivyo ni juhudi za makusudi zinazofanywa na wizara katika kutekeleza azma ya kuboresha elimu nchini.
Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo kutoka Canada Gwen Waimsley amesema nchi yake itaendelea kusaidia katika kuhakikisha walimu tarajali wanapata mafunzo bora ambayo yataleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi na sekondari.
Gwen amesema nchi ya Canada inaamini kuwa walimu wanapoandaliwa katika mazingira mazuri ya kupatiwa mafunzo zoezi zima la utoaji elimu katika hatua zote linakuwa limefanikiwa.
Naye Mkuu wa Chuo cha Ualimu Patandi..... ameishukuru serikali kwa kufanya mabadiliko makubwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo vimekuwa na mabadiliko ya miundombinu na kupatiwa vifaa vingi vya kufundishia na kujifunzia
Mkuu wa chuo huyo amesema kama watendaji walioaminiwa katika kusimamia vyuo hivyo wana wajibu wa kusimamia vyuo hivyo na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa kwani mazingira yamekuwa rafiki kwa utendaji na ufundishaji.
Vifaa vilivyokabidhiwa katika vyuo hivyo ni pamoja na kompyuta mpakato 43, kompyuta za mezani 780, mashine za kudurufu 74 vitabu vya masomo ya kufundishia na vitabu vya kitaaluma 26,470 , projectors na vifaa vya kufundishia elimu maalumu.

Jumanne, 11 Februari 2020
Kongamano la Kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya Utalii na Ukarimu
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema taasisi za mafunzo na wadau wa sekta ya utalii wanahitajika kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamto zilizopo ikiwemo nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha katika tasnia hiyo.
Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Kongamano la Kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya Utalii na Ukarimu ambapo amesema ushindani katika soko ni mkubwa hivyo kunahitajika maandalizi mazuri ya rasilimali watu ili kuweza kushindana katika soko la dunia.
Amesema Utalii ni moja ya Sekta inayolipatia Taifa fedha za kigeni akitolea mfano mwaka jana 2019 nchi ilipata fedha za kigeni dola milioni 2.4 kutokana na utalii hivyo kukiwa na nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha nchi itaneemeka kupitia utalii.
“Hakika tunahitaji kuandaa vizuri rasilimali watu, nchi jirani zimepiga hatua kwenye kuvutia watalii sio kwamba wana vivutio vingi kuliko sisi ni kutokana na pamoja na mambo mengine kuwa na nguvu kazi yenye weledi ndio maana kama Taifa tunawekeza katika kutayarisha vijana ili kuwa na nguvu kazi yenye weledi katika sekta ya utalii," amesema Naibu Waziri Ole Nasha.
“Ninawiwa kusema kuwa kongamano hili limekuja kwa wakati muafaka sana na Wizara yangu itayachukua kwa uzito mapendekezo yote yaliyotolewa ukizingatia kuwa kuimarisha muunganiko kati ya wanatasnia na wanataaluma ni moja ya vipaumbele katika wizara yangu ili kuhakikisha tunazalisha wahitimu bora wanaokidhi mahitaji ya soko,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.
Naibu Waziri Ole Nasha amekipongeza chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuandaa mkutano wa kuwaunganisha wakufunzi na watoe huduma hiyo walio katika biashara ya Utalii kwani kwa pamoja wanaweza kutatua changamoto zilizopo.
Naye Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Mlozi amesema kwa kushirikiana na vyuo vingine vinavyotoa mafunzo ya utalii wataendelea kuimarisha mpango wa utoaji mafunzo kwa kufanya kazi karibu na watoa huduma ili kupata nguvu kazi yenye weledi na ujuzi.
"Soko la hotelia na utalii liwe tayari kupokea mfumo wa mafunzo pacha hali kadhalika kuwa tayari kutoa nafasi kwa ajili ya walimu kupata ujuzi kwani kwa kufanya hivyo nchi itakuwa ya kwanza kuongoza kwenye sekta ya utalii na ukarimu," amesema Salema.
Kongamano la kimataifa la kuunganisha sekta ya Utalii na Ukarimu katika nchi zinazoendelea limefanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam na limewakutanisha wadau na wanataaluma katika sekta ya Utalii na Ukarimu kutoka nchi zinazoendelea.
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA KUJENGA KUJENGA BWALO KATIKA SHULE YA MRISHO GAMBO ILIYOPO MKOANI ARUSHA
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Wizara itajenga bwalo la chakula ili kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kuwa na sehemu nzuri na salama ya kupatia chakula watakapokuwa wakiishi katika mabweni yatakayojengwa na wizara.
"Nimeambiwa wanafunzi wa shule hii wanatoka maeneo ya mbali, Wizara ilishaahidi kujenga mabweni mawili sasa tutajenga na bwalo," amesema Dkt. Akwilapo.
Aidha, Dkt. Akwilapo amesema serikali ina wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika
mazingira salama na yenye miundombinu salama.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema shule hiyo imejengwa baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa Olasite baada shule yao kuzidiwa na wingi wa wanafunzi.
"Baada ya kupokea maombi kutoka kwa wakazi wa hapa na kuona kweli kuna shida katika shule hii ya Olasite ndipo tukaanza kutafuta wadau mbalimbali ambao walijitokeza na kusaidia uanzishwaji wa ujenzi wa shule hiyo," amesema Gambo.
Mkuu wa shule hiyo, Fedelis Michael amesema mazingira ya wanafunzi kusoma mbali sana na shule ni changamoto kwao kwani njiani wanakutana na mambo mengi ambayo yanaweza kuwasababishia kushindwa kusoma vizuri.
Jumatatu, 10 Februari 2020
CANADA YATOA ZAIDI YA BILIONI 90 KWA AJILI YA KUBORESHA ELIMU YA UALIMU
Serikali ya Canada imetoa zaidi ya bilioni 90 kwa Tanzania zitakazotumika kuboresha elimu ya ualimu nchini.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia na kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Kuendeleza Elimu nchini (TESP) ambapo amesema mradi huo pia umewezesha kuinua kiwango cha ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari kwa kuzalisha rasilimali watu yenye ubora.
.
Kiongozi huyo amesema kuwa Ushirikiano wa Tanzania na Canada unalenga kuongeza uwezo wa vyuo vya ualimu kufundisha walimu waliobobea watakaofundisha vizuri katika shule mbalimbali.
“Tunatoa shukrani nyingi sana kwa serikali ya Canada na Kitengo chao cha Global Affairs ambacho kinasimamia mradi huu, mafanikio makubwa yamepatikana kupitia mradi huu na matokeo yameshaanza kuonekana," amesisitiza Katibu Mkuu Akwilapo.
Dkt. Akwilapo amesema mafanikio ya mradi huo yameanza kuonekana ambapo walimu wameongeza uwezo katika ufundishaji na matumizi ya TEHAMA katika kufundisha.
Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo kutoka Canada Gwen Walmsley amesema kuwa Canada itaendelea kutoa fedha zaidi katika kuboresha sekta ya elimu nchini na mradi huo ni moja kati ya juhudi wanazozifanya katika kuunga mkono serikali ya Tanzania katika jitihada za kuboresha elimu.
Gwen ameipongeza Tanzania kwa kufanya Sekta ya Elimu kipaumbele ili kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, suala ambalo limewezesha zaidi ya watoto milioni 10.6 kujiunga na elimu ya msingi na sekondari
Mratibu wa Mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu TESP kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ignas Chonya amesema kuwa mradi huo umewawezesha walimu kuboresha mbinu za ufundishaji kupitia Tehama ambapo vyuo 35 vya ualimu vimeanganishwa na mfumo huo na wanatarajia kuunganishwa na mkongo wa Taifa.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia na kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Kuendeleza Elimu nchini (TESP) ambapo amesema mradi huo pia umewezesha kuinua kiwango cha ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari kwa kuzalisha rasilimali watu yenye ubora.
.
Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo kutoka Canada Gwen Walmsely akizungumza na wadau wa Elimu ya Ualimu jijini Arusha |
“Tunatoa shukrani nyingi sana kwa serikali ya Canada na Kitengo chao cha Global Affairs ambacho kinasimamia mradi huu, mafanikio makubwa yamepatikana kupitia mradi huu na matokeo yameshaanza kuonekana," amesisitiza Katibu Mkuu Akwilapo.
Dkt. Akwilapo amesema mafanikio ya mradi huo yameanza kuonekana ambapo walimu wameongeza uwezo katika ufundishaji na matumizi ya TEHAMA katika kufundisha.
Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo kutoka Canada Gwen Walmsley amesema kuwa Canada itaendelea kutoa fedha zaidi katika kuboresha sekta ya elimu nchini na mradi huo ni moja kati ya juhudi wanazozifanya katika kuunga mkono serikali ya Tanzania katika jitihada za kuboresha elimu.
Gwen ameipongeza Tanzania kwa kufanya Sekta ya Elimu kipaumbele ili kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, suala ambalo limewezesha zaidi ya watoto milioni 10.6 kujiunga na elimu ya msingi na sekondari
Mratibu wa Mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu TESP kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ignas Chonya amesema kuwa mradi huo umewawezesha walimu kuboresha mbinu za ufundishaji kupitia Tehama ambapo vyuo 35 vya ualimu vimeanganishwa na mfumo huo na wanatarajia kuunganishwa na mkongo wa Taifa.
Jumamosi, 8 Februari 2020
MKUTANO WA WATUMISHI WA WIZARA WALIOKO MAKAO MAKUU
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema utumishi wa umma una sheria, kanuni, taratibu, maadili na miiko ya kiutendaji ambayo kila mtumishi anapaswa kuielewa na kuzingatia katika utendaji kazi.
Katibu Mkuu Akwilapo amesema hayo wakati wa Mkutano wa Wafanyakazi wa kutathmini utendaji wa Wizara katika kipindi cha miezi sita kuanzia Julai hadi Desemba 2019 ambapo amesema ni vizuri kila mtumishi akazingatia taratibu hizo ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Amesema pamoja na kuzingatia sheria hizo ni vizuri tukafanya kazi kwa kushirikiana na kuelekezana ili kupata matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu.
Kiongozi huyo amepongeza watumishi wa Wizara hiyo kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kufikia malengo makubwa ya Wizara ambayo ni kutoa Elimu bora nchini.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. AveMaria Semakafu amesema ni vizuri watumishi wakaendeleza kasi liyopo sasa ya utendaji huku wakizingatia utendaji wenye viwango ili sekta ya Elimu iendelee kufanya vizuri.
Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Wizara Bwana Nicholaus Moshi ameupongeza Uongozi wa Wizara kwa namna unavyoweka mazingira wezeshi ya utoaji Elimu kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kuhakikisha uwepo wa vitendea kazi pamoja na ujenzi wa ofisi zikiwemo za Wathibiti Ubora wa shule na ukarabati na upanuzi wa Vyuo ya Ualimu.
Alhamisi, 6 Februari 2020
SERIKALI KUJENGA SHULE ZA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM KILA MKOA
Serikali imesema itaendelea na mpango mkakati wa kutekeleza elimu bila malipo pamoja na kutoa vipaumbele kwa watu wenye ulemavu kupata elimu iliyo bora.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu wakati wa ufungaji wa mafunzo ya TEHAMA na Teknolojia Saidizi kwa wakufunzi na walimu wa Sekondari wenye mahitaji maalum.
Dk. Semakafu amesema serikali imejipanga kuhakikisha walimu na wanafunzi wanapata elimu ya Tehama, elimu jumuishi sambamba na kujenga shule zao maalum katika kila mkoa ambapo kwa sasa wameanza na mkoa wa Katavi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akitoa maelekezo kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Tehama na Teknolojia Saidizi OUT, jijini Dar es Salaam. |
Hata hivyo awali ilielezwa kuwa tayari serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 5.9 kwa ajili ya kununua na kusambaza vifaa maalum vya kielimu saidizi katika shule za msingi na sekondari zinazopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini.
“Hii kazi pia si ndogo, napenda kwa namna ya kipekee kabisa kutumia nafasi hii kuushukuru Uongozi wa Chuo Kikuu Huria kwa kukubali kuendesha mafunzo haya hapa chuoni na kutoa wawezeshaji, vifaa pamoja na miundombinu mingine kwa ajili ya kufanikisha mafunzo haya muhimu,’’ amesema Dk. Semakafu.
Aliongeza kuwa mafunzo waliyoyapata ni muhimu kwani yatawasaidia katika matumizi ya TEHAMA kwenye ufundishaji na ujifunzaji, kutafuta rejea mbalimbali za kielektroniki kwenye mitandao na kutumia teknolojia saidizi zinazowezesha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Mwalimu wa shule ya sekondari ya Binti Mussa iliyopo Kiwalani jijini Dar es Salaam, Anna Mbogo alisema wanaishukuru kwa dhati Wizara ya Elimu kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa walimu wenye mahitaji maalum.
“Mafunzo haya yalilenga kutujengea uwezo sisi walimu kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ya sasa, pia tunaushukuru uongozi wa OUT chini ya serikali ya awamu ya tano kuonesha bayana nia ya kuwasaidia walimu wenye mahitaji maalum na kuwathamini watu wenye ulemavu kwa kuajiri watu wenye ulemavu,’’ amesema Mwalimu Anna.
MAKISATU 2020 KUENDELEA KUIBUA WABUNIFU
Serikali imesema inatambua umuhimu na mchango wa ubunifu na teknolojia katika kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2020, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema mashindano hayo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu na ugunduzi unaofanywa na watanzania.
"Lengo kubwa la MAKISATU pamoja na kukuza na kusaidia kubiasharisha, yanatoa fursa kwa wabunifu na wagunduzi wa teknolojia mbalimbali kujitangaza na kutangaza kwa wadau ubunifu unaozalishwa," amesisitiza Ole Nasha.
Mwakilishi wa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya akizungumza wakati wa Mkutano wa Waandishi wa habari kuzungumzia kuanza kwa mashindano ya MAKISATU, 2020 jijini Dodoma. |
Ole Nasha amesema MAKISATU inawalenga wabunifu kutoka makundi ya shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi stadi, vyuo vya kati, vyuo vikuu, Taasisi za utafiti na Mfumo usio rasmi.
Aliongeza kuwa kupitia MAKISATU 2019 Serikali imewaibua na kuwatambua wabunifu wachanga zaidi ya 415 huku wabunifu 60 mahiri wakiendelezwa ili ubunifu wao ufikie hatua ya kubiasharishwa.
Kiongozi huyo ametoa wito kwa watanzania wenye ubunifu mbalimbali kushiriki katika mashindani hayo na amewashukuru Benki ya CRDB kwa kukubali kufadhili mashindano hayo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa kutoka CRDB, Prosper Nambaya amesema Benki hiyo imeamua kuwa na ushirikiano endelevu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kusaidia kukuza ubunifu unaozalishwa nchini kutokana na kuwepo kwa watu wengi wenye mawazo ya kibunifu yanayopaswa kuendelezwa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)