Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo ya
awali kutoka kwa Profesa Florens Luoga (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma)
kuhusu ujenzi wa mabweni ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati
alipotembelea eneo la mradi huu muda mfupi kabla ya Rais kuwasili.Kushoto ni
Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli wakati
alipotembelea Mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna
Tarish akisalimiana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John
Pombe Magufuli wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe
Magufuli akipata maelezo kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa TBA Aktecti (Arch) Elius A.. Mwakalinga kuhusu mradi wa ujenzi wa
mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati alipotembelea Mradi huo chuoni
hapo. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe
Magufuli akikagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakati alipotembelea Mradi huo. Kushoto ni Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe. Profesa Joyce
Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akimshukuru Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa kujenga mabweni katika Chuo
kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni hatua katika kuleta ubora wa elimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe
Magufuli akizungumza na wanajumuiya ya Chuo Kikuu pamoja na Wafanyakazi wa
Mradi huo mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mabweni hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa
mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako
na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.