Ijumaa, 4 Novemba 2016

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yakabidhiwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Mkinga akimkabidhi  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish  baadhi ya nyaraka mbalimbali zinazohusu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ambavyo sasa vitakuwa vikiendeshwa na kusimamiwa  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Saimon Msanjila.


Katibu Mkuu Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akizungumza na watendaji wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  wakati wa  makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara.Makatibu wakuu wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hizo  mara baada ya makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii.

Alhamisi, 3 Novemba 2016

Wizara yakabidhi ramani ya michoro ya shule ya sekondari Nyakato


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akiwa ameshika ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Bukoba Vijijini Mwantumu Dau na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani ambaye yeye pamoja na wadau wengine wamejitolea kusaidia kukarabati baadhi ya miundombinu ya shule hiyo.  Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko


Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Majengo Tanzania Elius Mwakibinga akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera, huku Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani akishuhudia. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akimkabidhi Mkurugenzi wa Bukoba Vijijini Mwantumu Dau ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemekoKatibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mansoor induries Ltd Sharif Hirani ramani ya michoro inayokwenda kujengwa katika shule ya sekondari Nyakato iliyopo Mkoani Kagera. Shule hiyo  ni miongoni mwa shule ambazo ziliharibiwa na tetemeko


Ijumaa, 28 Oktoba 2016

Balozi wa Canada amtembelea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ofisini kwake


Balozi wa Canada Ian Myles  akisisitiza jambo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako  wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kumsalimia. Katika kikao hicho Balozi wa Canada aliahidi serikali yake kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa balozi wa Canada Ian Myles aliyefika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia Mradi wa kuboresha Elimu ya Ualimu.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Balozi wa Canada Ian Myles pamoja na Susazn Steffen Kansela Mkuu Ushirikiano na Maendeleo kutoka ubalozi wa Canada waliofika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia ushirlikiano kati ya serikali hizi mbili katika kuboresha elimu.


Wakurugenzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Gerald Mweli Kaimu Mkurugenzia wa Mipango na Sera (Mwenye shati Jeupe), Aletaulwa Ngatara Mkurugenzi Msaidizi Sera wa kwanza kulia na Mbarak Said  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifiatilia kwa makini mjadiliano kati ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Balozi wa Canada.

Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu UDSM


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Jumuiya ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Watumishi wa Serikali na wananchi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mabweni ya Chuo Kikuu cha UDSM.


      Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na Jumuiya ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Watumishi wa Serikali na wananchi waliofika kushuhudia uwekeaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa mabweni ya chuo hicho.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha UDSM wengine katika picha ni Mama Janeth Magufuri, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi na Naibu Katibu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leornad Akwilapo


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha UDSM uliofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho.


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuri, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Prof. Rwekaza Mkandara wakisikiliza kwa makini taarifa za ujenzi wa hosteli hizo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Majengo Tanzania Elius Mwakibinga (hayupo pichani)


      Baadhi ya wafanyakazi wanao husika na ujenzi wa hosteli za Chuo Kikuu cha UDSM wakimsiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuri (hayupo pichani)alipokuwa akiongea katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha UDSM uliofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho

Jumatatu, 17 Oktoba 2016WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIATAARIFA KWA UMMA

YAH: UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote  vinavyotoa shahada nchini  vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada  nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:


Katibu Mkuu

17/10/2016

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROFESA JOYCE NDALICHAKO AWAFUKUZA WALIMU 4 WALIOSHIRIKI KUMPIGA MWANAFUNZI MBEYA. 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO ametangaza kuwafukuza chuo walimu wanafunzi walioshiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi wa kidato cha TATU katika shule ya kutwa ya Sekondari mkoani MBEYA.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini DSM waziri NDALICHAKO amesema kuwa kitendo hicho ni cha kikatili, jinai na kuwa walimu hao wanafunzi hawafai kuendelea na taaluma hiyo ya ualimu na kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa.

Waziri NDALICHAKO amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanyika ni kosa la jinai na kuwa hakiwezi kufumbiwa macho.


Waziri pia ametoa onyo kali kwa wanafunzi wanaokwenda kwenye mazoezi kwa vitendo  na kuwa kwenda kinyume na taaluma, mwanafunzi wa vitendo  anakuwa amepoteza sifa hivyo amewataka  kuzingatia maadili  ya  fani na  taaluma  wanazozisomea.

Alhamisi, 8 Septemba 2016

Kaimu Kamisha Afungua Maadhimisho ya Siku ya Kisoma DunianiKaimu Kamishna wa Elimu, Nicholaus  Bureta akifungua   maadhimisho  ya siku ya Kisomo Duniani (International Literacy Day)Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish, katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Maadhimisho haya yalienda sambamba na ufunguzi wa ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu.
 Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi.Zulmira Rodriguez akimkabidhi Kaimu kamishna wa Elimu ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 
Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus Bureta akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa  wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, mashirika ya Kimataifa ya maendeleo pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wakionyesha ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu mara baada ya uzinduzi wake rasmi. Kushoto mwanzoni ni Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi.Zulmira Rodriguez.


Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus Bureta akiwakabidhi ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu baadhi ya walimu wakuu wa shule za Msingi nchini mara baada ya uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika  katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.