Waziri
wa Elimu amebainisha malengo ya mkutano huo kuainisha changamoto zinazofanana
na kubadilishana uzoefu wa namna wa kukabiliana na changamoto hizo, ambapo kwa
pamoja wanahitaji uwepo kwa elimu
jumuishi yenye usawa bila kujali wanakotoka.
Alhamisi, 16 Februari 2017
MKUTANO WA NCHI 13 ZA UKANDA WA A. MASHARIKI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDFELEO ENDELEVU SDGs4 YA ELIMU 2030
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifungua mkutano wa nchi
kumi na tatu za ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu utekelezaji wa Malengo yaMaendeo
Endelevu SDGs4 ya elimu 2030 ambao unafanyika tarehe 15/02/2017 hadi tarehe 16/02/2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Jumatatu, 6 Februari 2017
Waziri wa Elimu atoa vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika sekta ya Elimu nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Mia Saba na Nne, Mia Sita
Ishirini na Saba Elfu na Mia Nane Hamsini Na Sita (704,627,856/=) kwa
Halmashauri ya kwanza ya Kaliua Kati Ya Halmashauri zote Nchini
zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [
(P4r).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akikabidhi cheti cha ushindi kwa Halmashauri ya Kaliua iliyopata
ushindi wa kwanza Kati ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika
utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).
Jumanne, 6 Desemba 2016
Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakutana Dar
Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali ya Canada na Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa
ajili ya Ajira unaendesha warsha ya siku
tatu inayojadili Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kushirikisha mfumo shirikishi, mafunzo ya
kuendeleza ujuzi, na Masuala ya Jinsia.
Warsha hii
inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii (Bustani) inalenga kusaidia
uanzishwaji wa mfumo wa kuongeza
ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Elimu ya Ufundi na
Mafunzo ya Ufundi Stadi sekta nchini.
Wadau mbalimbali
wameshirikishwa katik warsha hii ambayo imewaleta pamoja wadau wa elimu ya ufundi
na wawakilishi mbalimbali wakubwa, mashirika mbalimbali yanayotoa elimu na
mafunzo, watu binafsi, waajiri na vyama vya waajiri, soko la ajira mashirika ya
habari na mashirika ya kiraia ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwezesha
wanafunzi wanaohitimu katika Elimu
ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi anakuwa na ujuzi wa kujiajiri na
kuajiriwa.
: Mshauri Mwandamizi wa Ufundi na mwakilishi
wa Vyuo na Taasisi zinazosaidia vyuo na
Vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi Canada Dr. Alan Copeland (aliyesimama) ambaye kwa sasa anasimamia
Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira nchini akizungumza katika warsha ya siku tatu
ya wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayofanyika jijini Dar
es Salaam inayojadia masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo.
Baadhi
ya Washiriki wa Warsha ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya
Ufundi na Mafunzo Ufundi Stadi. Warsha hii imewaleta pamoja wadau wa Elimu ya
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi
inavyoweza kufanya vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa wakiwa na ujuzi
stahiki.
Waziri wa Elimu hakutana na Ujumbe wa Benki ya Dunia
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na wajumbe
kutoka Benki ya Dunia waliofika wizarani kuongea naye masuala mbalimbali ya Elimu na jinsi ya benki hiyo
itakavyoendelea kusaidia sekta ya elimu nchini wengine katika picha ni Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Sajitha
Bashir, Cornelia Jesse na Gayle Martin kutoka Benki ya Dunia.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Elimu aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya elimu ambayo imekuwa chachu ya kuleta maboresho katika sekta ya elimu nchini. Hivyo amewaomba kuendelea kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika elimu ili kuhakikisha inaendelea kuboreshwa na kuwapa fursa watoto waengi wa Kitanzania kupata elimu iliyo bora.
Naye Mjumbe kutoka Benki ya Dunia Sajitha Bashir amemuhakikishia Waziri wa Elimu kuwa Benki ya Dunia itaendelea kufadhili miradi ya Elimu nchini pale itakapoitajika. Aidha, alisisitiza kuwa miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ni lazima itoe matokeo yanayokusudiwa
Waziri wa Elimu azindua mashindano ya Ujuzi
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Mashindano
ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika
Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa
mmoja wa washiriki wa mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills
Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.
Balozi wa Uingereza amtembelea waziri wa Elimu na kufanya mazungumzo
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako akiongea na Balozi wa Uingereza Sarah Cooke nchini aliyefika ofisini
kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu Elimu nchi. Aidha, katika mazungumz0
hayo Waziri aliishukuru Uingereza kwa kusaidia na kufadhili miradi mbalimbali
ya Elimu nchini
Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia baadhi ya taarifa kuhusu vitabu
vya lugha ya Kiingereza vinavyoandaliwa na DFID
kwa ajili ya kusambazwa kwa shuleni. Vitabu hivyo ni kwa ajili ya
wanafunzi pamoja na walimu, pichani ni Balozi wa Uingereza Sarah Cooke na
Mwakilishi wa DFID Tanya Zebioff
Alhamisi, 1 Desemba 2016
China yakabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Serikali
ya China imekabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kwa ajili ya kuwezesha wizara kufanya kazi kwa weledi. vifaa hivyo
vilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Prf. Saimon Msanjila ofisini kwake na Liu Yun
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Liu Yun alimwelezea Naibu Katibu Mkuu kuwa
wanajisikia faraja kubwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wizara kwani China na
Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa karibu sana katika sekta ya elimu hasa
katika upande wa elimu ya juu.
Vitendea
kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na Dell desk compture 6, mashine ya kudurufu
moja, scanner moja, video camera moja na komputa mpatako 10 vyote vikiwa na
thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano
Ushirikiana
huo umewezesha serikali hizi mbili kuweza kubadilishana wanafunzi wa elimu ya
juu katika fani mbali mbali. Pia alimuelezea uanzishwaji wa mafunzo ya lugha ya
kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam ambapo alisema hii ni
ishara tosha ya ushirikiano uliotukuka.
Naye
Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Yun kwa msaada huo wa vitendea kazi ambapo
alimuahidi kuwa vitafanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba inaongeza
ufanisi katika kuwahudumia wananchi wanaofika ofisi hapo kupata huduma
mbalimbali za kielimu.
Baadhi ya vtendea kazi vilivyotolewa na serikali ya China kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wa watumishi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakiweka saini makubaliano ya kupokea vifaa vilivyotolewa na China wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)