Serikali imesema haitavumilia mtu yeyote
ambaye atafanya matendo yatakayoashiria kwamba shule si mahala salama kwa
mwanafunzi, pamoja na kuwatia hofu wazazi waogope kuwaruhusu watoto kwenda
kupata Elimu.
Kauli
hiyo ya Serikali imetolewa leo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Profesa
Joyce Ndalichako siku moja baada ya kuwepo kwa taarifa juu mwalimu Respicius Patrick wa Shule ya Msingi
Kibeta iliyopo mkoani Kagera kumpiga hadi kumsababishia kifo mwanafunzi Sperius
Eradious mwenye umri wa miaka 13 wa darasa la tano.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako akiwakabidhi sheria na kanuni Wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza
la Mitihani Tanzania katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliyofanyika jijini Dar es
Salaam
Waziri
Ndalichako amesema Shule ni mahala salama kwa wanafunzi kujifunza, kitendo
hicho kilichofanywa na mwalimu huyo ni kinyume na malengo ya serikali ambayo imekuwa ikiboresha Elimu na kufanya
kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wanapata Elimu bora na tena kwenye mazingira
mazuri.
“
Suala ambalo limefanywa na huyu Mwalimu ni kinyume kabisa na maadili ambayo
Mwalimu anatakiwa kuwa nayo, kwa umri ambao mwanafunzi alikuwa nao Mwalimu
ndiyo alitakiwa awe msaada mkubwa wa kumuelimisha na kumfundisha mwanafunzi,niendelee
kuwaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu, wakati vyombo vya Sheria
vinaendelea kufanya kazi yake,” alisema Waziri Ndalichako.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wataalamu
wa waandaaji wa walimu wa somo la hesabu (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam,
ambapo amewataka walimu kuangalia namna nzuri ya kumuandaa mwanafunzi kupenda
somo la hesabu.
Katika
hatua nyingine Waziri Ndalichako amewataka wataalamu wa somo la hesabu
kuangalia namna bora ya kuimarisha ufundishaji wa somo la hilo ili kuwezesha
walimu kufundisha na kuhamasisha
wanafunzi kupenda somo hilo.
Waziri
Ndalichako amesisitiza hilo katika kongamano la tano la wataalumu wanaoandaa
walimu wa somo la hesabu Barani Afrika kuwa ni muhimu kuangalia mbinu
wanazopewa walimu wanaofundisha somo hilo kama zinawasaidia kufundisha kwa
kutumia njia shirikishi.
Kongamano
linalowakutanisha wataalamu wa hesabu linafanyika jijini Dar es Salaam kwa kwa
lengo la kuimarisha ufundishaji wa somo la hesabu ambapo mgeni rasmi katika kongiomano
hilo ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Kupitia
kongamano hilo amewataka kuangalia pia namna nzuri ya kuwezesha walimu wa
hesabu kuondoa dhana potofu kwa wanafunzi kuwa somo hilo ni gumu, na
kusisistiza kuwa mwanafunzi akielewa hesabu inamuwezesha kumudu masomo mengine
vizuri kutokanana kutumia zaidi mantiki katika kutatua hesabu.
Akiwa
jijini Dar es salam Waziri Ndalichako pia amezindua bodi ya Baraza la Mitihani
la Tanzania ambapo amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha mitihani
inaandaliwa katika ubora unaotakiwa na wahakikishe wanakuwa na umakini katika uendeshaji wa Kazi zote
zinazohusiana na mitihani.